Kwanini wajivalishe pete za ndoa na uchumba

Kwanini wajivalishe pete za ndoa na uchumba

Haya mimi sipingi kwani nimeona mtu mmoja alikuwa na pete jamaa alimpenda sasa jamaa akawa anajirusha nae siku ya siku huyo msichana analetewa kadi ya harusi jamaa anakwenda kuoa msichana hiyo presha juu na kulazwa alipoulizwa sababu alisema alijua yeye ndo ataolewa alipoulizwa jamaa akasema huyo ni mke wa mtu angalia amevaa pete. Alipoulizwa huyo msichana hana jibu. Basi kwa kifupi wanajipunguzia nafasi ya kupata bwana
 
Kama hujaolewa ukivaa zile pete ni sawa na kujifungia bahati ya kuolewa. Ni kisirani hicho. Mwanaume ambaye yuko serious na mwenye heshima akishaona mtu amevaa pete huwa anakuwa na heshima naye. Kama sasa utakuwa umevaa pete hizo na bado kuna jamaa anakutafuta kimapenzi ujue ni fataki huyo au wale wanaume ambao huwa hawaheshimu ndoa za wengine. Hivyo basi kama ikitokea akikuoa basi fahamu atakuwa pia anafuata wenye pete wengine maana inaonekana ni tabia yake sugu kupenda wenye pete.

Hata kama umri utapita ninaamini kama una tabia nzuri bado utampata mume tu, mbona kuna mabinti nawafahamu wameolewa mid 30s na wengine hata 40s. Hata miaka 50 ikipita utaolewa japo na mzee mwenzio mzeeshane pamoja. Imagine mbona wajane huwa wanaolewa tu tena na watoto wa kufikia wanao? Jiheshimu utapata mume, usijifunge na mipete hiyo.
 
Kwa kweli hata mimi najiuliza ya nini kujivisha mapete kibao vidoleni lakini nakosa jibu. Kwa uzoefu wangu naona wanawake ndio wanapenda sana kuzivaa hasa mbili. Nadhani kwao inawaongezea hadhi fulani na hata heshima mbele za jamii inayowazunguka. Japo ni gharama kuyanunua kwani lazima litakuwa la gold au silver.........!!!!!! Lakini kwa upande mwingine kwa mafataki hupendelea zaidi wake za watu kwa kukwepa gharama kwani anajua hata kama sitaweza kumhudumia vizuri financially yupo wa ku-cover hiyo gap
 
wengi wao wanaona umri umeenda na ngoma bila bila kwa hiyo wana pretend wako occupied kumbe kila cku wanalala na msongo wa mawazo na wamekumbatia mto.wengi wao ukiongea nao wanakuwa na kahasira fulani hivi kasiko na chanzo.
 
ni kweli mkuu kila mmoja na sababu zake ila wengi wanakuwa na waume za watu

Hiyo ndo sababu nzito. pamoja na kuwa kila mtu ana sababu zake lakini inasemekana kwamba wanaume wengi hasa waliooa wanapenda kuwa na wake za watu, nadhani ni katika kupunguza usumbufu. kwa hiyo wale wasioolewa wanaona ni bora wajivalishe pete ili kuwatia hao waume za watu
 
Back
Top Bottom