Umeuliza swali zuri na fikirishi ila nimeuliza swali pia kutokana na context ya mtoa mada
Binafsi yangu yaweza kuwa
" Reason behind our existence"
" Lakini pia hizi life routines za kuzaliwa, kuishi na kufa, purpose yake kubwa nini haswa kwa watu binafsi"
Sababu (reason) ya wewe kuwapo ni kwamba wazazi wako wamekuzaa.
Sababu ya watu kuwapo ni kwamba, evolution ime favor tuwepo kama species.
Mfano, kitendo kinachopelekea sexual reproduction kina raha sana, watu wanapenda kukifanya, na wakikifanya kinapelekea kupata watoto. Pengine bila hata kupanga kuwa na mtoto. Na watoto wanazidi kuzaana.
Nina hakika ingekuwa kitendo cha sex kinaumiza kama kukatwa mkono, watu wangegoma kukifanya na matokeo yake tusingekuwepo hapa.
Zaidi ya kutaka kuendeleza maisha tu, process ya evolution haina lengo maalum.
Kifalsafa zaidi, maisha hayana maana (purpose), wewe unayeishi ndiye una uwezo wa kuchagua uyape maisha yako maana gani.
Kwa mfano, unaweza kuona watu wengi wanataabika kwa kuugua na kufa kwa Malaria, ukajikita kusoma ugonjwa huu mpaka upate chanjo yake ya kuukomesha.
Ukifanikiwa, jambo hilo litafanya maisha yako yawe na maana sana, kwamba umesaidia watu wengi sana kutougua ugonjwa wa Malaria.
Lakini, hatuwezi kusema ulizaliwa ili ulete chanjo ya Malaria, kwa sababu hicho ni kitu ambacho wewe mwenyewe ulijipangia katika maisha yako.
Ukweli kwamba tutakufa, hauondoi maana ya maisha, kama vile ukweli kwamba hatuwezi kuhesabu mpaka infinity, hauondoi ukweli kwamba tunaweza kuhesabu.