kidole cha simba
JF-Expert Member
- Jun 3, 2022
- 1,994
- 2,510
Ndugu m2mishi,serikali inaelewa umuhimu wa haya makanisa kwani ni moja wapo ya kazi za makanisa haya ni kama therapy kwa wenye matatizo ya akili,,,wengi wa wanaoenda kwenye makanisa haya wana matatizo ya akili kutokana na msongo mkali wa maisha,maradhi sugu,kutopata watoto,matatizo ya ya makazini,n.k,,,,so sio wote wanaosema wamepewa upanga ni kweli{nani kamwona malaika?] si unamkumbuka MALKIA ZAMURADI alisema yeye ni MUNGU? na akasema alienda mpaka mbinguni na kuna magorofa marefu na akapiga story na YESU??{sasa utasema huyu ni mzima kweli????],,,,matokeo yake waumini wake wakaamini na kuanza kumwabudu mpaka wakawa kama mataaira na hapo TISS wakaingia kazini kwani wangechelewa tu yangetokea kama yale ya kenya ya msitu wa shakahoza{wa2 walifunga mpaka kufa ili waende MBINGUNI!!!,,,,so sio kwamba serikali inaacha,no wanawachunguza kwa kuchomeka wa2 wao kujifanya nao ni walokole,ila wakiona dalili za hatri ndo wanaingilia kati!!Moja kwa moja....
Nilimsikia mama mmoja anasema katika ulimwengu wa roho amechinja wachawi karibu mia, alipewa upanga na malaika. Sasa watu mia kuchinjwa rohoni ni upotevu mkubwa wa nguvu kazi.
Mwingine unamsikia anasema walikuwa wachawi, wanasababisha ajali, wanakinga damu. Wanajinadi kuwa wameua watu wengi. Hii ni kama Genocide ukijumlisha mauaji hayo ya ajali zetu kwa mwaka.
Mwingine alienda mbali eti hadi Hayati Mkapa alipopata ajali akiwa kwake Ikulu yeye na team ya wachawi walikuwa wanapambana naye. Hii sio ajabu maana Ikulu hadi Brazili na Malawi tulishasikia hayo ya watu kupigwa kishirikina hadi kukimbia Ikulu.
Hapo achilia mbali majambazi, wauwaji na watenda maovu ya kutisha wanapotoa shuhuda zao live tena kwa kushangiliwa na hatuoni wanapelekwa Jela kutumikia kifu go cha uharifu huo wakati hawajamjua Bwana Yesu.
Najiuliza kama mtumishi
Huwa tunapangwa tu na Serikali huwa inajua na kuamua kupotezea?
Hakuna ushahidi wa kisheria kuwachukulia hatua kwenye mambo ya kiimani?
Au Serikali inatambua makanisa ni chombo saidizi cha kubadili mienendo ya jamii hivyo wanasaidiwa kazi na wachungaji
Wakuu kitaalam hii imekaaje. Au wewe ulishawahi kusikia shuhuda gani za kutisha hadi ukageuka kuona kama kuna Polisi anasikia?