Na ni Mtanzania!
Kwa hivyo hata nynyi hii lugha hamuijui sana kwa ufasaha mnavyodai. Yeye si wa kwanza kumuona akiandika hicho Kiswahili.
Sisi kwetu kuchanganya hili lugha na ndimi zingine hakumaanishi hatulijui. Tazama utafiti zinazoonyesha ya kwamba wanafunzi wa Kenya hufanya vyema katika somo la Kiswahili kuliko.wa Tanzania.
Ni vipi basi wakenya wengi zaidi ya watanzania wameajiriwa na makampuni ya teknolojia kama Facebook, Microsoft ama Google kutafsiri maagizo za programu zao kwa Kiswahili? Hata maprofesa wengi wanaofunza lugha hii katika vyuo kadhaa ni wakenya- wengi wao!
Ni dhahiri ya kwamba wakenya ndio wanaobobea katika lugha hili, na ndio walio kwenye mstari wa mbele kabisa kuendeleza lugha hili.
Lugha tunaifaham, tatizo kubwa linalotusibu ni kutokuwa makini pale tunapotumia lugha ya maandishi (written) na lugha ya maongezi (oral/spoken).
Watanzania wengi hatuko makini kwenya written language (sio kiswahili tu, ni lugha nyingi tunapuuzia vitu vya msingi),
Lakini pia kwa sababu ya asili (mother tongue) inachagiza suala hilo! Hapa tz kuna makabila mengi sana, kuna baadhi ya makabila wao wanachezesha sana ndimi zao, hivyo "R" inatamkwa haraka zaidi kuliko L, wengine ndo hivyo hawezi kutumia R badala yake huweka L kila sehemu, iko mifano mingi!
Hata hivyo hii haiondoi dhana kwamba hatukijui hata hicho kiswahili, La hasha! Ni kukosa umakini tu kwa baadhi ya watu!
Suala la Wakenya kuajiriwa kwa wingi na makampuni makubwa ya kimataifa lina sababu nyingi!
Tuanzie kwenye ile video ya kwanza inayozungumzia maisha ya Yesu, baada ya Mkenya mmoja kuwa amepata tenda ya kuingiza maneno ya Kiswahili kwenye video ile, jamii ya kimataifa iliifahamu Kenya kama kitovu cha kiswahili na hapo ndo nyota yenu iling'aa! Lakini kiswahili kilichoingizwa kilikuwa hakijanyooka!
Baada ya hapo hao Wakenya wachache walikuwa ni kivutio kwa wenzao, zikitokea nafasi huko walikuwa wanawataarifu haraka wakenya wenzao hivyo wakajikuta wakiongezeka!
Lakini kama unafuatilia vizuri masuala, wakati Facebook wametoa tenda kwa wakenya kutengeneza Menu ya kiswahili, waliomba msaada kwa watanzania ili kuingiza kiswahili kilichonyooka! Mtu kama Prof Masamba amefanya kazi kubwa tu ya kutengeneza ile menu!
Pamoja na hayo mambo nihitimishe kwa kusema, Kiswahili sio cha Tanzania pekee, ni cha Africa Mashariki na kati! Kwa hiyo hata kama ni Mkenya au Mtanzania au Mrundi anakikuza nje ya mpaka ni jambo jema! Zaidi ni kuona kiswahili kikikua!