Kwanini wamachinga wameandamana huku wakisema "tunataka soko letu"?

Kwanini wamachinga wameandamana huku wakisema "tunataka soko letu"?

mirindimo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2009
Posts
901
Reaction score
1,742
AD7D7A5B-CDAE-4B72-B3A1-2A9D6F47CF66.jpeg


Nani kachukua soko lao? Si limeungua? Kwanini hawataki uchunguzi ufanyike wajue chanzo au wanakijua tayari ndo maana wanataka waruhusiwe waendelee na mishe zao?

By the way uchunguzi utachukua siku 14, zitaongezwa 7 kisha wataambiwa wanatafutiwa eneo lingine pale panawekwa kitu kingine ama stand ya vyombo vya moto ama kitu chochote mradi machinga wasirudi pale.
 
Tusubiri uchunguzi! Fine barabarani hatutakiwi...soko letu ndo hivyo....cha msingi tusubiri kuhamishiwa kilosa
 
Lao kivipi wakati pale waliwekwa kwa muda tu hadi majengo makubwa mawili ya soko la Machinga complex yamalizike wahamie baada ya ujenzi wakagoma ni wachache tu walikubali na bado wapo and wengine wakauza nafasi zao...

Kama ni eneo lao walete documents na wengi pale hawapo kwenye list ya wafanyabiashara waliowekwa kwa muda baada ya kuondoshwa mtaa wa Congo miaka ile...
 
hiyo sehemu ni siku nyingi serikali walitaka kuwaondoa kuwa peleka machinga complex.

ukiangalia kwa mazingira ya kufikiria pale karume palikuwa stendi na mabasi yana kaa kabisa.

ukiwaza kwa jicho la tatu ile sehemu ni nzuri ya stendi ya mabasi ambayo watu buguruni,temeke,kigogo,au makutano
 
View attachment 2085687

Nani kachukua soko lao? Si limeungua?Kwanini hawataki uchunguzi ufanyike wajue chanzo au wanakijua tayari ndo maana wanataka waruhusiwe waendelee na mishe zao?

By the way uchunguzi utachukua siku 14 , zitaongezwa 7 kisha wataambiwa wanatafutiwa eneo lingine pale panawekwa kitu kingine ama stand ya vyombo vya moto ama kitu chochote mradi machinga wasirudi pale.
Huo ni uwongo,kwani soko la kariakoo,limeungua na linajengwa soko tena umesikia kuwa pale panawekwa kitu kingine badala ya soko,?kwanini tunapenda kuzusha uongo?
 
Back
Top Bottom