Kwanini wanaotoa ushuhuda makanisani huwa hawachukuliwi hatua za kisheria?

Serikali haingiliani na mambo ya ibada na ndoto za kiimani
Historia inaonyesha, Ulaya serikali ziliongoza mambo mengi kupitia kwenye vitubio au Confession booth.

Watu wanakiri na kuongozwa kutoa siri zao kwa makasisi, wengine kumbe ni vibaraka basi siri za upande wa pili zinaingia upande wa pili.

Pia hata viongozi wa kiserikali katika kutubu kwa viongozi wa kidini walipeea maelekezo maalum mambo mengi yanayofanyika kwenye siasa yakawa ni matolea ya maelekezo ya kwenye vitubio.

Kuna kipindi france hizi mambo zilikuwepo.
 
nimezingatia katiba ya JMT , ila raia wanahaki ya kuabudu nje ya hapo mengineyo ni nyuma ya pazia. nakubaliana nawewe
 
Shuhuda zile huwa ni katika uga wa kiimani. Mambo ya kiserikali hayaendeshwi kwa imani, bali through facts.
 
Wasanii wana haki ya kuigiza chochote nchii hui isipokua Video za ngono na kuikosoa serkali. Usanii ni ajira pia ni burudani.
 
Shuhuda zile huwa ni katika uga wa kiimani. Mambo ya kiserikali hayaendeshwi kwa imani, bali through facts.
Kwenye imani mfano anasema aliingia kijijini gamboshi akapiga mishale watu mia ambao walikuwa wanamloga. Alafu kwenye uhalisia kweli kuna mauaji yamefanyika gamboshi ya watu wasipungua 80 kwa mishale na kunyongwa.

Hauni kama hapo kuna interest ya serikali. Maana hao hata kama ni wachawi bado ni raia.

Au vile vifo huwa ni story za imani tu havina uhalisia.
 
hata wewe unaweza ukawa umechinjwa. Maana za kuchinjwa kiroho ni zaidi ya moja.
1. Mtu akichinjwa kiroho anamaanisha amemuua kiroho. Mfano ulikuwa mfanyabiashara baada ya kufanyika mambo yao kiroho ufanya biashara wako unakufa. (japokuwa wewe unaishi lakini lile jambo zuri ulilopewa katika maisha yako linauawa)
2. pia wanaweza wakakuchinja ukafa hadi mwili.
NB. UPANGA NI NENO. MTU YEYOTE ALIYEPEWA NGUVU HIYO NA MUNGU AMA MIUNGU ANAWEZA KUFANYA HIVYO KUTOKANA NA AMRI ANAYOPEWA NA MUNGU AMA MIUNGU ILIYOMTEUA KUKAA KWENYE NAFASI HIYO.
 
Uchawi bado ni imani. Labda mfano mwingine; hata kama mmoja atashuhudia waziwazi kwamba alikuwa jambazi na alipora na kuua watu kwa silaha za moto bado serikali itafanya uchunguzi kwa taratibu zake including PGO na sio kumkamata kwa sababu kakiri katika kusanyiko la waabuduo. Na huu ni utaratibu wa toka kale; toka nyakati za mitume sio wa jana wala juzi.
 
Yule mama niliyemsikia redioni anasema,
Kuna wabaya wake walikuwa wanamtesa mume wake, anasema alipewa upanga mkali kinyama, akaenda kuwachinja huko kwenye kambi yao


Anadai kulifanyika umwagaji damu mkubwa sana. Yaani damu ilitapakaa pori zima maana walikuwa wengi.

Sasa mkuu hii sio Genicide/ Mauaji ya kimbari. Au ni Spiritual genocide.
 
Kuna watu wengine wanatengeneza hadithi lakini wengine ni wanafanya hivyo.
Ajabu ni kuwa kama huna uwezo wa kuingia katika ulimwengu wa roho huwezi kuona ndiyo maana unasikia watu wanaenda kwa watu wenye uwezo huo kama vile baadhi ya watumishi wa Mungu au wengine huenda kwa waganga wa kienyeji.
Hebu fikiri mtu anakuroga mguu unakatika kabisa lakini huna uwezo wa kumshitaki kwa namna ya mwili japokuwa tunaona kabisa kwa jinsi ya mwili umekatwa mguu. Hivyo ni lazima upiganie katika ulimwengu uleule aliokupigia ndipo umshinde.
 
πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘

Waefeso 6:12
Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
 
Hv akifanya confession kanisani au akiconfess mbele ya mtu ambaye hana mamlaka ya kusikiliza ambapo hao viongozi wa dini wanaangukia humo.
 
Kabisa mkuu, na wanalipwa kwa shuhuda hizo za uongo na wengine wanapigwa pu pia [emoji3][emoji3]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…