Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Kipengele kilichofanya huo muswada ukawa objected sio kumpunguzia rais madaraka pekee.
Pamoja na mambo mengine, kuna issue ya confidentiality kwenye hilo proposed baraza la usalama. Ni kubwa utadhani mkutano wa hadhara au kikao cha bunge. They need to brainstorm who the must be-s in that baraza.
Nime adress hili hapo juu, kwamba ukipinga muswada kwa sababu ya confidentiality/ namba ya watu basically hupingi muswada, unapinga aspect yake, na namba inaweza kushushwa hata kufika aliposema Diallo au chini yake. Kwa hiyo hii si point ya msingi, ama sivyo utasema hata shughuli za baraza la mawaziri nazo ziendeshwe na rais pekee, kwa sababu kuna maswala ya ulinzi nyeti sana yanaongelewa pale.
By they way I second kwamba huo muswada mzima ungepatikana ungekata mzizi wa fitina.
Wewe ushawapa msemo kwamba haya mambo ni confidential sana hivyo hayahitaji baraza, halafu unategemea wakuwekee muswada hapa? Wakitumia kanuni yako wewe mwenyewe kwamba hili ni suala nyeti sana kuwekwa public? Utashi wako mwenyewe kuhusu details za musada huu unaonyesha jinsi gani kuna umuhimu wa kuwa na baraza.
In general, Sophia kachemsha. Kama angekuwa anauelewa huo muswada vizuri angeusimamia na kujibu zile hoja properly. Kushindwa kwake kufanya hivyo ndiko kumepelekea muswada kupigwa chini.
Huyu Sophia tushamzoea ni mtu wa michemsho na mipasho, na nilishasema sehemu appropriate kwake ilikuwa pale Ilala kwenye mipasho. Having said that, yeye kama courtier wa Kikwete, hata kama angekuwa smart angekuwa na wakati mgumu sana kuitetea hii hoja. hii hoja ni sawa na kuwapa wabunge bonus katika system ambayo inafuata checks and balances (tatizo sisi hatuna, bunge letu haliko hata kwenye rubber stamp, ni an empty shell tu). Usiamini hata siku moja kwamba serikali ya Kiwete wanataka huu muswada upite, wanafanya maigizo tu pale, na Simba asingeweza kutetea sana huu muswada kwa sababu hiyo haikuwa nia ya serikali, walipeleka pale kama geresha tu kujionyesha kama wao wako tayari kufanyan reform.Lakini hawana nia thabiti, wangekuwa na nia kwanza wala asingeupeleka Simba pale, angeenda AG au mtu mwingine atakayejua cha kuongea.
Kwa mfano, ameshindwa hata kutetea hiyo hoja ya kwa nini Rais apunguziwe madaraka. Amedhihirisha kwamba alikuwa desa one-to-one au alikariri tu, au hakuusoma kabisa. Na kama ni kutaka check and balances ziwepo kwenye madaraka, basi mhusika wa kwanza ni yeye Sophia Simba.
Again this is exactly serikali ilichotaka, ukimpeleka kipanga anayejua sheria na kuongea sana anaweza kuwasomesha wabunge mpaka wakaelewa kwamba hili deal linafaa, mwishowe wakampunguzia Kikwete madaraka, Kikwete hataki hilo.