Kwanini walinda mlango weusi sio wengi ligi za ulaya?

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Kwa muda mrefu Afrika imekuwa ikitoa viungo, washambuliaji na mabeki wazuri wanaotamba kwenye ligi mbalimbali barani ulaya. Toka enzi za akina George Weah, Samuel Etoo, Jayjay Okocha, Michael Essien, Yaya Toure nk.

Lakini habari ni tofauti kwa makipa, idadi ya magolikipa ni ndogo sana barani ulaya hasa katika ligi kubwa. Je magolikipa hao hawana uwezo mbele ya wazungu wanaotamba kama vile akina De Gea, Alisson Becker, Jan Oblak na wengineo.

Golikipa pekee mweusi kutoka barani Afrika anayetamba kwasasa katika ligi kubwa za ulaya ni Andre Onana wa Ajax.

Je, tatizo ni nini?
 
Huyu golkipa wa ajax ni raia wa wapi?
 
mweusi au kutoka Afrika ?
 
Kuna sababu nyingi za kwanini waafrica au watu weusi(ambapo wengi ni kutoka Africa) hawapo kwenye ligi zenye ushindani ulaya.

1. Inatokana na background ya mpira wetu Africa. Mipira ya africa ambayo vijana wanaanza kupiga soka la mitaani halina formula na vijana wanaingia wakiwa na motivation ya kucheza na kufunga magori. Watu wabovu au wasiojua ndo wanaachwa walinde gori au wacheze nyuma. Yaan anayefunga magori ndo anaonekana anajua
That z y tumefanikiwa kutengeneza mastrikers wakubwa kwenye soka waliotikisa na wanaotilisa mpaka sasa huko.
No necessity of mentioning them.
Kwa anayeshabikia mpira atakuwa anajua epl top scorers kwa msimu uliomalzika ni kina nani na wanatoka wapi?
2.sisi hatuna academies za kuandaa vijana na inajulikana ratio za hiyo nafasi ni ndogo ukilinganiesha na na wachezaji wengine 1/11. Halafu hakuna maandalizi yaan ni probability tu tena ndogo.
-Hata hivi nafasi ya goalkeeping naona kama siyo deal sana ko ina despised.
NB:
Mameneja weasi nao hatuna pia.
 
Umeongea vyema, lakini jaribu kuandika kwa ufasa maana unaonekana msomi ila lafudhi inakurudisha nyuma
 
Tim Howard | 6 Attributes Every Goalkeeper Needs | Pro Tips

The Colorado Rapids and USMNT no.1 tells you what you need to have in your armoury to be a top-class goalkeeper


Source: FourFourTwo
 
Nakumbuka enzi za utoto matipwatipwa ndo walikuwa wanakaa golini[emoji3][emoji3]. Anyway, sehemu ya goalkeeping ni nafasi nyeti sana inahitaji mtu anayeaminika, pengine wazungu bado hawatuamini watu weusi. Pia umesahau kuuliza kuhusu makocha, ni nadra pia kuona makocha weusi kwenye ligi kubwa barani Ulaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…