KERO Kwanini wageni wanaruhusiwa kupiga picha daraja la Kigamboni huku wenyeji wakizuiwa?

KERO Kwanini wageni wanaruhusiwa kupiga picha daraja la Kigamboni huku wenyeji wakizuiwa?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Naomba kuwasilisha malalamiko kuhusu mwenendo wa baadhi ya askari polisi katika eneo la Daraja la Nyerere, Kigamboni, Dar es Salaam.

Ndugu yangu alikuwa akielekea Kigamboni kwa bajaji kwa ajili ya kutazama mazingira na alikuwa akijirekodi video akiwa njiani. Alipofika eneo la Daraja la Nyerere, alidaiwa kusimamishwa na baadhi ya askari polisi waliomtishia, kumnyang’anya simu na kufuta video pamoja na picha alizokuwa amepiga.

Kinachozua maswali ni kwamba watu wengine wamekuwa wakirekodi katika eneo hilo bila kuzuiwa, wakiwemo wageni kutoka nje ya nchi. Ikiwa kuna sheria au utaratibu unaokataza upigaji picha au video katika eneo hilo, tunaomba uwekwe wazi na utekelezwe kwa usawa kwa kila mtu bila upendeleo.

Pia tunaomba mamlaka husika zifuatilie namna matukio kama haya yanavyoshughulikiwa, kwani kumtendea mtu kama mtuhumiwa hatari au kumtisha kwa kutumia nguvu kupita kiasi kunaweza kumjengea hofu na kumdhalilisha bila sababu ya msingi.

Tunaomba ufafanuzi kuhusu utaratibu unaotumika katika maeneo kama haya na kuhakikisha haki za wananchi zinazingatiwa.
 
Back
Top Bottom