Kwanini Waingereza wanamu-underrate Wayne Rooney?

Teko Modise

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
2,331
Reaction score
7,733
Yuko wapi yule aliyesema tenda wema uende zako!

Wayne Rooney pamoja na kuvunja rekodi za kutosha kwa ngazi ya klabu yake ya zamani (Man Utd) na kwa ngazi ya timu ya taifa ya England ikiwemo kuwa Mfungaji bora wa wakati wote kwa Man Utd pamoja na England tena rekodi zote dhidi ya Sir Bobby Charlton, lakini Waingereza bado hawajawahi kuukubali uwezo na mchango wa Wayne Rooney Wazza (Pele Mweupe).

Pamoja na kucheza kwa kiwango cha hali ya juu kwa muda mrefu mfulululizo bado Rooney hatukuzwi na mashabiki waliowengi wa Kiingereza. Na majuzi ametangaza kustafu kuchezea timu ya Taifa ya England lakini Mashabiki wengi ni kama wameshukuru kwani ni kama aliwachosha. Rooney anashambulia, anakaba, anahamasisha anajitolea kwa asilimia 100.

Rooney haimbwi kama anavyoimbwa David Beckham mtu ambaye alikuwa anajua kupiga krosi tu enzi anacheza, lakini anatukuzwa kuliko Rooney. Kinachoniuma ni kwamba Nguvu zote alizotumia kuwafurahisha na kuwabeba Waingereza zimepuuzwa.

Je ni kwanini Waingereza wanamshusha na kumuona Rooney mchezaji wa kawaida licha ya kuvunja rekodi za kutosha?
 
Wikiendi ijayo anafanyiwa bonge la sherehe ya kumuaga pala Wembley.
 
Rooney hamna kitu so over rated

Slippy Gerald, you served football.
 
Tatizo mji anakotokea ndio tatizo kama angekuwa anatokea pale London au Manchester nakwambia jamaa angesifiwa sana. Rooney amezaliwa na kukulia katika mji wa wahuni wa Liverpool . Waingereza ujawafaamu vizuri wanawabuaguana ata kwa mji wanakotokea.

Nakutakia kila la heri the captain Rooney .
 

Ukweli, ni Kama unatokea London wanakueshimu kidogo, pia ni kama uko kwenye class yao (middle class and upper class) watakusaidia, lakini baadaye watakuponda. Muhimu wewe umetokea wapi kama wewe ni umetokea kwenye working class au underclass from north inabidi ujitahidi sana. Lakini media na press ya UK wanapenda sana kujenga watu na baadaye kuwabomoa, na kukuweka chini. Hivi ndivyo wanawetengeza pesa zao. Ni wanafiki sana.
 
Hii itakua dharau kubwa sana kwa Manchester, huwezi kumchongea scouser sanamu old Trafford.

Slippy Gerald, you served football.
Kwanini isiwezekane? Mchango wake ni mkubwa kuliko yeyote pale toka manchester imeundwa
 
Kwanini isiwezekane? Mchango wake ni mkubwa kuliko yeyote pale toka manchester imeundwa
Unazungumzia mchango kwenye magoli pekee au?

Slippy Gerald, you served football.
 
Kwanini isiwezekane? Mchango wake ni mkubwa kuliko yeyote pale toka manchester imeundwa
namkubali Rooney na pengine anaweza kuingia top 10 ya ma legend wa Man U ila no way awe bora zaidi ya wote kuna watu kama george best, Giggs, charlton, wapo juu yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…