A
Anonymous
Guest
Tunaomba ufafanuzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI kuhusu uteuzi wa walimu wa shule binafsi kusimamia mitihani ya NECTA.
Kabla ya mwaka 2021, walimu wa shule binafsi walikuwa wakiteuliwa kushiriki katika usimamizi wa mitihani ya NECTA. Hata hivyo, tangu mwaka 2021 hadi sasa, walimu wa shule binafsi katika Wilaya ya Ngara, Mkoa wa Kagera, hawajateuliwa tena, ilhali katika mikoa mingine wanaendelea kushiriki.
Je, ni sababu gani inayowafanya walimu wa shule binafsi wa Wilaya ya Ngara wasipewe nafasi hizi? Je, changamoto ipo kwa waajiri, ngazi ya wilaya au ni utaratibu wa Serikali?
Tunaomba mamlaka husika zitolee ufafanuzi na kuhakikisha walimu wa shule binafsi wa Wilaya ya Ngara wanapata fursa sawa na walimu wenzao katika maeneo mengine ya nchi.