...Uhuru Jinga... ni msamiati wenye maana pana sana.
Wenye matatizo siyo mabinti, bali ni baba zao wazazi.
Yaani mababa poa, mababa lofa, mababa wasiowajibikia maadili ya familia zao, wapo wapo tu wakidhania kupanga kwa binti na kujitegemea, wao huondolewa majukumu ya kutunza, ni ulofa halisi usio na neno mbadala la kutumia kufichia aibu hiyo.
Mababa waliokatwa ndimi kwa mahaba niue na kukabidhi nyadhifa dume kitandani kwa wake zao, wapo kupangiwa na kuongozwa.
Ni mababa wa heshima na si mababa watendaji, ni 'wanaume suruali' wa ukweli.
Hayo yote ninazungumzia makahaba wanaozalishwa kutoka kwenye milango ya ndoa tu, sina mamlaka ya kuwasemea mabinti wanaotokea kwenye milango ya single mothers.
Ni nani aliyewaambia msichana ama mwanamke hukua kwa wazazi wake na kwenda kujitegemea kwa kupanga kabla ya ndoa?
Unakuta msichana hata hajaenda kikazi 'mikoani' eti kapanga anajitegemea!
Hana kazi official huku wazazi wake wote wapo hai na wanaishi pamoja na wapo tu wakifurahi kwa kukenua meno bila kuhoji huo uozo!
Hapo utasema msichana ana matatizo, tusiwabebeshe lawama mabinti!
Binti asipopata mchumba na kuolewa, hubakia nyumbani kwa baba yake maisha yake yote.
Haruhusiwi 'kutanga na njia' kama mvulana atafutaye maisha.
Heshima ama staha ya binti ndiyo inayobeba heshima ya wazazi wake!
Kwani binti 'akizeekea' nyumbani akatulizana, kabla hajapata mume, kuna kitu anakuwa kakichelewa au kukikosa hadi akapange!
Ni maendeleo 'kabila gani' anayoyataka kwenye mapango asiyoweza kuyapata akiwa kwa wazazi wake?
Mimi binafsi binti yangu 'akifosi' kwenda kupanga huku nikiwa hai, anakuwa kanitusi na kunivua nguo hadharani.
Nitamfuta kwenye orodha ya watoto wangu, siyo kwa maneno kama wakoseavyo wazazi wengi, nitamfuta kisheria ili asiwe na baba akajitegemee vizuri apendavyo period
Sent using
Jamii Forums mobile app