GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Kinachonisikitisha tu ni kwamba kila ninapopita nawaona Mashabiki wa Simba na Azam wakifurahia Kilichotokea muda si mrefu huko nchi yenye Joto Kali Barani Afrika lakini kwa Mashabiki wenzangu wa Yanga SC yetu wote nawaona wamenuna mno na hata kabla ya Mtanange ndiyo waliokuwa wakizungumza sana na kuiombea Mabaya Timu yetu ya Taifa ila Mwenyezi Mungu amewakatalia.
Halafu ni kwanini lakini hawa Wachezaji wetu wa Yanga SC waliopo Taifa Stars akina Abdallah Makame na Faisal Salum pamoja na akina Metacha Mnata na hata Kelvin Yondan huwa hawana Mchango sana katika Timu kama walionao Wachezaji wa Wapinzani wetu Simba SC kama akina Jonas Mkude, Muzamir Yassin, Erasto Nyoni na Hassan Dilunga? Na Siku zote ni hawa hawa Wachezaji wa Simba SC ndiyo huwa wanaikoa na hadi Kuing'arisha Taifa Stars.
Japo Mimi ni mwana Yanga SC kabisa tena mwenye Kadi yangu ya mwaka 1990 lakini kwa huu mwenendo wa kila Siku naona tu Wachezaji wa Simba SC ndiyo wanafanye vyema katika Kikosi cha Taifa Stars naweza muda wowote kuanzia sasa nikahamia Simba SC. Na kama kweli Sisi wana Yanga SC ni Wanamichezo hasa namuomba kila mwana Yanga SC hapo alipo amuamkie Beki Erasto Nyoni kama Heshima Kubwa Kwake kwa Kufunga lile Goli zuri ambalo tokea niijue Yanga SC yangu sijawahi Kumuona Mchezaji wetu yoyote yule akifunga sana sana kila mara nashuhudia tu Wachezaji wetu Yanga SC wakiwa wanajifunga tu wenyewe.
Ila huyu Jonas Gerald Mkude kweli ni ' Injini ' kabisa katika Dimba la Kati hadi natamani ahamie Kwetu Yanga SC ila tatizo ni moja tu kuwa Yanga SC ni Masikini hatuwezi Kumlipa kama ambavyo analipwa Kitajiri kabisa huko kwa Watani zetu na wanaojua Mpira kuliko Sisi Simba SC. Na huyu Erasto Nyoni yaani anaujua Mpira hadi anakera sasa kiasi kwamba hata Beki wetu Yanga SC Lamine Moro hamfikii kabisa.
au kama vipi wana Yanga SC wote tuhamieni zetu rasmi kunako Simba Sports Club kwani huko ndiko Kumenoga hasa tu.