Kwanini wanaoteuliwa kuelimisha mambo ya kodi sio TRA wala hawana elimu hiyo?

Kwanini wanaoteuliwa kuelimisha mambo ya kodi sio TRA wala hawana elimu hiyo?

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
9,397
Reaction score
12,415
Swali la kipima joto la leo

Ipi haja ya kuwepo kwa TRA kama wanaoteuliwa kuelimisha mambo ya kodi sio TRA wala hawana elimu hiyo.

Je, kuna haja ya kuendelea kusomesha watanzania shahada za mambo ya kodi (Taxation)?

Je, fedha za kuwalipa hao wanaoelimisha zinatoka kwenye mfuko upi? Je, kwanini tusichukue watu wa TRA au waliosomea mambo ya kodi ndio waelimishe hayo mambo?

Bodi ya wahasibu mko wapi, mmenyamaza tu.

Karibuni kwenye kipima joto wakubwa
 
Nameona kuna mtu anataka kushindana na ric ross..!!
Hahahahahahahahahaha..........
 
Sensitization ni Kipaji sio Elimu au PhD ya Udsm
 
Mkuu namsubiri Mabeto huku Namabengo nimpige swali la hesabu za kukadiria kuongezeka/kupungua kwa thamani za mali zangu, ndio watajua kuwa wanajua kuwa tunawajua.

Kwa kifupi huku ni kuharibu kazi na taaluma za watu, kuna siku tutakuja kuletewa akina Kingwedu. Steve Nyerere na kuambiwa wanahamasisha Watanzania tujue Kiingereza na sheria au Katiba ya nchi.
 
Ulipaji wa kodi lazima uanzie juu kwa hao wholesalers na TRA wanakwama huko
Labda bidhaa muhimu zaidi zingekuwa price marked ijulikane moja

Mbona coke na sigara na pombe wameweza?

La sivyo mmoja anauziwa kwa bei ya risiti na mwingine ananunua kwa bei ya chini na wote wanauza bei moja
Hapo ndio tunakwama hata aje nani afundishe ulipaji hakuna kitu
 
Kila penye rizki hapakosi fitna na wivu.

Wenye taaluma hiyo wameshindwa kujiongeza na kuonyeshadalili ya tija,
Mamlaka imeamua kuja na plan B Wachawi sasa haoooo barabarani.
Kaeni na maelimu yenu tuone hawa walioteuliwa watakuwa na faida gani,
Wakishindwa kuleta tija tutaangalia mbele tufanyeje lakini kwa sasa tuache makelele hayasaidii sana.
 
Mkuu acha longolongo kulipa kodi ni sheria.
 
Back
Top Bottom