Kwanini Wakristo na Waislamu wa zamani walichukulia utumwa kama jambo la kawaida ni sio uovu?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Wakristo na Waislamu waliomiliki watumwa kabla biashara ya utumwa haijakomeshwa walikuwa watu wema wa dini zao au waovu watakaochomwa moto?

Kwa nini inaonekana watu wa hizi dini kubwa mbili walikuwa wanachukulia utumwa kama jambo la kawaida tu hapo zamani? Hawakuwa na utashi(conscience)??
 
Mungu wetu ni Mungu wa majeshi ,mfano Mungu aliruhusu wanaisraeli wakae utumwani Misri miaka kadhaa.
Pia baada ya kuwatoa utumwani Misri kwa Mungu mwenyewe kuwapigania wakiongozwa na Musa na Haruni..Mungu aliwapa nchi ya ahadi Kanani lakini hiyo nchi waliyopewa ilikuwa na watu ,Mungu aliruhusu wapigane vita aliwapigania kuna sehemu Mungu aliruhusu wachukue mateka ILI WAWAFANYE WATUMWA WAO.
Lakini kuna sheria nyingi za kuishi nanhao watumwa kwa kuwajali na kutokuwonea.
HATA SISI tunavyoishi na ma hose boy na ma beki tatu,shamba boy,walinzi tuishi nao vizuri kwa kuwajali kama sehemu ya familia.
KWANINI Mungu aliruhusu baadhi ya watu waingie utumwani/wawe watumwa.
ADHABU kwa wale waliomuasi Mungu hata wana Israel wenyewe walishawahi kuwa watumwa Misri.
Adhabu inaweza ikawa kwa kosa walilofanya mababu na mabau vizazi hata vinne vilivyotangulia(kama laana)
Lakini watumwa wakitubu dhambi zao na kuomba Mungu rehema na toba .Mungu huwatoa utumwani.
 
Attachments

  • images - 2024-11-11T002807.668.jpeg
    images - 2024-11-11T002807.668.jpeg
    11.6 KB · Views: 5

Mpaka keo utumwa upo umebadilika jina tu.
 
utumwa
 
Hapo nyumbani kwako unaye house girl au house boy au tuseme tu mfanyakazi? Fuatilia maana halisi ya neno 'slave' utaona hao watu wapo...
Waliokuja kuharibu ni wale mean bosses wanaotesa wafanyakazi wao au kuwafanyisha kazi bila malipo.. unaeza kuta hata wewe ni mtumwa.
 
Kuna baadhi ya verse kwenye biblia zinasema wazi "Enyi watumwa watiini bwana Zenu."
Kuna nyingine inasema iwapo mtumwa wako utampiga Hadi kuharibu jicho utamuacha aende zake maana wee ndiwe umempa ulemavu.

Kwa muktadha huu vitabu vililenga utumwa uonekane wa maana sana asee!
Usisahau pia kutaja andiko linalosema, Mpende jirani yako kama nafsi yako.

Mathayo 7:12 Basi yoyote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.

Ukristu haukuutuza utumwa, bali ulikuwa ukiwaongoza Wakristu waliokuwa wakiishi katika tajamani za kitumwa (civilization of slavery), kwenda katika njia bora zaidi ya hapo.

Ndiyo maana Paulo Mtume anasema pamoja na kwamba zamani Mungu aliruhusu mambo haya, sasa anawaagiza watu wote waufuate mwenendo bora (Matendo 17:20).
 
Wakristo na Waislamu waliomiliki watumwa kabla biashara ya utumwa haijakomeshwa walikuwa watu wema wa dini zao au waovu watakaochomwa moto?

Kwa nini inaonekana watu wa hizi dini kubwa mbili walikuwa wanachukulia utumwa kama jambo la kawaida tu hapo zamani? Hawakuwa na utashi(conscience)??
Kwa sababu moral consciousness ya jamii ya wakati huo haikuona utumwa kuwa kitu cha ajabu sana, ingawa kuna watu waliokuwa wakisema kuwa utumwa si sahihi.

Ni kama vile ambavyo inawezekana watu wa miaka ijayo inawezekana wataacha kuchinja wanyama na kula nyama halafu kutushangaa kwa nini watu wa wakati huu tulikuwa tunachinja wanyama na kuwala nyama, moral consciousness ya jamii yetu haijafikia kuona kuchinja wanyama kama jambo baya hivyo, ingawa kuna watu wanaoona kula nyama si kitu sahihi.
 
Hapo nyumbani kwako unaye house girl au house boy au tuseme tu mfanyakazi? Fuatilia maana halisi ya neno 'slave' utaona hao watu wapo...
Waliokuja kuharibu ni wale mean bosses wanaotesa wafanyakazi wao au kuwafanyisha kazi bila malipo.. unaeza kuta hata wewe ni mtumwa.
Acheni kutetea upuuzi....nyie...
Utumwa wa biblia sio utumwa wa housegal. Housegal analipwa, ana uhuru wa kusepa, hurusiwi kumlipa, hujamnunua kama bidhaa dukani...
Utumwa kwenye biblia umeelezwa kabisa namna ya kukamata, kununua, kupiga, etc watumwa...
Acheni kutetea ujinga someni biblia yenu na mkubali walioandika ni binadamu kama nyie hamna Cha mungu hapo
 
Mbona utumwa mpaka leo upo.
sema sasa hivi ni kibarua na vijakazi wa ndani.
Na hata maofisi pia ni utumwa
 
Niniwa sababu ya uhaguzi na kujiona bora kama dini zao. Kama walikubali kuacha dini mila hata majina yao ulitegemea nini? The Curse of Salvation
 
Mungu wetu ni Mungu wa majeshi ,mfano Mungu aliruhusu wanaisraeli wakae utumwani Misri miaka kadhaa.
Pia baada ya kuwatoa utumwani Misri kwa Mungu mwenyewe kuwapigania wakiongozwa na Musa na Haruni..Mungu aliwapa nchi ya ahadi Kanani lakini hiyo nchi waliyopewa ilikuwa na watu ,Mungu aliruhusu wapigane vita aliwapigania kuna sehemu Mungu aliruhusu wachukue mateka ILI WAWAFANYE WATUMWA WAO.
Lakini kuna sheria nyingi za kuishi nanhao watumwa kwa kuwajali na kutokuwonea.
HATA SISI tunavyoishi na ma hose boy na ma beki tatu,shamba boy,walinzi tuishi nao vizuri kwa kuwajali kama sehemu ya familia.
KWANINI Mungu aliruhusu baadhi ya watu waingie utumwani/wawe watumwa.
ADHABU kwa wale waliomuasi Mungu hata wana Israel wenyewe walishawahi kuwa watumwa Misri.
Adhabu inaweza ikawa kwa kosa walilofanya mababu na mabau vizazi hata vinne vilivyotangulia(kama laana)
Lakini watumwa wakitubu dhambi zao na kuomba Mungu rehema na toba .Mungu huwatoa utumwani.
Waafrika walimuasi lini Mungu wakati walikutana na Ukristo kwa mara ya kwanza baada ya wazungu kufika Africa na hapo hapo wakaanza kukamatwa kama Watumwa??
Hao Wakristo waliokuwa wanawachukua watumwa kwa nguvu walikuwa wanaesabihiwa kama waovu au wenye dhambi??
 
Mbona utumwa mpaka leo upo.
sema sasa hivi ni kibarua na vijakazi wa ndani.
Na hata maofisi pia ni utumwa
Huelewei maana ya utumwa, housegirl au houseboy wa leo wanachagua hiyo kazi kwa hiyari/ridhaa yao wenyewe, hakamatwi kwa kuwindwa na bunduki kama walivyokuwa wanafanya Waarabu.
 
Hapo nyumbani kwako unaye house girl au house boy au tuseme tu mfanyakazi? Fuatilia maana halisi ya neno 'slave' utaona hao watu wapo...
Waliokuja kuharibu ni wale mean bosses wanaotesa wafanyakazi wao au kuwafanyisha kazi bila malipo.. unaeza kuta hata wewe ni mtumwa.
Utumwa watu walikuwa wanakamatwa na wanalazimishwa kufanya kazi kwa bunduki, vitanzi vya kunyongea na mijeledi. Housegirl, Houseboy na wewe mwenye kipato cha chini wanachagua kufanya hizo kazi kwa hiyari yao, kama hamzitaki mnaweza kuacha kwenda kulima au kufuga ng'ombe porini.
 
Waafrika walimuasi lini Mungu wakati walikutana na Ukristo kwa mara ya kwanza baada ya wazungu kufika Africa na hapo hapo wakaanza kukamatwa kama Watumwa??
Hao Wakristo waliokuwa wanawachukua watumwa kwa nguvu walikuwa wanaesabihiwa kama waovu au wenye dhambi??
Mungu anaweza akaruhusu upate majaribu au chamgamoto kama hizo lakini akaja kukutoa baadae na kukuinua zaidi akakurudishia zaifi mara dufu kama utakuwa na imani thabiti kwake,kama utakuwa mnyenyekevu,utaendelea kumuomba.
Sababu za kuruhusu watu wake wapitie magumu /majaribu changamoto mbalimbali ikiwemo utumwa,magonjwa n.k
zipo nyingi ila hiyo ya kutenda dhambi ni moja wapo.
Mfano YUSUFU /JOSEPH aliuzwa utumwani Misri lakini hakumuasi Mungu na pindi anauzwa hakuwa amemuasi Mungu alikuwa na imani kwa Mungu na mtumwa mnyenyekevu na mwaminifu.Mungu alikuja kumfanya waziri mkuu wa misri.
Mungu aliruhusu ndugu zake wamuuze utumwani lakini hakumuacha,sasa kwq sababu utumwa ulikuwa na utamaduni wa watu wa zamani,ile kuwa humble ilimfanya apendwe na slave masters wake hata gerezeni alipewa unyampala sasa asingekuwa mtumwa mtiifu ,asingeoata favour na Mungu anatuagiza tuwe humble watu wote wakati wote.tumtumaini Mungu atatuokoa katika hali zote hata utumwani waisraeli waliomba Mungu akasikia kilio cha waizraeli akamtuma Musa aende kwa FARAO wa misri ili awatoe watu wake .
Japo pia kumuasi Mungu kuna maana hata upagani ukishakuwa mpagani wale watu watu wanao abudu miungu ni wamemuasi Mungu,na makosa hayo wanaweza wakaadhibiwq hata kizazi chao cha nne.
Mana kuabudu miungu ni laana inayoweza kuathiri hata vizazi vyako vijavyo.
 
Kwa sababu moral consciousness ya jamii ya wakati huo haikuona utumwa kuwa kitu cha ajabu sana, ingawa kuna watu waliokuwa wakisema kuwa utumwa si sahihi.

Ni kama vile ambavyo inawezekana watu wa miaka ijayo inawezekana wataacha kuchinja wanyama na kula nyama halafu kutushangaa kwa nini watu wa wakati huu tulikuwa tunachinja wanyama na kuwala nyama, moral consciousness ya jamii yetu haijafikia kuona kuchinja wanyama kama jambo baya hivyo, ingawa kuna watu wanaoona kula nyama si kitu sahihi.
Ulaji nyama ni sehemu ya evolution ya binadamu, ulaji nyama kwa kiwango kikubwa ulileta mabadiliko makubwa katika ubongo na mwili mzima wa binadamu ulipelekea mabadiliko makubwa zaidi, kula nyama kwa binadamu ni moro of necessity than just a choice, tafiti mbalimbali zinaonyesha watoto vegan au watu vegan hukabiliwa na changamoto mbalimbali za afya zitokanazo na ukosefu wa virutubisho.
 
Waafrika walimuasi lini Mungu wakati walikutana na Ukristo kwa mara ya kwanza baada ya wazungu kufika Africa na hapo hapo wakaanza kukamatwa kama Watumwa??
Hao Wakristo waliokuwa wanawachukua watumwa kwa nguvu walikuwa wanaesabihiwa kama waovu au wenye dhambi??
Ila sio Africa yote,,mfano Ethiopia na misri ukristo uliingia kabla hata ya wazungu kuja Africa
 
Mungu anaweza akaruhusu upate majaribu au chamgamoto kama hizo lakini akaja kukutoa baadae na kukuinua zaidi akakurudishia zaifi mara dufu kama utakuwa na imani thabiti kwake,kama utakuwa mnyenyekevu,utaendelea kumuomba.
Sababu za kuruhusu watu wake wapitie magumu /majaribu changamoto mbalimbali ikiwemo utumwa,magonjwa n.k
zipo nyingi ila hiyo ya kutenda dhambi ni moja wapo.
Mfano YUSUFU /JOSEPH aliuzwa utumwani Misri lakini hakumuasi Mungu na pindi anauzwa hakuwa amemuasi Mungu alikuwa na imani kwa Mungu na mtumwa mnyenyekevu na mwaminifu.Mungu alikuja kumfanya waziri mkuu wa misri.
Mungu aliruhusu ndugu zake wamuuze utumwani lakini hakumuacha,sasa kwq sababu utumwa ulikuwa na utamaduni wa watu wa zamani,ile kuwa humble ilimfanya apendwe na slave masters wake hata gerezeni alipewa unyampala sasa asingekuwa mtumwa mtiifu ,asingeoata favour na Mungu anatuagiza tuwe humble watu wote wakati wote.
Achana na Waisraeli,
Zungumzia Waafrika, Wazungu, Waarabu, Wahindi n.k ambao hawakuwa "watu wake"
 
Back
Top Bottom