Kwanini wakala wa Tigo Pesa, M-pesa, Airtel Money hawataki pesa itolewe na mtu wa mbali?

Kutoa hela mbali haikubaliki kwa sababu matapeli wanatumia hii mbinu kuiba:

Tapeli yupo Mwanza, wala haendi kwa wakala, anawasiliana na tapeli mwingine Dar na kumwambia aende kwa wakala. Huyu tapeli wa Mwanza anapewa details za wakala - namba ya kutolea hela, anafanya mwamala kutoa hela kwa wakala aliyepo Dar. Transaction inafanyika Mwanza, hela anachukua tapeli aliyepo Dar. Baada ya tapeli aliyepo Dar kuchukua hela, huyu tapeli wa Mwanza anapiga simu kwenye mtandao husika, tuseme Tigo, na kuwaambia kuwa amekosea kutoa hela anaomba irudishwe.

Wahudumu wa mtandao husika wakiangalia kwenye mfumo wao wataona ni kweli huyu mtu yupo Mwanza lakini amefanya transaction ambayo imeenda kwa wakala aliyepo Dar.

Wahudumu na mitandao ambayo haipo makini mara kadhaa wamesababisha mawakala kuibiwa kwa namna hii kwa sababu huwa wanazuia miamala ya namna hiyo na kumrudishia hela tapeli (wa Mwanza).

Ningependa kupata maelezo kutoka mitandao ya simu namna wanavyoshughulikia hili tatizo la utapeli.

Sababu zingine kama vile transaction boundaries na mgawanyo wa faida kati ya wakala, wakala mkuu, serikali na mtandao husika zimekwishaelezwa na wadau.
 
Nafikiri hili pia wangeliangalia. Either wakatae kuwa mtoaji yuko mbali na mtoa huduma ya uwakala au mteja mtoaji atoe code ya wakala aliyepo karibu kama namba zina uelekeo wa kufanana na aliyepo mbali.
 
Wapo wanaokataa hata kumwekea mtu aliyeko mkoa mwingine, wapo wanaokubali kutoa hata kama uko mkoa mwingine. Voda wangetwambia kanununi ni ipi
Kanuni ni anahudumiwa aliyepo ofisini
 
Kikubwa cha kutotia huduma hiyo kwa mteja alieko mbali in achangiwa na mambo matatu muhimu
1. Haishauriwi kwenye muongozo
2. Kamisheni kuounguzwa
3. Sababu za kiutapeli
Replay sababu unayotaka hapo nikupe ufafanuzi vizuri
 
Hitimisho ilkua nini?
wanataka umtumie ndugu(kuna makato-A) kisha ndugu ndiyo akatoe kwa wakala(kuna makato-B)
ukituma(kwa kutoa) moja kwa moja kwa wakala wa mbali, makato-A yatakosekana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…