Wakikuyu na wajaluo ni mandugu, na ni jambo la kawaida sana kwa mandugu kutofautiana kwa mambo fulani.
Umekosea hapo sana kwenye hilo swali lako, ambalo ndicho kichwa cha mada "ni kwanini wakikuyu wanawachukia wajaluo". Mbona isiwe ni wajaluo kuwachukia wakikuyu> Swali lako ingekuwa ni je, ni kwanini wajaluo na wakikuyu hawapendani au ni kwanini makabila za Kenya hazipendani? Hapo haungesemekana kuegemea upande wowote kama inavyoonekana kwenye hilo wazo lako hapo juu.
Ningependa kutofautiana kabisa na hizo kauli za
Juakali1980 na
Tim Choice ambao wanasema ni kwasababu wajaluo hawatairi. Wajaluo sio kabila pekee Kenya lisilotairi. Mbona basi kumekua na uhasama baina ya wakikuyu na wakalenjin ambao pia wanatairi?
Jambo linalozua huu ugomvi wote ni siasa mbaya ya kuwagawanya makabila kwa misingi ya kikabila na wanasias. Ni hili la kueneza dhana ya kuwa kabila hili na lile ni tishio kwa malengo yetu ya maendeleo kama jamii, kwa hivyo ni lazma tuwapinge.
Lakini mwisho wa siku, hawa wote ni wakenya, na wananchi wa kawaida hujikuta kutangamana tu vyema. Wananchi wa kawaida wanaishi tu pamoja kama mandugu, wanafanya kazi pamoja, wanabudu pamoja, kula pamoja kwenye mikahawa, wanachumbiana, kusoma pamoja, wakiwa wagonjwa wanenda kwenye mahospitali sawa. Matatizo tunazuexperience ni sawa.
Wakikuyu na wajaluo hawachukiani haswa, ni mivutano tu baina ya wanasiasa.
I hope umenielewa.