Kwanini wakala wa Tigo Pesa, M-pesa, Airtel Money hawataki pesa itolewe na mtu wa mbali?

Kwanini wakala wa Tigo Pesa, M-pesa, Airtel Money hawataki pesa itolewe na mtu wa mbali?

Na mimi nasema tangu tozo zianze huwa natuma pesa moja kwa moja kupitia wakala pia huwa natoa kwa wakala alie umbali wa km 1000, na mtandao ni mmojawapo wa iliotajwa.
 
Hapo wanataka kuwapiga mara mbili.

Kuna wakala namfahamu, yeye nampa cash na namba ya kutuma, na anatuma bila shida.

Ingekuwa halipwi commission asingekuwa anakataa kutuma hizo hela ambazo anatuma almost kila weekend.

Na kama hawalipwi commission ingeonesha wakati wanataka ku-confirm kutuma pesa.
 
Huyo anayetoa kutoka mkoa mwingine akipiga simu kwa mtandao husika na kusema amekosea namba ya wakala ni rahisi hiyo hela kurudishwa kwani itaonekana ametoa hela kwa wakala ambaye yuko mbali na yeye so kuna chances kubwa kuwa amekosea na huo muamala utazuiwa fasta.

Mawakala wengi kama hamjuani huu ujanja ujanja hawafanyi.
 
Hiyo ni miamala isiyo na Commision kwasasa so Mitandao husika watakupa kamisheni kwa miamala waliyoruhusu tu.

Miamala iliyoruhusiwa ni ipi?

Ni miamala yote inayofanyika location(eneo) 1 kati ya wakala na mteja.

Mteja akiwa bukoba wakala akiwa Dar Huo muamala wakala akiufanya ni kajitolea tu kama sadaka ila Hapati hata senti.

Vigezo na Masharti kuzingatiwa.
 
Hapo wanataka kuwapiga mara mbili.

Kuna wakala namfahamu, yeye nampa cash na namba ya kutuma, na anatuma bila shida.

Ingekuwa halipwi commission asingekuwa anakataa kutuma hizo hela ambazo anatuma almost kila weekend.

Na kama hawalipwi commission ingeonesha wakati wanataka ku-confirm kutuma pesa.
Hawalipwi! na Yawezekana hajui kama Halipwi! Akijua Halipwi itakua mwisho kukusaidia.

Ukiona anaendelea kukusaidia ujue huyo wakala mmeivana so anakusaidia ki itu tu ila sio kwamba hajui kama anachofanya hapati FAIDA.
 
Utaratibu wa Kifedha ni Umhudumie mtu unaemuona,
Kama Wakala utamwambia atume pesa kwa mtu aliye Mbali ni amekufanyia Msaada tu,
Pili ambalo nahis ndo inatakiwa iwe moja ni Kuepuka Matapeli,
Mfano,
Ukiwa Dar na ukatoa pesa kwa wakala labda wa Kigoma ni Rahisi sana wew mtoa pesa wa Dar kupiga simu kweny kampuni husika na ukadanganya kwamba umekosea Muamala nia yako ilikuwa kutoa kwa wakala wa Dar,na Kampuni bila hiyana itakusikiliza na kuamua kukurudishia Muamala wako ambao kiuhalia ulishautoa kupitia mtu wa Kigoma kwa Maan wataangalia na Distance yako na kule ulikotoa pesa na kuamin kwamba kweli umekosea,
Hyo hali inamsababishia Hasara wakala kwa Sababu atalipa au atakatwa pesa ambayo yeye hajaitumia.
Sasa ili kuepuka hyo Wakala anashauriwa kumhudumia mtu anaemuona
 
Huku kwetu unaenda kwa wakali unamtoa chake then anakutumia hela popote pale unapotaka
 
Hebu Soma Terms and Condition
Tigo Pesa Tariffs | Tigo Tanzania (sorry Moderator nimeweka link ili kuelimisha.
Kipengele cha pili Kinamtaka Mtoaji na Muwekaji Fedha kwa wakala kuonyesha KItambulisho Chake. Sasa Wakala uko naye Mwanza unataka mtu wa Dar atoe Hela, hicho kitambulisho atakionaje?

Mitandao yetu ya simu wangeboresha huduma kama safaricom….mpesa ya safaricom ukitaka kutoa au kuweka na uko mbali na wakala inagoma moja kwa moja….inakupa ujumbe kuwa upo mbali na wakala!
 
Mkuu Wewe ni wakala au unataka ligi,Mimi ni wakala na nimeandika uhalisia
Kwamba unataka kutuaminisha mtu ambaye siyo wakala hawezi kujuwa jambo hili?

Kwamba sijawahi kufika Marekani ndio nisijuwe New York iko Marekani?

Kwani kutapeliwa si wajinga wengi tu kila siku wanatapeliwa kwa kutumiwa msg ile ela tuma kwenye namba hii na wajinga wanatuma kweli bila confirmation ya ujumbe umetoka kwa nani.
 
Hiyo ni miamala isiyo na Commision kwasasa so Mitandao husika watakupa kamisheni kwa miamala waliyoruhusu tu.

Miamala iliyoruhusiwa ni ipi?

Ni miamala yote inayofanyika location(eneo) 1 kati ya wakala na mteja.

Mteja akiwa bukoba wakala akiwa Dar Huo muamala wakala akiufanya ni kajitolea tu kama sadaka ila Hapati hata senti.

Vigezo na Masharti kuzingatiwa.
Hivi ni kweli ulimdhulumu yule dada laki kadhaa?je umemlipa?Nilikuwa na mume wangu siku ile tunasoma wote akasikitika sana wewe kula hela ya mwanamke akasema unajitafutia laana tu.
Kama hujamrudishia ni vyema ukamrudishia.
 
Amemdhulumu mwanamke atapata laana!!?
Heehhee.....
Kwani anaestaili kudhulumiwa ni mwanaume tu!?
 
Nachojua Mimi taratibu haziruhusu na pia mtu akitoa pesa kama yupo mbali ni rahisi kwa wakala kutapeliwa kwani mtandao huangalia location ya mtoaji na mpkokeaji
LA pili voda wanaitaji mapato wakukate unapotuma wakate inapotoa
 
Nakuelewesha, kwa msaada wa wengi.

Juu ya swala la kutoa kwa wakala, kwa mteja aliyepo mbali.
Hili wanalikataa kwa sababu ya usalama na kuepuka kutapeliwa.
Wateja wengine ni wajanja na hiyo ni mbinu yao ya kupiga fedha kirahisi.

Anaenda kwa wakala, anamuambia anatoa pesa. Anamtumia mwenzake aliyepo mbali, madhalani mkoa mwingine. Mwenzake akishatoa, anapewa cash na wakala, anaondoka.
Akishaondoka, yule aliyetoa pesa anapiga simu huduma kwa wateja kuomba fedha zirudishwe kwa sababu katoa kimakosa.

Huduma kwa mteja wanachofanya wanakupigia nawe kuuliza huku mmeunganishwa na mteja husika. Bila shaka utasema ulimhudumia mteja na ulimpa cash.

Mteja ataulizwa na atakataa kata kata. Wanachofanya huduma kwa wateja, wanaangalia mteja ametolea fedha wapi na wakala yupo wapi. Kama mteja alikuwa mbali, yeye atarudishiwa fedha.

Wakala utafata taratibu za kisheria kudai hela yako. Mfano, kupeleka shitaka polisi ukiwa umeambatanisha na kitabu alichosaini mteja akiwa anachukua fedha, kilicho na namba ya simu, na namba ya kitambulisho pamoja na namba ya muamala.

Bahati mbaya sana, wateja hawataki kusaini na hivyo hutokuwa na kithibitisho. Maana yake umekula hasara kama wakala.
 
Na hii ndo sababu hasa, wasipoelewa na hapa hakuna namna tena ya kuelewa
 
Juu ya swala la kumuwekea mteja aliyepo mbali.

Hii ni kutokana na wakala kutopata malipo 'Commision' ya huduma anayofanya.

Twende kidogo kidogo. Mteja anapoweka fedha kwenye simu yake, kiasi chote cha pesa kinaingia kwenye account yake bila kupunjwa hata mia. Je, commission ya wakala anayemuwekea mteja fedha mtandao husika inapata wapi?

Commission inapatikana kwa fedha atakayokwatwa mteja pindi atakapotoa fedha au kufanya malipo.

Kiasi anachokatwa mteja anapotoa fedha, inagawanywa katika msusuru wa watoa huduma. Wakala aliyetuma, wakala atayemtolea mteja, wakala Mkuu aliyemhudumia wakala wa kawaida, serikali (VAT), Vodacom nao wapate chao.

Sasa kilichopo ni kuwa, kuna kitu kinaitwa transaction boundaries. Yaani mipaka ya miamala.

Yaani kumuingilia mtu katika mpaka wake wa kufanya biashara.
Kila mkoa ina muwakilishi Mkuu wa mtandao husika. Sasa miamala inayotoka nje inamnyima ufanyaji wa biashara. Hivyo, wakala hatalipwa Commision.

Ukitaka kuelewa, angalia ufanyaji wa biashara wa viwanda vya vinywaji. Hawaingiliani.
 
Nakuelewesha, kwa msaada wa wengi.

Juu ya swala la kutoa kwa wakala, kwa mteja aliyepo mbali.
Hili wanalikataa kwa sababu ya usalama na kuepuka kutapeliwa.
Wateja wengine ni wajanja na hiyo ni mbinu yao ya kupiga fedha kirahisi.

Anaenda kwa wakala, anamuambia anatoa pesa. Anamtumia mwenzake aliyepo mbali, madhalani mkoa mwingine. Mwenzake akishatoa, anapewa cash na wakala, anaondoka.
Akishaondoka, yule aliyetoa pesa anapiga simu huduma kwa wateja kuomba fedha zirudishwe kwa sababu katoa kimakosa.

Huduma kwa mteja wanachofanya wanakupigia nawe kuuliza huku mmeunganishwa na mteja husika. Bila shaka utasema ulimhudumia mteja na ulimpa cash.

Mteja ataulizwa na atakataa kata kata. Wanachofanya huduma kwa wateja, wanaangalia mteja ametolea fedha wapi na wakala yupo wapi. Kama mteja alikuwa mbali, yeye atarudishiwa fedha.

Wakala utafata taratibu za kisheria kudai hela yako. Mfano, kupeleka shitaka polisi ukiwa umeambatanisha na kitabu alichosaini mteja akiwa anachukua fedha, kilicho na namba ya simu, na namba ya kitambulisho pamoja na namba ya muamala.

Bahati mbaya sana, wateja hawataki kusaini na hivyo hutokuwa na kithibitisho. Maana yake umekula hasara kama wakala.
Wewe ndiye Wakala pekee unayejitambua.. maelezo yako yameleweka
 
Tangu ongezeko la tozo kwa mitandao ya simu, mawakala wengi hususani Tigo Pesa na M Pesa wamekua wakigoma mtu kutoa pesa akiwa nje ya eneo la ofisi zao.

Jamaa yangu alikua anataka kunitumia pesa akashauri niende kwa wakala ili atoe hapo na nichukue pesa.

Wakala akakataa kwa hoja mtoaji yupo mkoa mwingine hivyo atapata kiasi kidogo sana. Ikabidi jamaa anitumie kwenye simu yangu ili nitoe.

Lakini leo kuna mtu nimemtuma kitu na akapungukiwa pesa nikaamua aende kwa wakala wa Tigo pesa ili nitoe pesa achukulie hapo lakini takribani wakala wote wamekataa wakimwambia atumiwe pesa na atoe yeye.

Nipo Mkoa mmoja na ninayetaka achukue pesa. Hivyo hoja ya kuwa mkoa mwingine haikuwepo.

Sijajua kwa nini wamekataa. Suala la miamala ya simu imekua na changamoto nyingi kwa sasa

Mwenye kujua atujuze.
Sababu ni kuwa watakosa fedha kupitia makato... Fikiria..
1. Unaweka hela bure
2. Unapomtumia mtu, mtumaji unakatwa.... na hii ndo wanayoikosa
 
Back
Top Bottom