Hapana, kwa mtazamo wangu "haujazima data" na swali lako ni zuri, inatakiwa na inapaswa kila mtu kujiuliza maswali kama hayo. Naamini aulizae ataka kujuwa.
Kabla sijaenda mbali zaidi, naona kama swali lako linanichanganya kidogo. Kwa kuwa linanichanganya itanibidi nikuulize maswali maswali mawili matatu ili nilielewe vyema.
Nimeshawahi kuona mtu akiuliza "kwanini tumeumbwa ?", lakini wewe hapana, hauna haja ya kujuwa kwanini tumeumbwa, wewe unataka kujuwa kwanini tupo duniani. Si ndivyo?
Pia naona umeshakiri na kukubali kuwa wewe ni "mwanadamu". Hapo pia umepunguza sana ya kunifanya nifikiri sana, kwani ayari unajijuwa kuwa u mwanadamu. Ingekuwa ni mtu u na si mwanadamu, kidogo jibu lingekuwa vingine na lisingeambatana maswali haya.
Pia nimefurahi sana kuona kuwa unaelewa kuwa tunangoja "kifo" tu. Maana kuna wengine huwa wanauliza "mie nangoja nini hapa duniani?", kwa hiyo na hpo umenipunguzia kazi ya kukuelewesha tunangoja nini, au siyo?
Baada ya kuyafikiria hayo maswali yangu natumai utakuwa na majibu au maswali mengine, rukhsa kuuliza tena.
Jibu lako kwa ufupi, kutokana na swali lako, upo hapa duniani kwa sababu "Adamu" alikuwa hapa duniani, na wewe umeshakiri kuwa u mwanadamu.
Nakaribisha maswali ya ziyada, kutokea kwako au kwa mwngine yeyote.