Kwanini wanafunzi wa darasa la 7 wanachelewa sana kutoka Shule?

Kwanini wanafunzi wa darasa la 7 wanachelewa sana kutoka Shule?

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
3 (29).jpg

Hivi siku hizi ni kwamba utaratibu wa masomo ya wanafunzi wa primary hasa wa la 7?

Kwa sababu asubuhi mida ya saa kumi na moja unawakuta wako barabarani wanasubiri usafiri na jioni hadi mida ya saa mbili unakutana nao wamesimama huko barabarani ndo wanaenda nyumbani.
Nimejaribu kuwauliza wanasema wanawahi shule na wanachelewa kutoka kwa sababu ya masomo ya ziada shuleni
Sasa ukijiuliza mwanafunzi wa darasa la saba ana miaka 10 hadi 12 bado ni wadogo. Walimu wanawaza kweli usalama wa hawa watoto tena wakati wa jioni ambapo usalama unasumbua hasa hapa dar

Mamlaka husika liingilie kati japo hili na kutafauta njia mbadala ili kuwalinda hawa wanafunzi
 
Ebungoja kwanza nione kama itawezekana atulipe lile deni..😶
Nani tena bro, madeni tuyaache kwanza. Kurudi kwenye mada hawa watoto wanateseka na hawafurahii kusoma kwao, ama kuwe na plan B ili wakitoka hapo wawe na gari lakuwapeleka majumbani Elimu gharama ukiambiwa ELIMU BURE TAFAKARI
 
Mzee, dunia sio lele mama, Kama unaona saa 12 muda mbaya muhamishe shule akae home kwako.

Watoto inatakiwa wajue maisha ni kuhangaika na kufanya kazi kwa bidii sanaaaa, ndio mana yakitoka matokeo madogo wamefaulu mnasema mitihani ni rahisi ila madogo ukweli wanasoma sana siku hzi.
 
Nani tena bro, madeni tuyaache kwanza.
Kurudi kwenye mada hawa watoto wanateseka na hawafurahii kusoma kwao, ama kuwe na plan B ili wakitoka hapo wawe na gari lakuwapeleka majumbani Elimu gharama ukiambiwa ELIMU BURE TAFAKARI
Duhhhh...
Haya mambo tulisha kubaliana kitambo.
Ona sasa nilikua najibu sms wakati nishalewa na nina comment...😑
 
Shule ya sekondari itumba iko Ileje wanatoka saa mbili usiku. Ukizingatia mazingira na jiografia ya Ileje na shule yenyewe ni mixed....halafu wamevuna SASA hivi ni mwendo WA kula nakuwaza ngono....naogopa Sana Kwa huyu binti yangu.
 
Wapo wanachelewa kutoka ila saa kumi na mbili wameshatoka.

Wapo wanaokaa tu hapo stend hawataki kwenda nyumbani kupika na kuosha vyombo.

Yaani wanasimama stend hata lije bus tupu hawapandi
 
Unaongea nini wewe

Watu tuliosoma karibu na mbuga ndio unapita uende shule tuseme nini?

Maisha ni kupambana acha wapambane bwana
 
Shule ya sekondari itumba iko Ileje wanatoka saa mbili usiku. Ukizingatia mazingira na jiografia ya Ileje na shule yenyewe ni mixed....halafu wamevuna SASA hivi ni mwendo WA kula nakuwaza ngono....naogopa Sana Kwa huyu binti yangu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hivi siku hizi ni kwamba utaratibu wa masomo ya wanafunzi wa primary hasa wa la 7?

Kwa sababu asubuhi mida ya saa kumi na moja unawakuta wako barabarani wanasubiri usafiri na jioni hadi mida ya saa mbili unakutana nao wamesimama huko barabarani ndo wanaenda nyumbani.

Nimejaribu kuwauliza wanasema wanawahi shule na wanachelewa kutoka kwa sababu ya masomo ya ziada shuleni

Sasa ukijiuliza mwanafunzi wa darasa la saba ana miaka 10 hadi 12 bado ni wadogo. Walimu wanawaza kweli usalama wa hawa watoto tena wakati wa jioni ambapo usalama unasumbua hasa hapa dar

Mamlaka husika liingilie kati japo hili na kutafauta njia mbadala ili kuwalinda hawa wanafunzi
Wahamie Feza kwa mtoto wa bwana fedha hakuna mambo hayo.
 
Ni lini huu utaratibu wa watoto kupoteza muda eti kujiandaa na mitihani utaisha? Yaan ni kukaririshwa tuuu akija mtaani maisha ni tofauti na ya shule.
 
Ingekuwa poa sana watoto wangesoma maximum 4 hours a day. Ili muda mwingine wajifunze skills za maisha wakiwa makwao. Sababu hakuna kitu anachoambiwa shuleni hakiko kwenye simu
 
Back
Top Bottom