Kwanini Wakenya hawajui kiswahili!!!

Kiswahili chako ni kibovu kuliko hata hao wakenya jitafakari kwanza kumbuka unapomnyooshea mwenzako kidole vitatu vinakutizama wewe
 
Abomination!
Wewe bwana hebu acha porojo! Huyo anamshinda mleta mada lakini sio wengine! Nashangaa unamsifia kwa lipi wakati huo ujumbe wake alioandika umejaa makosa mengi ya kisarufi!

Au basi tupe mtihani wa wazi mimi na MK254
Haha ati abomination?


Tafadhali usiombe kushindana na Mkenya kwa mtihani wa Kiswahili cha makaratasi, hapo atakushinda vibaya . Kiswahili cha kuzungumza ndio pengine......


Btw, ningependa kumsikiliza MK254 akizungumza Kiswahili, is it as poetic as vile huziporomosha humu Jf?
 
Kama huamini weka open test hapa tufanye mimi na MK254,

Wewe unamsifia wakati mimi naona kuna makosa kwenye uandishi wake, hatusemi maana sio malengo ya jukwaa!


Kama huamini subiri comment ya MK254 inayofuata hapa utaona makosa ya kisarufi.
 
Kama huamini weka open test hapa tufanye mimi na MK254,

Wewe unamsifia wakati mimi naona kuna makosa kwenye uandishi wake, hatusemi maana sio malengo ya jukwaa!


Kama huamini subiri comment ya MK254 inayofuata hapa utaona makosa ya kisarufi.
Wewe unaangalia makosa madogo ya kisarufi badala ya mpangilio na mtiririko wake wa maneno? Jamaa ako sawa despite hizo makosa madogo. Hata watanzania kama mwanzilishi wa hii thread hufanya makoaa katika uandishi na maongezi.

Anyway, mimi siko sawa sana kwenye lugha ya Kiswahili, ni kuhitahidi tu. Siwezi kusimamia hiyo open test kati yenyu.
Hivi sasa ninasoma kijimagazine flani hapa ya hawa maWitnesses wa Jehova, imeandikwa kwa Kiswahili safi sana, napenda wanavyochanganua mambo flani ya kisayansi hapa.
 


Ahhaaaaa umenikumbusha vijarida vya hao jamaa, nahisi hapo utakuwa unasoma kile cha "Mnara wa mlinzi"[emoji23] [emoji23] [emoji23]

Back to the topic, Hata mimi nakubali na kuuthamini uwezo wake kwenye lugha ya kiswahili, mwanzoni nilijua ni mtu wa pwani, lakini niliona hapa kama sio wa huko!

Kuhusu kuangalia hayo makosa madogo madogo ni kwa sababu tunaangalia sarufi (grammar) na ndio kazi yake kuona kama sentensi iko katika mtindo na muuundo unaotakiwa!

Ingekuwa tunaangalia ufahamu hapo wala huwezi kujihusisha na grammar, unaangalia tu mantiki ya mtu na kuelewa, na hiki ndicho tunachokifanya kila siku hapa!


Yaani ni sawa ukipewa swali la essay sidhani kama msahihishaji atakukata alama kwa kukosea mtindo au muundo wa sentensi, badala yake ataangalia tu ufahamu na mawazo yako katoka swala husika na kukupa alama! Hii ni tofauti na kwenye sarufi, kosa kidogo huna alama!


Kuhusu huyu mwanzilishi wa uzi, huyu wala sio mtu wa kuandika sana, ni mwongeaji mzuri tu kama vijana wa nai wanavyobonga sheng
 
we mwenyewe umechapia uzi wako wote mpaka unatia kichefu chefu
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 

Hehehehe!! Kawaida huwa naendana na matabaka yote, ukinikuta kwa Wapemba kule Zanzibar huwa natiririka Kiswahili chao hadi raha, halafu nikiibukia Dar nawabadilishia kwa lafudhi yao ya Wazaramo. Nikigeuza na kurudi Nairobi natema yai mjini hadi basi, na nikiwa kitaa Nrb nawashushia sheng kwa raha zangu.
Japo sheng ya siku hizi kidogo hunichanganya....vijana wamebuni maneno mapya hadi nahisi kama nimezeeka vile.
 

Wewe jamaa inaonekana ni mpenda sifa sana.

Anyway next week nakuja nairobery tuongee hiyo accent ya kizenji.
 
Kiswahili cha zenji huwezi hata kidogo wewe kama unabisha basi reply hapa kwa hicho kiswahili cha visiwa vya karafuu tuone huo umahiri wako[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Umeshawasikiliza wakenya wangapi mpaka kuhitimisha kuwa hawajui Kiswahili? Ina maana wewe hujawahi kukutana na watanzania wasioweza kuzungumza Kiswahili fasaha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…