Kwanini wanadamu tupo Duniani?

Kwanini wanadamu tupo Duniani?

Vijana kueni kiakili na kufikiria, unaposema "Kwa sababu Mungu hayupo" hii haiwezi kuwa sababu, unatakiwa uandike umejuaje Mungu hayupo.

Lakini matumizi ya "nge" ni kuonyesha kushindwa katika hoja na kukosoa kadhalika. Sisi tutakuuliza umejuaje kama kutokuwepo kwa Mungu ni matokeo ya haya ambayo yapo na yanayo tokea ?

Nani amekwambia hafahamiki ? Wewe na wenzako ndio hamumfahamu. Bali anafahamika na ushahidi wa uwepo uko wazi kuliko ushahidi wa uwepo wako wewe, ndio maana huwa tunasema nyinyi hamna akili.

Hakuna kitu ambacho ushahidi wake uko wazi kuzidi ushahidi wa uwepo wa Mungu.

Anajificha vipi wakati yeye ndio anaendesha haya mambo na kufanya Dunia iwe hivi ilivyo.

Ni nyinyi peke yenu hamumjui sababu hamtaki kumjua na mnajifanya hamnazo.
Quran ilisha haribu akili yako, huwezi kufikiri nje ya hapo.
 
Bila kifo dunia inge endelea kuwa na idadi ileile ya watu?

Nafasi ya kuishi kwa kila kiumbe inge patikana?

Ina onesha hata hukwenda shule.

Hukusoma na hujui mambo ya Population increase, Ecosystem, over population n.k

Unacho jua ni kuvaa kobasi na kukariri fiction stories za Quran.

Hoja ni kauli yako ya kuwa watu wangekuwa wengi na ingejaa, Sasa jibu maswali niliyo kuuliza huko juu.

Sijui kama ingepatikana au la, tusubiri mpaka pale kifo kikiwa hakipo. Uje uulize swali hili.

Jibu maswali niliyo kuuliza, kwenda kwangu shule au kutoenda, utakuona utakapo jibu.
 
Wakuu sorry

Labda nimejizima data, Ila sielewi haya maisha. Baada ya kupata CHANGAMOTO, nimejiuliza Mambo mengi

Kwanini wanadamu tupo Duniani, ili iweje, wakati tunasubiri kifo tu

Dah
Shida zikizidi tunamlaumu kila mtu
 
وَمَا خَلَقۡتُ ٱلۡجِنَّ وَٱلۡإِنسَ إِلَّا لِیَعۡبُدُونِ﴿ ٥٦ ﴾

•Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.

Adh-Dhariyat, Ayah 56
Jibu hili hapa.
Tuletee na quotes za uhindu pia
 
Ukiishajua anapoishi utakuwa umelingana naye uwezo, kumbuka wewe ni kiumbe chake na huna uwezo wa kulingana naye ata kidogo..

Kinyago ulichokichonga hakiwezi kukutisha au kukuzidi maarifa.
😂😂😂😂Mimi sio kinyago asa Mimi ni mtu...na watu wameprove kujua vingi kuliko Mungu wa biblia au wa Quran. Biblia inasema Mungu yupo mawinguni Ila kila Leo air Tanzania inapita mawinguni hatumwoni so inabidi mtafute Chaka lingine la kumzuga
 
Vijana kueni kiakili na kufikiria, unaposema "Kwa sababu Mungu hayupo" hii haiwezi kuwa sababu, unatakiwa uandike umejuaje Mungu hayupo.

Lakini matumizi ya "nge" ni kuonyesha kushindwa katika hoja na kukosoa kadhalika. Sisi tutakuuliza umejuaje kama kutokuwepo kwa Mungu ni matokeo ya haya ambayo yapo na yanayo tokea ?

Nani amekwambia hafahamiki ? Wewe na wenzako ndio hamumfahamu. Bali anafahamika na ushahidi wa uwepo uko wazi kuliko ushahidi wa uwepo wako wewe, ndio maana huwa tunasema nyinyi hamna akili.

Hakuna kitu ambacho ushahidi wake uko wazi kuzidi ushahidi wa uwepo wa Mungu.

Anajificha vipi wakati yeye ndio anaendesha haya mambo na kufanya Dunia iwe hivi ilivyo.

Ni nyinyi peke yenu hamumjui sababu hamtaki kumjua na mnajifanya hamnazo.
😂😂😂😂Kama ana fahamika mbona kila mtu ana Mungu wake. Hata katika dini moja kila mtu anamwelewa kivyake. 😂😂unajuaje anaendesha dunia umemwona? Amekuambia? Acha kuforce agency katika vitu ambavyo havina agency
 
Fikiria pia kama kifo kisinge kuwepo,

Watu na wanyama si tungekuwa wengi sana kiasi kwamba kusingekuwa na Nafasi ya kuishi na kufanya makazi.

Yani tungekuwa tumejazana kama utitiri kiasi kwamba kusingekuwa hata na nafasi ya kupita au kujenga barabara.

Kila Kiumbe Lazima Kife, Ili Kiumbe kingine kipate Nafasi ya kuishi.

Rejea kifo cha Simba Bob junior aliye uwawa na simba wenzake ili wapate utawala, Sasa je Asingekufa hao simba wenzake wange ishi vipi?
Mi naona bado hujajibu swali, unaishi ili iweje sasa? Usipokuja/ishi duniani kipi kinabadilika?
 
una
Mi naona bado hujajibu swali, unaishi ili iweje sasa? Usipokuja/ishi duniani kipi kinabadilika?
unagoma kuelewa tu,

Narudia tena,
Ili tumjue, tumpende na tumtumikie ili mwishowe tufike kwake juu mbinguni.
basi ni hivyo tu, unataka nn tena....

ni kwasabb umekuja duniani ndio maana unahoji usingekuja kipi kinabadilika,
wakati unajua fika kwamba usingekuja duniani hata iyo Infinix hungekua nayo na wala hapa JF usingekuepo.

unaweza kuniuliza tena, kwanini usingekuepo ?
ni kwasabb alietuumba ameonelea usiwepo huku kama ulivyo.

pia usingekupo huenda tusingekua na swali kama hili...
 
Issue ndio ipo hapo mkuu

Unawezaje kujitoa kwenye hizo attachments ili uweze kufikiria kwa akili binafsi

Na kingine hapo, unaweza kuwa una imani na Mungu 100% na pengine hutaki kuacha imani yako lakini Mungu anavyokuwa presented katika njia ambayo ipo somehow controversial kiasi cha kuzua migongano ya kidhehebu na kidini. Unawezaje deal na hili
Ni kupitia yoga mkuu,you can break all attachments za kuanzia utotoni mpaka hapo ulipo. Utakuwa free man. Unaweza pia kuvunja zile mambo ya kurithishana ambazo huenda ukoo hadi ukoo..
 
Wakuu sorry

Labda nimejizima data, Ila sielewi haya maisha. Baada ya kupata CHANGAMOTO, nimejiuliza Mambo mengi

Kwanini wanadamu tupo Duniani, ili iweje, wakati tunasubiri kifo tu

Dah
You are right, umeletwa uishi ili usubiri kifo. Yaani wewe na mimi tupo hapa kweye foleni ya kwenda kuchomwa moto mbinguni na baba aliyetuumba, this according to imani za kuletewa toka Palestina na Israel ila wao wanaamua kuwahi foleni ya kuchomwa moto kwa kuuana through vita.
 
Jibu utapata ukirudi nyuma hadi kipindi kabla Adamu na Hawa hawajamkosea Mungu

Mwanzo 1:28 BHN
Mungu akawabariki na kuwaambia, “Zaeni muongezeke, mkaijaze nchi na kuimiliki; muwatawale samaki wa baharini, ndege wa angani, na kila kiumbe hai kitembeacho duniani.”

Haya matatizo yaliyojitokeza baada ya Adamu na Hawa kuzingua pale Edeni ndiyo yanayofanya wengi kama mleta mada kuuliza hilo swali

Ila Mungu alikuwa na nia nzuri sana na sisi wanadamu tuishi Edeni huku wote tunamtumikia yeye peke yake. Ila wazazi wetu wa kwanza ndio walizingua. Tunavuna alichopanda Adamu na Hawa
 
Wakuu sorry

Labda nimejizima data, Ila sielewi haya maisha. Baada ya kupata CHANGAMOTO, nimejiuliza Mambo mengi

Kwanini wanadamu tupo Duniani, ili iweje, wakati tunasubiri kifo tu

Dah
Hapana, kwa mtazamo wangu "haujazima data" na swali lako ni zuri, inatakiwa na inapaswa kila mtu kujiuliza maswali kama hayo. Naamini aulizae ataka kujuwa.

Kabla sijaenda mbali zaidi, naona kama swali lako linanichanganya kidogo. Kwa kuwa linanichanganya itanibidi nikuulize maswali maswali mawili matatu ili nilielewe vyema.

Nimeshawahi kuona mtu akiuliza "kwanini tumeumbwa ?", lakini wewe hapana, hauna haja ya kujuwa kwanini tumeumbwa, wewe unataka kujuwa kwanini tupo duniani. Si ndivyo?

Pia naona umeshakiri na kukubali kuwa wewe ni "mwanadamu". Hapo pia umepunguza sana ya kunifanya nifikiri sana, kwani ayari unajijuwa kuwa u mwanadamu. Ingekuwa ni mtu u na si mwanadamu, kidogo jibu lingekuwa vingine na lisingeambatana maswali haya.

Pia nimefurahi sana kuona kuwa unaelewa kuwa tunangoja "kifo" tu. Maana kuna wengine huwa wanauliza "mie nangoja nini hapa duniani?", kwa hiyo na hpo umenipunguzia kazi ya kukuelewesha tunangoja nini, au siyo?

Baada ya kuyafikiria hayo maswali yangu natumai utakuwa na majibu au maswali mengine, rukhsa kuuliza tena.

Jibu lako kwa ufupi, kutokana na swali lako, upo hapa duniani kwa sababu "Adamu" alikuwa hapa duniani, na wewe umeshakiri kuwa u mwanadamu.

Nakaribisha maswali ya ziyada, kutokea kwako au kwa mwngine yeyote.
 
Wakuu sorry

Labda nimejizima data, Ila sielewi haya maisha. Baada ya kupata CHANGAMOTO, nimejiuliza Mambo mengi

Kwanini wanadamu tupo Duniani, ili iweje, wakati tunasubiri kifo tu

Dah
Ukija kujua kwanini wanadamu tupo duniani na nini hatma yake utakuwa mwenye mafanikio na furaha tele!
 
Wakuu sorry

Labda nimejizima data, Ila sielewi haya maisha. Baada ya kupata CHANGAMOTO, nimejiuliza Mambo mengi

Kwanini wanadamu tupo Duniani, ili iweje, wakati tunasubiri kifo tu

Dah

pole hiyo inaonekana umepoteza tumaini!!
kwa kizungu tunaita “feeling of being lost”
mtu kutoona maana ya maisha, kutojua kwann tunaishi…..

Hamna mtu anaweza kukujibu hili swali.ila naweza kukusaidia kuiondoa hii hali…

1.Tambua matatizo ni sehemu tu ya maisha
2.Kila jambo lina muda wake na kila kiumbe kinapitia wakat mgumu
3.Funga na kuomba “Emptness “ au purpose ya maisha ni mungu tu anaweza kukuambia
 
Back
Top Bottom