Kama hujaolewa ukivaa zile pete ni sawa na kujifungia bahati ya kuolewa. Ni kisirani hicho. Mwanaume ambaye yuko serious na mwenye heshima akishaona mtu amevaa pete huwa anakuwa na heshima naye. Kama sasa utakuwa umevaa pete hizo na bado kuna jamaa anakutafuta kimapenzi ujue ni fataki huyo au wale wanaume ambao huwa hawaheshimu ndoa za wengine. Hivyo basi kama ikitokea akikuoa basi fahamu atakuwa pia anafuata wenye pete wengine maana inaonekana ni tabia yake sugu kupenda wenye pete.
Hata kama umri utapita ninaamini kama una tabia nzuri bado utampata mume tu, mbona kuna mabinti nawafahamu wameolewa mid 30s na wengine hata 40s. Hata miaka 50 ikipita utaolewa japo na mzee mwenzio mzeeshane pamoja. Imagine mbona wajane huwa wanaolewa tu tena na watoto wa kufikia wanao? Jiheshimu utapata mume, usijifunge na mipete hiyo.