Kwanini wajasiriamali wengi matajiri hawakumaliza masomo yao ya elimu ya juu?

Kwanini wajasiriamali wengi matajiri hawakumaliza masomo yao ya elimu ya juu?

Na mimi naacha shule mazima
Lengo sio kuacha shule, bali ni kufikia mafanikio kwa njia yoyote ile iliyo halali na pasipo kuvunja sheria. Hivyo usiache shule mkuu, shule ni muhimu sana.
 
Nataka ujiulize swali la pili katika hao matajili kwanini branding name za business zao zina uhusioano na namba ya mpinga kristo, 666.
Mkuu tujadili mbinu zitakazotutoa hapa tulipo na kufikia mafanikio, Hivyo nashauri tuweke pembeni masuala ya imani. Maana tunaweza kwenda mbali kwa kusema kila mwenye mafanikio anahusiana na imani kama za Freemasons, Antichrist, nguvu za giza nk. .....

Tuelezee matatizo yanayotuzuia kufikia mafanikio na namna ya kutatua matatizo hayo.
 
Mimi namtazamo tofauti kidogo na wadau wengine waliochangia ,kwanza nakubaliana na mtoa mada kwamba matajiri wengi ni watu waliokatiza masomo yao hata hapa kwetu ni hivyo mtazamo wangu ni huu: 1, moja ya nguzo ya biashara ni mtaji, lakini mtaji ni zaidi ya pesa taslimu kuna suala la kujiamini ,ujasiri, uzoefu, na uvumilivu na ubunifu , watu hawa ukiwafuatilia maisha yao ya kila siku lazima vt hivyo wanavyo, labla tuongelee suala moja la uzoefu; watu hawa wanapoka shule wanapata changamoto nyingi kutimiza ndoto zao ,kufeli ktk mipango yao ni jambo ambalo wamepitia sana jambo lililowapa uzoefu mkubwa na hasa ukichukulia wana ujasiri ndani yao, hawakati tamaa na wameacha shule ili watimize ndoto yao , sasa muda wa kupanda na kushuka ni sawa na kusoma phd katika masuala ya biashara ,wakati wewe mostly unasoma kwa nadharia huku ukifundishwa risk management ambayo inakupa tahadhari nyingi kabla ya kuamua, hawa watu tayari wanakua wanazikabiri risk kwa vitendo, .unapotoka shule unakuja kuajiriwa na kampuni za watu hawa ziwe international au local kama bakhresa etc,
Lakini jambo hili haliondoi umuhimu wa elimu kwani mwisho wa siku wanapokua kibiashara wanahitaji wasomi na taaluma mbalimbali kuendsha shughuli zao.
Jambo la msingi ni kujua watu wa aina hii wapo waliozaliwa na karama za Mwenyezi Mungu na wapo ambao njia za maisha zimewapeleka huko pia lazima kizazi na kizazi katika dunia hutokea jamii ya watu wenye mtazamo tofauti na wengine lakini husimamia maamuzi yao na kufanikiwa haijalishi amefeli mara ngapi , ili dunia iende ni lazima iwepo hasi na chanya, zikivutana ,ila usjaribu hasi wala chanya kama ww ni baridi , usiwe katikati chagua moja ,and you have to think big!!!!
 
Kusoma sana ni utumwa.
Mimi nikishamaliza hiki kibachelor sisomi tena,kwani nataka kuvumbua nini kipya!!
ahahahaaa ni kweli kak ila uwe umejpanga vya kutosha maana kutoboa sio mtaji tu kunahtaji uondoe uoga wa kufail maisha na usiwe mvivu pia uwe mbunifu saana..maana ata ukianglia hyo mifano apo juu hawakusema mm nkmalza bachelor sisomi tena,yaan wao waliacha chuo kabla ata kumalza bachelor ila waliamin na waltumia nguvu kbwa kutoboa..maisha ya kiafrica ukshafka apo tu wee kama na elimu yko ndo itakutoa boss ila mm nna mfano wa mshkaji alivomaliza 4m 6 yey akakataa kwenda chuo sas hvi ana miliki maduka ya hardware mwanza na hostel za gharama saut zinamfanya achukue hadi mkopo wa mil.200 bank
 
Lengo la huu uzi si kuhamasisha watu kuachana na masomo bali ni kujadili kwa pamoja njia walizotumia baadhi ya wanafunzi walioacha shule hadi kufikia mafanikio. Kumbuka kuna wengine waliacha shule na hawakufikia mafanikio yoyote pia kuna wengine waliendelea na shule hadi kuhitimu tena kwa madaraja/ufaulu mzuri lakini pia hawakufanikiwa kutimiza malengo yao. Wana JF hebu tujadili kwa pamoja mambo mbalimbali yanayoweza kutuletea mafanikio kwa kutumia mifano michache ya hawa waliofanikiwa tena bila kusoma vyuo vikuu. Ili kusiwe na kisingizio cha elimu hebu tujadili mambo ya msingi yanayoweza kutufanikisha katika malengo yetu. Bila kubagua waliosoma na wasiosoma maana wote wanahitaji mafanikio.

Kwa miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia ongezeko kubwa la wasomi na wahitihu wa elimu ya juu katika vyuo tofautitofauti, na kupelekea ongezeko kubwa la ukosefu wa ajira katika maeneo mengi duniani. Hapa nchini pia tatizo la ajira ni kubwa sana kuliko watu wanavyolichukulia. Sasa tunawezaje kujiendeleza na kutimiza malengo yetu na kuwa na maisha mazuri kwa kutumia njia mbadala ya kupata ajira kupitia ujasiriamali?


HOWEVER, there list of people who dropped out and didn't succeed / lost opportunities because of that is much much larger. Your Degree is like a little savings account for a rainy day: when you really need it - you'll be able to fall back on it. What if your 1st or 2nd idea doesn't pan out and you need something in between while you are getting ready for your 3rd idea? So stay in school 🙂

  • Bill Gates - moja kati ya waanzilishi wa Microsoft - utajiri wake ni $78.8 Billion. Aliacha chuo cha kikuu cha Harvard akiwa na miaka 19.
main-qimg-8134578f383b3d72eda1385f55e440eb

  • Steve Jobs - muanzilishi mwandamizi wa kampuni ya Apple Inc - Jumla ya utajiri wake $8.3 Billion - Aliacha chuo baada ya kusoma muhula mmoja (semester)
main-qimg-920965f940a4c52853a4093cac3abc90

  • Mark Zuckerberg - CEO na moja kati ya waazilishi wa mtandao wa kijamii wa Facebook - Jumla ya utajiri wake $33.7 Billion - Aliacha chuo (Harvard) akiwa na miaka
main-qimg-a41266fb0c885e90971f0466d679519f

  • Michael Dell - Mwanzilishi wa komputa za Dell (Dell Computers) - Jumla ya utajiri wake $20.1 Billion - Aliacha chuo cha Texas akiwa na miaka 19.
main-qimg-22f74daa89f410a771139f99e2ccc6c9

  • Larry Ellison - moja kati ya mwanzilishi na CEO wa zamani wa kampuni ya Oracle - Jumla ya utajiri wake ni $47.6 Billion - Aliacha chuo kikuu cha Chicago akiwa na miaka 20.
main-qimg-3b75f0bf7c8fece58124bb191b7683e8

  • Jan Koum- CEO na mwanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Whatsapp - Jumla ya utajiri wake ni $8.6 Billion - Aliacha chuo kikuu cha San Jose akiwa na umri wa miaka 20.
main-qimg-79afca2f881528be6dde56ebf6241d1f

  • Travis Kalanick - CEO and moja kaji ya waanzilishi wa kampuni ya kimtandao ya Uber - Jumla ya utajiri wake ni $6.2 Billion - aliacha chuo cha UCLA akiwa na miaka 21.
main-qimg-bafaed08b87de6e957e1fc30c8a5f5c5

  • Evan Williams - moja kati ya waanzilishi na CEO wa zamani wa mtandao wa kijamii wa oftwitter - Jumla ya utajiri wake ni $1.71 Billion - Aliacha chuo kikuu cha Nebraska–Lincoln akiwa na miaka 20.
main-qimg-2455683d084d80ab2683bb9a63cffec6

  • John Mackey -mwanzilishi wa kampuni ya Whole Foods - utajiri wake ni $ 100 million - Aliacha chuo kikuu chaTexas - Austin akiwa na miaka 22.
main-qimg-aa25479794f58e24ef2c878a0108cd22

  • Paul Allen - moja kati ya waaanzilishi wa kampuni ya Microsoft - Utajiri wake $17.7 billion - Aliacha chuo kikuu cha Washington State University akiwa na miaka 20.
main-qimg-2b5ef0dc3548e37f4ac5bd950f880830

  • Dustin Moskovitz - Moja kati ya waanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Facebook - Utajiri wake $9.2 Billion - Aliacha chuo Harvard
main-qimg-af19f5ec3dc170ef79703bb603ff740f

  • Leslie Wexner - CEO wa L Brands - Utajiri wake ni $7.2 Billion - Aliacha chuo kikuu cha Ohio State
main-qimg-59b3939ebe84fd2bfec37a4bd48a49cf

  • Elizabeth Holmes - CEO na mwanzilishi wa Theranos - Net Worth $3.6 Billion - Aliacha chuo kikuu cha Stanford
main-qimg-636b9b347cd059443c3c8cd1c851bb16

  • Jack Dorsey - CEO na moja kati ya wanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Twitter- Utajiri wake ni $2.3 Billion - Aliacha chuo kikuu cha New York.
main-qimg-b8b3fa41140b9473449b70a74c6edece

  • Gabe Newell - moja kati ya waazilishi na managing director wa kampuni ya gemu za video ya Valve - Utajiri wake ni $1.3 Billion – Aliacha chuo kikuu cha Harvard.
main-qimg-6898d68c8a5d78c621e734f0de5e9ac4

  • Stacey Ferreira - mwanzilishi wa Forrge and moja kati ya waanzilishi wa Mysocialcloud - Aliacha chuo kikuu cha New York - Anamiaka 23 !
main-qimg-bf0741528a538b7785575cfe0fe4bfd9

  • Ralph Lauren - Mwanzilishi wa shirika la Ralph Lauren - Utajiri wake ni $5.6 billion - Aliacha chuo cha Baruch.
main-qimg-8edb484b45ecbce5b2971878c00f8b5e

  • Evan Spiegel - CEO na moja kati ya waanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Snapchat - Utajiri wake ni $2.1 billion - Aliacha chuo kikuu cha Stanford.
main-qimg-44e82a40faf2d29ca016bff528995de0

  • Sheldon Adelson - Mwanzilishi wa shirika Las Vegas Sands - Utajiri wa $25.8 billion - Aliacha chuo cha City College of New York
main-qimg-48ebacfdf3a575a1bc2901f415541ff9

Images source: Wikipedia and google images

Kwahisani ya Quora



Ni kwa sababu hawa walikuwa na vipaji vya hajabu, si kila kilaza yuko hivi. Tizama hapa Bongo watu waliokacha shule wanavyoishi. Wengi wamejiingizza kwenye gemu la kukopi na kupaste (fleva), wengine wauwaji kwa ajili ya kusambaza sembe ili watajirike, na wengine makahaba huko Bongo muvi.
 
Nilichojifunza ni kwamba wote wameacha wakiwa chuo kikuu
Sasa wewe acha ukiwa form 3'
Alafu iko wazi mfumo wa chuo si suportive saana kwa watu wenye
IQ kubwa coz they are always independent ...hata wakihitimu huwa wanakuwa wamegombana sana na wakufunzi wao
 
Kusoma si kosa ila kusoma sana ndio tatizo! Unakuta mtu akishapata 1st degree anajiona yeye ndo wa daraja la juu, anawaza white colar jobs. Kusoma kwa ajili ya kuja kuwa mtumwa wa ajira ni ujinga. Elimu Masters degree, Mshahara 1000k kabla ya makato, umri miaka 40, bado kujenga, kusomesha ndugu na watoto na unataka ku mantain maisha ya u-masters holder ili uonekane wa juu, kustaafu bado miaka 20tu. Mshahara kupandishiwa mpaka maandamanona migomo. ElimikaZinduka.
 
Back
Top Bottom