Kwanini Waamuzi wa Tanzania hawachezeshi mechi za kimataifa?

Kasongo

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2007
Posts
3,150
Reaction score
2,273
Wapenzi na wadau wa mpira wa miguu ni matarajio yangu mlifurahi mitangani ya UEFA CL jana usiku.Nimekuwa nikifuatilia sana waamuzi wetu wa mpira wa miguu Tanzania hivi karibuni au tangu zamani kutopata nafasi ya kuchecheza michezo ya kimataifa (mbali na hii ya CECAFA) na kushindwa kupata jibu.Tatizo nini?Waamuzi wa Tanzania hawateuliwi na CAF (achana na FIFA) kuchezesha michuano ya kimataifa iwe ya vilabu au ya mataifa.Nilikuwa naangalia hii michuano inayoendelea ya CAF kwa mfano mifano.

1.Yanga v Etoile-Daresalaam,waamuzi-MSUMBIJI-Kombe la shirikisho
2.Etoile vs Yanga (marudiano),Waamuzi-UGANDA
3.Sjouliba AC de Bamako vs Accra Hearts of OAK,CAF CL,waamuzi-BURUNDI
4.Orlando Pirate Vs C.Mounana,CAF CL,waamuzi-KENYA
5.As Kaloum v Usm Alger,CAF CL,waamuzi-SUDAN
6.TP Mazembe vs Stade Malien,CAF CL,waamuzi-ZAMBIA
7.Waamuzi kutoka RWANDA wanachezesha hii michuano ya kimataifa.

Tatizo la waamuzi kutoka Tanzania nini?,wanaweza kuwa wanachezesha labda sifahamu lakini siwaoni sana kama wa nchi jirani hizi za ukanda wetu.Tujadili
 
Nashindwa kujua vigezo vinavyotumika mpaka kutowapanga kwenye michuano ya CAF kwani hata wanaopangwa ni wababaishaji kama wa kibongo mfano yule wa msumbiji aliyechezesha mechi ya YANGA Vs ETOILE.
 
Tatizo litakuwa lugha mkuu maana usifanye masiala na kiingereza mkuu, mchezaji anakuja kukulaumu sasa cjui utamjibu vp mkuu
 
Mambo ni mazuri kwa waamuzi wetu,majuzi Nkongo alichezesha na mwezi may Jonesia atachezesha Gabon vs Congo.Tunaongeza jitihada za kuinua uwezo wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…