Kwanini Wakerewe wengi hawapendi kujenga nyumba Ukerewe?

Msiogope jamani, mbona mimi nipo na ndugu zangu hata wa ulaya wanakuja tu na tunawachinjia ng'ombe na mbuzi walionona na hawapatwi na balaa lolote? Hamjui na sisi wakerewe sa ivi tumekuwa kama wachaga, kila december lazima waje nyumbani na wote wanarudi salama mijini kwao bila hata kudhurika?

iVle vibibi vilishaisha, kweli walikuwepo wabibi ukifika tu anataka ajue ratiba yako yote. anaweza akakuuliza 'okubha oli hanu mpaka lihi?' yaani utakuwepo mpaka lini. Ukimwambia obhwoyo bhumo (wiki moja) basi kamati yao ya ufundi inaweza ikakujadili na ikiwezekana unaweza ukawa chizi ama ukafa tu ghafla!

Ila yalishaisha jamani muwe mnakuja nyumbani tu
 

Kweli mkuu! Wasalimie La Bima na Porax!
 

Wameanza kubadirika sasa! Angalia vitu vipya kama : Holiday in motel, Gallu motel, La Bima, Porax, Pius Msekwa Complex, Ua la jangwani, Ua la waridi, kaseni Beach n.k
 

mmh! Mi sirudi tena huko. Wanaweza kunitumia mamba.
 
Wanga sijui wachawi walintesa sana (Ukerewe-Murutunguru) enzi za utoto (5 - 12 yrs) nashkuru tulivyokuja kuhama hadi leo nalala kwa amani usiku.
 
Wanga sijui wachawi walintesa sana (Ukerewe-Murutunguru) enzi za utoto (5 - 12 yrs) nashkuru tulivyokuja kuhama hadi leo nalala kwa amani usiku.

Pole sana mkuu.
lakini pale Bugolola safiiii, hakuna upuuzi .
Hamia pale.
 

Mabagala, unanikumbusha mbali, nilikuwa nikienda home likizo hilo swali la utakuwepo mpaka lini nilikuwa naambiwa kabisa kabla sijafika kule nijibu vipi, yaani wakati natoka dsm kwenda huko naambiwa ukiulizwa upo mpaka lini mi nijibu nipo sana tu, halafu ghafla tu after a week huyo natimua zangu, ila sikujua reason behind kumbe ndo hiyo umeisema hapo juu. Ila nina miaka mingi sijaenda ngoja mwakani nifanye mpango wa kutembelea tena UK, maana nyumbani ni nyumbani tu hata kama kuna wanga.
 

Osaka kwani siku hizi wilaya ya Ukerewe ina Umeme wa Gridi ya Taifa au? Maana mi siku nyingi sana tangu nitoke huko ila taarifa za Umeme kufika huko sina, hebu nihabarishe ndugu. Maana umeme ndio maendeleo, ila sasa tukajenge nyumbani nyumba za maana.
 
Wameanza kubadirika sasa! Angalia vitu vipya kama : Holiday in motel, Gallu motel, La Bima, Porax, Pius Msekwa Complex, Ua la jangwani, Ua la waridi, kaseni Beach n.k

Osaka kama una picha ya hivyo vitu vipya kama Holiday In Motel, La Bima, Porax na Pius Msekwa Complex hebu tuwekee humu tujionee.
 
Pole sana mkuu.
lakini pale Bugolola safiiii, hakuna upuuzi .
Hamia pale.

Ahsante mkuu, ila nimepaniss Ukerewe nna kumbukumbu nyingi za utoto nshawahi kulewa mapuya nkiwa darasa la pili na kuna jogoo mtaani lilikuwa likiniona mimi lazima linikimbize liniparue yaani ilikuwa "Why always me" ka Baloteli ila nadhani ni wachawi haohao walikuwa wananiandama hadi mchana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…