Mkuu
Mkandara,
Nimekusoma hapo juu na kukuelewa vema tu ingawa umeondoka katika nyuzi yako iliyopita ambayo niliikubali kabisa.
Nyuzi ile ulizungumzia kuwa sensa itumike katika kupanga maendeleo ya taifa na si vinginevyo.
Kipengele cha dini katika sensa sina tatizo nacho kwani ni sehemu ya 'dermograph' ya taifa.
Baada ya kusema hivyo narudi kwenye msimamo wangu wa kila mara kuwa jambo lolote linaloashiria kuvunja umoja wa kitaifa sikubalini nalo.
Mimi kama wewe naamini kuwa wakoloni wote waliofika nchini walitugawa kwa makundi hata kama walikuwa na thamani walizokuja. Ni matokeo hayo ndiyo yanatufanya tusiongelee utaifa na kubaki kuongelea katika imani kitu kinachopswa kuwa cha mtu binafsi.
Kabla sijajenga hoja yangu naomba kusema kuwa haki ni kitu kimoja na kupigania haki ni kitu kingine, na jinsi ya kupigania haki ni kitu kingine. Unaweza kuwa na haki lakini kama hujui haki ipo wapi na jinsi ya kuipata basi utajikuta huna haki. Ndiyo maana hata kama mtu anajua ana haki bado atamweka mtu mweledi (lawyer) kusimamia hiyo haki.
Ni ngumu lakini nitaeleweka kadri ninavyosonga mbele.
Natambua kuwa kuzuia kipengele cha dini si kuogopa kuweka wazi kisichojulikana. Ni jitihada za kuzuia mitafaraku inayoweza kutokea kutokana na baadhi ya watu kutumia mwanya huo kujenga hoja za uzushi, uongo na fitna.
Ni kutokana na watu kupinda ukweli kwa kutumia data.
Tatizo la Waislam ni mchanganyiko wa mambo kadhaa. Nasema tatizo la waislam kwa kuzingatia malalamiko ya hoja zao
Kwanza, Waislam hawatafuti chazo cha matatizo yanayowakabili.
Pili, hawakubali ukweli wa chanzo cha matatizo.
Tatu, wanatafuta njia za mkato kutatua matatizo yao.
Nne, hawakubali kuwa tatizo lipo miongoni mwao na usuluhishi upo miongoni mwao na wanaamini kuwa kutafuta suluhu ya bandia ni njia muafaka.
Tano, Wameachia agenda za issue zao kwa mashabiki na sio watu wenye weledi.
Nina uhakika umesoma maandiko mengi ya waandishi wa kiislam akiwemo Mzee Mohamed Said. Ms kwa mfano, amejenga hoja mara nyingi sana kuonyesha wingi wa waislam ingawa hakuna anayehoji wapi alipata data. Mwaka jana ametoa data hizo hizo katika makongamano hata kama ilikuwa za mwaka 1957, si kwasababu ya kujenga hoja bali kujenga hoja kwa kusaidiwa na wingi wa watu. Mara nyingi sana hoja zake hupoteza mashiko kwasababu hazisimami zenyewe zinasimama kwa kutegemea kitu kingine.
MS anaposema waislam kwa sensa ni wengi na ndio wameachwa nyuma kieleimu na madaraka, hapa anaongelea Quantity. Asichoongelea ni Quality. Ndio maana Mohamed Sosshi hapo juu nimemuuliza, aliposema waislam wengi waliandikisha watoto baada ya uhuru lakini bado wamebaki nyuma licha ya wingi wao,je hao wengi walimaliza shule? walifaulu? walirudi kuisadia jamii yao? Hakuwa na jibu.
Pengine kwa kutumia dhana ya MS yeye anaamini kuwa unaweza kuwa na waziri kwasababu umeandikisha watoto shule hata kama hawajamaliza au kufaulu. Nimetoa mfano wa Kilwa, nikauliza shule inapofungwa kwa kukosa wanafunzi unategemea lini utapata mwalimu, bwana shamba au mhasibu miaka 10 ijayo? Sikupata jibu kwasababu ninaongelea source na nilipaswa niongelee matokeo!!
Hoja ya sensa inaposhikwa na akina Ponda kwa msaada wa wasomi washabiki wengine inapoteza nguvu kwasababu haijengwi katika mantiki zaidi ya ushabiki na uchochezi usio na weledi.
Wanapojenga hoja kuwa tunataka tujue idadi ili tuone uwezekano wa kujiunga na OIC kwasababu ya wingi, ni kosa.
Hivi waislam wakiwa 50% wakristo 30% na wapagani na wasioamini 20% hiyo inatosha kushawishi umma kuwa sasa ni wakati wa kujiunga na OIC?
Wanapojenga hoja kuwa maeneo yaliyo na waislam yameachwa nyuma makusudi, akatokea mtu na kueleza shule zilivyo na matatizo ya kukosa wanafunzi Kilwa, je, hoja hapo inasimama?
Wanapojenga hoja kuwa hakuna mkuu wa NECTA tangu uhuru, akatokea mtu na kuonyesha shule yenye watoto 250 na mwalimu mmoja, je, hoja ina mashiko hapo.
Tatizo ni mkuu wa NECTA au wanafunzi 250 wasiosoma na kufaulu?
Kama watu watajenga hoja za kisayansi zinazoonyesha umuhimu wa kipengele cha dini nadhani kila dini watakubaliana na hilo. Hoja hizo zinapojengwa kwasababu rahisi na za kishabiki zinapoteza nguvu yake. Hapo ndipo tatizo lilipo.
Kwanini mtu alenge data za wakristo na asije nazake kuonyesha mbadala! Kwanini mtu aseme wakristo ni kadha asitaje wapagani ambao ni wengi sana kuliko wakristo na waislam. Narudia wapagani na waisoamini ni wengi sana kuliko waislam na wakristo. Atakayetaka ufafanuzi aniulize!
Nimalizie kwa kusema, Ponda na masheikh kama Halifa na akina Mohamed Said wamekuwa wakimlaani sana Nyerere kwa mambo kama ya kuondoa sensa. Hatujasikia wakisema Kikwete bali wanakwepa kwa kutumia serikali.
Ni hawa wanaosema CCM inaongoza vema, na ni hao hao walisema CCM imewakandamiza waislam kwa kutumia TANU na yenyewe mwaka 2000 na 1995. Na ndio hao hao wanaongoza zoezi la kususia sensa.
Narudi kwenye nukta zangu za awali kuwa kuna tatizo, suluhu si kutafuta mchawi au njia za mkato ni kulikabili tatizo kuanzaia chanzo. Nitue hapa kwanza.