Teko Modise
JF-Expert Member
- May 20, 2017
- 2,331
- 7,733
Yuko wapi yule aliyesema tenda wema uende zako!
Wayne Rooney pamoja na kuvunja rekodi za kutosha kwa ngazi ya klabu yake ya zamani (Man Utd) na kwa ngazi ya timu ya taifa ya England ikiwemo kuwa Mfungaji bora wa wakati wote kwa Man Utd pamoja na England tena rekodi zote dhidi ya Sir Bobby Charlton, lakini Waingereza bado hawajawahi kuukubali uwezo na mchango wa Wayne Rooney Wazza (Pele Mweupe).
Pamoja na kucheza kwa kiwango cha hali ya juu kwa muda mrefu mfulululizo bado Rooney hatukuzwi na mashabiki waliowengi wa Kiingereza. Na majuzi ametangaza kustafu kuchezea timu ya Taifa ya England lakini Mashabiki wengi ni kama wameshukuru kwani ni kama aliwachosha. Rooney anashambulia, anakaba, anahamasisha anajitolea kwa asilimia 100.
Rooney haimbwi kama anavyoimbwa David Beckham mtu ambaye alikuwa anajua kupiga krosi tu enzi anacheza, lakini anatukuzwa kuliko Rooney. Kinachoniuma ni kwamba Nguvu zote alizotumia kuwafurahisha na kuwabeba Waingereza zimepuuzwa.
Je ni kwanini Waingereza wanamshusha na kumuona Rooney mchezaji wa kawaida licha ya kuvunja rekodi za kutosha?