gwantemala
Member
- Aug 9, 2016
- 22
- 5
Du kumbe Wajaluo ni watu wazima?Somehow Wakikuyu wanafikiri Wajaluo si wanaume kwa sababu utamaduni/ mila zao haiwaruhusu kukata govi la uume.
Kuna mikoa mingi tu TZ tohara ni option, kwa kanda ya ziwa ukiacha wakurya na baadhi ya makabila madogo madogo ya mkoa wa Mara, kagera, Mwanza,Shinyanga, Tabora na hata IringaDu kumbe Wajaluo ni watu wazima?
Haha haha...am not Luo bt do I say..Du kumbe Wajaluo ni watu wazima?
Hawa jamaa ni wa ajabu sana. Marekani imeweza kupata Rais Mjaluo ila Kenya inashindikana, why!!!?Walete hao ni lazima tuwashauri ili maisha yaendelee mpaka sasa hawako salama kwa kuwa na dhambi ya ubaguzi bado inawatafuna kwanini wanasema wazi wazi kuwa waluo kamwe awatali kenya wakati ni wakenya kama wakenya wengine?
Wewe palipoandikwa ya kuwa lazima Kenya iwe na rais mjaluo ni wapi,kitabu gani hicgo?Quraan,Bibilia au ni Bhagavad Vita?Unaongelea mjaluo gani kwanza Ken Okoth,Dalmas Otieno,Raphael Tuju au nani ndo atawa rais mjaluo wa kwanza?Wacha ushabik wa kijuha wewe!Tumekuwa na waziri wakuu wawili,wametoka kabila gani?Kabila izo zingine 44 kati ya 47 watapata rais wa kabila lao lini?Wacha kujifanya unaelewa Kenya na wakenya,hujui hata ng'o!Hawa jamaa ni wa ajabu sana. Marekani imeweza kupata Rais Mjaluo ila Kenya inashindikana, why!!!?
Wakikuyu na wajaluo ni mandugu, na ni jambo la kawaida sana kwa mandugu kutofautiana kwa mambo fulani.Wala si jambo geni ya kuwa Rais wa kwanza Kenya alikuwa ni JARAMOGI OGINGA ODINGA maana yeye ndiye aliyesaini mkataba wa uhuru kule UN wakati Kenyatta akiwa gerezani na akatamka ya kuwa Uhuru na Kenyatta leo hii wakikuyu wamegeuka mbogo kwa waluo kiasi cha kuwachukia na kufika hatua kuwaua viongozi wao kama akina TOM MBOYA'ROBERT OUKO nk wenginewe wengi tu inakuaje na sasa anapambana na Raila tuwasaidije hawa jamaa zetu?
Hii kali, kwani kuna govi la sehemu nyingine tofauti na uume?Somehow Wakikuyu wanafikiri Wajaluo si wanaume kwa sababu utamaduni/ mila zao haiwaruhusu kukata govi la uume.
Kuna govi la akili au ubongo.Ukifanikiwa kukata govi hilo si unakuwa mtu mzima tu?Hayo mengine ya sijui kungolewa meno,kuchanjwa au hata kukatwa 'govi la uume',hahaha,hayana maana yeyote!Hii kali, kwani kuna govi la sehemu nyingine tofauti na uume?
Well said brother wanasiasa sio watu kabisa na ni kikundi cha watu wachache ambao ndio wanafaidika na rasilimali za nchi ndio wanayozua yote haya na chuki haiwi ya upande mmoja lazima iwe na pande mbili..... Ila chuki ya kenya ipo hapo ilipo sababu wanasiasa walishashinda vita ya kuwatenganisha watu na hii ni faida kwao ila mwisho wa siku kila kitu kina mwisho na ipo siku mwisho wa chuki utaisha..... So shemeji zangu tulieni endeleeni kupiga kazi mjenge kenya yenu ili siku moja mseme no to tribalism...Wakikuyu na wajaluo ni mandugu, na ni jambo la kawaida sana kwa mandugu kutofautiana kwa mambo fulani.
Umekosea hapo sana kwenye hilo swali lako, ambalo ndicho kichwa cha mada "ni kwanini wakikuyu wanawachukia wajaluo". Mbona isiwe ni wajaluo kuwachukia wakikuyu> Swali lako ingekuwa ni je, ni kwanini wajaluo na wakikuyu hawapendani au ni kwanini makabila za Kenya hazipendani? Hapo haungesemekana kuegemea upande wowote kama inavyoonekana kwenye hilo wazo lako hapo juu.
Ningependa kutofautiana kabisa na hizo kauli za Juakali1980 na Tim Choice ambao wanasema ni kwasababu wajaluo hawatairi. Wajaluo sio kabila pekee Kenya lisilotairi. Mbona basi kumekua na uhasama baina ya wakikuyu na wakalenjin ambao pia wanatairi?
Jambo linalozua huu ugomvi wote ni siasa mbaya ya kuwagawanya makabila kwa misingi ya kikabila na wanasias. Ni hili la kueneza dhana ya kuwa kabila hili na lile ni tishio kwa malengo yetu ya maendeleo kama jamii, kwa hivyo ni lazma tuwapinge.
Lakini mwisho wa siku, hawa wote ni wakenya, na wananchi wa kawaida hujikuta kutangamana tu vyema. Wananchi wa kawaida wanaishi tu pamoja kama mandugu, wanafanya kazi pamoja, wanabudu pamoja, kula pamoja kwenye mikahawa, wanachumbiana, kusoma pamoja, wakiwa wagonjwa wanenda kwenye mahospitali sawa. Matatizo tunazuexperience ni sawa.
Wakikuyu na wajaluo hawachukiani haswa, ni mivutano tu baina ya wanasiasa.
I hope umenielewa.