Kwanini wajasiriamali wengi matajiri hawakumaliza masomo yao ya elimu ya juu?

Na mimi naacha shule mazima
Lengo sio kuacha shule, bali ni kufikia mafanikio kwa njia yoyote ile iliyo halali na pasipo kuvunja sheria. Hivyo usiache shule mkuu, shule ni muhimu sana.
 
Nataka ujiulize swali la pili katika hao matajili kwanini branding name za business zao zina uhusioano na namba ya mpinga kristo, 666.
Mkuu tujadili mbinu zitakazotutoa hapa tulipo na kufikia mafanikio, Hivyo nashauri tuweke pembeni masuala ya imani. Maana tunaweza kwenda mbali kwa kusema kila mwenye mafanikio anahusiana na imani kama za Freemasons, Antichrist, nguvu za giza nk. .....

Tuelezee matatizo yanayotuzuia kufikia mafanikio na namna ya kutatua matatizo hayo.
 
Mimi namtazamo tofauti kidogo na wadau wengine waliochangia ,kwanza nakubaliana na mtoa mada kwamba matajiri wengi ni watu waliokatiza masomo yao hata hapa kwetu ni hivyo mtazamo wangu ni huu: 1, moja ya nguzo ya biashara ni mtaji, lakini mtaji ni zaidi ya pesa taslimu kuna suala la kujiamini ,ujasiri, uzoefu, na uvumilivu na ubunifu , watu hawa ukiwafuatilia maisha yao ya kila siku lazima vt hivyo wanavyo, labla tuongelee suala moja la uzoefu; watu hawa wanapoka shule wanapata changamoto nyingi kutimiza ndoto zao ,kufeli ktk mipango yao ni jambo ambalo wamepitia sana jambo lililowapa uzoefu mkubwa na hasa ukichukulia wana ujasiri ndani yao, hawakati tamaa na wameacha shule ili watimize ndoto yao , sasa muda wa kupanda na kushuka ni sawa na kusoma phd katika masuala ya biashara ,wakati wewe mostly unasoma kwa nadharia huku ukifundishwa risk management ambayo inakupa tahadhari nyingi kabla ya kuamua, hawa watu tayari wanakua wanazikabiri risk kwa vitendo, .unapotoka shule unakuja kuajiriwa na kampuni za watu hawa ziwe international au local kama bakhresa etc,
Lakini jambo hili haliondoi umuhimu wa elimu kwani mwisho wa siku wanapokua kibiashara wanahitaji wasomi na taaluma mbalimbali kuendsha shughuli zao.
Jambo la msingi ni kujua watu wa aina hii wapo waliozaliwa na karama za Mwenyezi Mungu na wapo ambao njia za maisha zimewapeleka huko pia lazima kizazi na kizazi katika dunia hutokea jamii ya watu wenye mtazamo tofauti na wengine lakini husimamia maamuzi yao na kufanikiwa haijalishi amefeli mara ngapi , ili dunia iende ni lazima iwepo hasi na chanya, zikivutana ,ila usjaribu hasi wala chanya kama ww ni baridi , usiwe katikati chagua moja ,and you have to think big!!!!
 
Kusoma sana ni utumwa.
Mimi nikishamaliza hiki kibachelor sisomi tena,kwani nataka kuvumbua nini kipya!!
ahahahaaa ni kweli kak ila uwe umejpanga vya kutosha maana kutoboa sio mtaji tu kunahtaji uondoe uoga wa kufail maisha na usiwe mvivu pia uwe mbunifu saana..maana ata ukianglia hyo mifano apo juu hawakusema mm nkmalza bachelor sisomi tena,yaan wao waliacha chuo kabla ata kumalza bachelor ila waliamin na waltumia nguvu kbwa kutoboa..maisha ya kiafrica ukshafka apo tu wee kama na elimu yko ndo itakutoa boss ila mm nna mfano wa mshkaji alivomaliza 4m 6 yey akakataa kwenda chuo sas hvi ana miliki maduka ya hardware mwanza na hostel za gharama saut zinamfanya achukue hadi mkopo wa mil.200 bank
 



Ni kwa sababu hawa walikuwa na vipaji vya hajabu, si kila kilaza yuko hivi. Tizama hapa Bongo watu waliokacha shule wanavyoishi. Wengi wamejiingizza kwenye gemu la kukopi na kupaste (fleva), wengine wauwaji kwa ajili ya kusambaza sembe ili watajirike, na wengine makahaba huko Bongo muvi.
 
Nilichojifunza ni kwamba wote wameacha wakiwa chuo kikuu
Sasa wewe acha ukiwa form 3'
Alafu iko wazi mfumo wa chuo si suportive saana kwa watu wenye
IQ kubwa coz they are always independent ...hata wakihitimu huwa wanakuwa wamegombana sana na wakufunzi wao
 
Kusoma si kosa ila kusoma sana ndio tatizo! Unakuta mtu akishapata 1st degree anajiona yeye ndo wa daraja la juu, anawaza white colar jobs. Kusoma kwa ajili ya kuja kuwa mtumwa wa ajira ni ujinga. Elimu Masters degree, Mshahara 1000k kabla ya makato, umri miaka 40, bado kujenga, kusomesha ndugu na watoto na unataka ku mantain maisha ya u-masters holder ili uonekane wa juu, kustaafu bado miaka 20tu. Mshahara kupandishiwa mpaka maandamanona migomo. ElimikaZinduka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…