Kwanini wakristo wakatoliki wanaungama dhambi kwa padri? AKA kuhani?

Kwanini wakristo wakatoliki wanaungama dhambi kwa padri? AKA kuhani?

paqwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2019
Posts
2,593
Reaction score
3,603
Kwa miongo kadhaa, tumekubali uwongo eti kwamba kuomba msamaha wa kibinafsi na wa kimoyomoyo ndio kitu pekee ambacho Mungu anahitaji ili kufuta dhambi kubwa.

Lakini Mungu wa Biblia hakuweka kamwe mfumo wa upatanisho usioonekana kabisa.

Zaidi ya miaka elfu moja kabla ya Kristo, Mungu aliwaamuru Waisraeli katika Mambo ya Walawi 5 kukiri dhambi zao kwa sauti kwa kuhani mpatanishi kabla ya upatanisho kufanywa.

Neno la Kiebrania lililotumika katika maandishi ni yada: likimaanisha kutoa dhambi kinywani mwako. Lazima utamke usikike.

Huwezi tu eti "kujisikia vibaya" kuhusu dhambi na kutiwatia huruma kwamba ndo yameisha; Mungu anadai ubebe mzigo wako uwe accountable ,own it!

Yesu Kristo alipofika, hakuondoa muundo huu wa sauti wenye ukali na wa kuvutia. Aliuinua vizuri tu.

Katika Yohana 20, aliwapulizia mitume wake Roho Mtakatifu na kuwapa mamlaka ya kutisha na ya Kimungu ya kusamehe au kuhifadhi dhambi.

Fikiria kuhusu hilo: Kwa nini Kristo aliwapa mitume uwezo wa kuhifadhi dhambi ikiwa hakutarajia uzungumze dhambi hizo waziwazi?

Na pia kisaikologia pia, unapata wepesi na kujiskia kutua mzigo mzigo sana.

Wewe mkatoliki unajifanyaga mjuaji kwaresma hii. NENDA KAUNGAME KWA KUHANI AKA PADRI.

+

Mods; Iacheni kama ilivyo tafadhali.
 
Nitaenda kiongozi,nangoja Jumakuu lianze niende na mimi kufanya hiki kitu.

Shukrani kwa ukumbusho.
 
Back
Top Bottom