Tangu ongezeko la tozo kwa mitandao ya simu, mawakala wengi hususani Tigo Pesa na M Pesa wamekua wakigoma mtu kutoa pesa akiwa nje ya eneo la ofisi zao.
Jamaa yangu alikua anataka kunitumia pesa akashauri niende kwa wakala ili atoe hapo na nichukue pesa.
Wakala akakataa kwa hoja mtoaji yupo mkoa mwingine hivyo atapata kiasi kidogo sana. Ikabidi jamaa anitumie kwenye simu yangu ili nitoe.
Lakini leo kuna mtu nimemtuma kitu na akapungukiwa pesa nikaamua aende kwa wakala wa Tigo pesa ili nitoe pesa achukulie hapo lakini takribani wakala wote wamekataa wakimwambia atumiwe pesa na atoe yeye.
Nipo Mkoa mmoja na ninayetaka achukue pesa. Hivyo hoja ya kuwa mkoa mwingine haikuwepo.
Sijajua kwa nini wamekataa. Suala la miamala ya simu imekua na changamoto nyingi kwa sasa
Mwenye kujua atujuze.