Huo msemo hauna maana yoyote kwa swala la Ngorongoro. Hii ni vita ya kiuchumi kati ya Tanzania ambayo mimi ni mmoja wapo, na Kenya ambayo wewe ni mmoja wapo. Wamasai wa Kenya mmekuwa mkitumia ardhi yetu kupitia mgongo wa wamasai wa Tanzania. Mmejipenyeza, mkapewa hifadhi na baadhi ya wamasai wa Tanzania wasiokuwa wazalendo wa taifa lao. Na baadhi yenu wakatafutiwa vibali vya uraia wa mchongo wa Tanzania kupitia maafisa wanaoendekeza rushwa huko uhamiaji. Sasa serikali imeshtuka na kuamua kuwaweka raia wake (wamasai wa Tanzania) mbali na mpaka wa nchi kwa sababu kuu mbili. 1) kuwaweka mbali na maeneo ya hifadhi ya taifa kwa ajili ya masilahi ya kiuchumi kwa taifa letu. 2) kuwaweka mbali na mpakani ili kuzuia ule muingiliano wa wamasai wa Tanzania na Kenya ambao ulitengeneza kichaka cha kuhalalisha wakenya wengi kuingiza mifugo yao katika ardhi yetu, kulima katika ardhi yetu na wengine kufanya ujangili katika ardhi yetu. Ingekuwa sisi Tanzania ndio tunafanya hivyo kwa upande wa Kenya basi humu mitandaoni pangekuwa hapatoshi kwa matusi, kejeli na dhihaka. Serikali yetu imewapa raia wake wenye asili ya kimasai ofa ambayo hakuna jamii nyingine yoyote hapa Tanzania iliwahi kupewa na serikali. Ofa hiyo ya kujengewa nyumba nzuri, shule nzuri, hospital nzuri, barabara nzuri, miundo mbinu ya maji, umeme na mazingira mazuri, pia kila mmasai na familia yake wamepewa kipande kikubwa cha ardhi kwa ajili ya ufugaji na kilimo. Wakati wamasai wakiwa wamependelewa ofa zote hapo juu, kuna watanzania wengine wakati wa utawala wa Nyerere waliwahi kuhamishwa kutoka katika maeneo yao ya asili, na kupelekwa katika mikoa mingine bila kujengewa hata nyuma ya miti. Pia kuna watu ambao walivunjiwa nyumba zao huko Kimara ili kupisha upanuzi wa barabara bila kupewa chochote, kuna watu wengine pia waliwahi kuhamishwa kutoka ubungo ili kupisha miradi ya serikali wakapelekwa pemben kbs na mji kwa kupewa tu viwanja vya miguu 20 kwa 20 bila kujengewa. Sasa inashangaza eti mmasai aliependelewa na serikali yetu kupitia kodi zetu akatae kuhama kwa sababu zisizokuwa na maana. Ukweli ni kwamba hakuna mmasai wa Tanzania anaekataa kwenda kuishi katika mazingira mazuri waliyoandaliwa na serikali, hao wanaokataa ni wale wamasai wa mchongo waliotokea Kenya na kuingia Tanzania kusaka uraia wa mchongo ili kuwarahisishia wao kufanya mambo yao kinyume na sheria kama vile kulisha mifugo yao katika ardhi yetu, kulima nk kupitia mgongo wa uraia huo wa mchongo. Wamasai hao wa Kenya wanahofia kwenda kuishi mbali na mpaka wa nchi yao kwa sababu itakuwa rahisi kule kuwagundua lkn pia ile style yao ya kuigeuza nchi yetu shamba la bibi itakuwa imekufa kibudu. Dunia imebadilika ndugu zetu wa Kenya, hakuna namna ya kutulaghai tena kama zamani, rudieni nchini kwenu mkapambane na serikali yenu ili wabadilishe sheria ya ardhi kwa kila mkenya kumiliki ardhi kama ilivyo kwa Tanzania.