Kwanini wanasema simu ya mpenzi wako sumu?

Kwanini wanasema simu ya mpenzi wako sumu?

Binadamu amehamishia data zake kwenye simu. Ni kama kahamishia medula oblangata yake kwenye simu. Simu inatumika kumsaidia kutunza kumbukumbu hata zenye siri kubwa. Ukitaka kujua siri ya mtu wewe dukua simu yake tu.
Ukifanikiwa kujua siri zilizopo kichwani kwa mwenzio ni dhahili utakumbwa na mshangao baada ya kujua yupo tofauti na ulivyokuwa unamdhania.
Mlio kwenye ndoa au mahusiano ya mapenzi eleweni kuwa kile unachoenda kukitafuta kwenye simu ya mwenza wako ni lazima siku moja utakipata.
Je umejiandaaje na matokeo?
 
Mimi simu ya Mume wangu naishika na nitaendelea kuishika. Kama tumeunganishwa na kuwa mwili mmoja kwann niogope kushika simu yake...?
Msingi wa mahusiano ni uaminifu. Hilo linaanza kabla ya kupendana.

Kama mmeanza kupendana kisha uaminifu ukaja baadaye inakua ni tatizo hata kwa ishu ndogo. Privacy ni muhimu na inakua rahisi kugeana privacy kama mwanzoni kabisa msingi wenu ulikua uaminifu.
 
Na hio nafasi ndio mnayoitumia ku entertain watongozaji na ma crush wenu makazini wanaowainamisha kwenye siti za magari na vyooni huku mkiitana bae bila aibu!
Haya maelezo yamekuja na experience ndani yake? No?
 
Wengi wanajutia au hata kufurahia uamuzi wao wa kujikuta wanachungulia ujumbe na mawasiliano ya wenzao katika simu zao za mkononi lakini matokeo yake ni jambo ambalo hawakulipangia.

Ni kifaa kidogo cha mkononi ambacho kilifaa kurahisisha mawasiliano miongoni mwa watu.

Lakini sasa hivi kama kuna njia rahisi ya kuvunjika kwa ndoa ama sababu kubwa ya kuvunja mahusiano, ni simu ya mkononi imetajwa kuwa nambari moja katika orodha hiyo.

Tafiti nyingi zinaonesha kwamba kiwango cha talaka kinaongezeka kila uchao hasa kwa wenye umri wa makamo kwasababu ya simu ya mkononi ikiwa wazi kwamba imegeuka na kuwa sumu katika ndoa badala ya faraja au furaha.

Lakini je uhalisia ukoje?

Ndio hali ambayo Bity Wariama amejikuta kwani kila siku anayoishi akijiambia kwamba laiti angelijua basi hangepambana kwa udi na uvumba kuichukua simu ya mume wake na kuangalia jumbe zake!

Aliposoma na kuona wote waliokuwa wakiwasiliana naye hakutaka kupata majibu alifungisha virago vyake na kuondoka.

Tatizo ni kwamba, sasa miezi kadhaa badaye alipofahamu kwamba kuna wanawake wengi waliokuwa wakiwasiliana na mume wake naye hakuwa na haja bali alikuwa tu akiwajibu kwa minajili ya mazungumzo.

Bity alianza kujuta na kufikia wakati huo, mume wake alikuwa ashaamua kwamba Bity ana akili za kitoto na basi akasonga mbele na maisha yake kwa kupata mke mwingine .

Kwanini mwenza wako achunguze simu yako?

Mara nyingi tu anayemchunguza mwenza wake huwa anamuhisi kwamba sio mwaminifu na cha msingi kwake ni kutafuta ushahidi kuthibitisha madai yake.

Lakini mtu anaweza kumchunguza mume, mkewe, au mchumba wake kwa sababu zingine pia:

Mwenzi wako anaweza kukuchunguza kama anashuku pengine wewe ni mlevi na umemficha, unatumia dawa za kulevya au kutumia muda wako na watu ambao kwake yeye ni hatari au wenye ushawishi mbaya mfano aliyekuwa mchumba wako.

Mwenza wako anaweza pia akakushuku kuwa unatumia pesa nyingi zaidi ya unavyostahili au hata kuiba katika biashara ya familia.

Pia mpenzi wako anawe kuwa ana kushuku tu kwamba wewe unakwenda kazini lakini sio kweli.

Wakati mwengine huenda ikawa anatafuta ushahidi utakao uwezesha kutalakiana nawe

Pia ni vyema kujua kwamba kuna watu walioumbwa hivyo - yaani uwe unafanya zuri au baya wao watakushuku tu na kufikia kiwango cha kukera.

Ikiwa kuna wakati mume au mke aliwahi kumdanganya mwenza wake katika mahusiano, moja kwa moja itakuwa inaeleweka kuwa na wasiwasi na kuamua kumchunguza kutaka kujua kama ameacha tabia hiyo au anazuga tu.

Aidha, kuna wale ambao huwa wanajihisi kutokuwa salama.

Kila wakati yeye anashuku kuwa mwenza wake sio muaminifu.

Kuna wengine ambao wanapenda kudhibiti wengine.

Wanatambua kwamba mwenye maarifa ndio mwenye nguvu na wao kujua kile unachofanya kwa siri kuna wafanya wahisi kuwa na nguvu na udhibiti wa maisha yako.

Dalili za mtu mwenye kumsababishia mwingine wasiwasi na simu yake.

Lakini yote tisa, kumi kama wewe unamdanganya mwenza wako mfano katika mahusiano au kitu kingine chochote kile, bila shaka kuna yale ambayo ukifanya yatakuwa ni yenye kuzua maswali mengi machoni pa mwenzio.

Kunung'unika kama unazungumza na simu

Kutotaka simu yako kushikwa na mwingine kabisa

Kuitikia tu wakati ukiwa katikati ya mazungumzo na umemuona mwenza wako

Kuweka namba ya simu kwenye simu yao

Kuwa na matumizi yasioelezeka

Kuwa mkali haraka sana unapoombwa na mwenza wako kuwa katika mazungumzo kwasababu ya baadhi ya mambo ambayo hayamuendei sawa

Kujitetea katika wakati wa mazungumzo badala ya kuzungumza hoja

Na wakati mwingine hata kuwa tayari kuvunja mahusiano baada ya kujua kuwa mwenza wako ametambua ukweli usiotaka kukiri

Ushauri Nasaha

Hadi leo kuna visa vingi ambavyo marafiki, jamaa katika familia na hata viongozi wa kidini wanapatanisha wana ndoa kisa na mkasa, mmoja alichukua simu ya mwenza wake ili kutaja kujua yaliyomo.

Wengi wanashauri kwamba kila mtu azingatie mambo yake na simu yake.

Simu ya mwenzio usiwe na uchu wa kutaka kujua yaliyomo kwa sababu kwa mfano kama mwanamke, ukitaka kupata ushahidi kwamba kuna mwanamke mwingine anawasiliana na mume wako basi utapata.

Sasa kuna wanawake ambao wamejipa busara ya kusema, ugonjwa ambao haunipi uchungu sina haja ya kujua unaitwaje.

Wao hawana haja ya kuziangalia simu za waume zao kwa sababu wanaogopa kupatwa na mshutuko wa moyo bure.

Lakini pia kunao wenye dhana kwamba iwapo katika ndoa hamfichani lolote au hakuna anayefanya mabaya huko nje, hamna haja ya kuificha simu yako ili mwenzako asione jumbe au simu unazopiga.

Sasa kuna tofauti hapo ya jinsi kila walio katika ndoa wanavyoendesha mambo yao hasa kuhusiana na masuala ya simu ya mkononi.

Na hadi kufikia sasa, simu ya mkononi imesalia kuwa fumbo kubwa katika ndoa, je imekuwa neema au laana?

Chanzo:

View attachment 1815457
Mpenz wangu anapenda sana kupekua simu yangu, na akichukua app ya kwanza kufungua huwa ni whatssap, kisha gallery, lakin Mungu mkubwa sijawah kushindwa kesi yoyote dhidi yake

Sent from my SM-G9250 using JamiiForums mobile app
 
Utamwaminije asieaminika?
Hiki kitu kipo very delicate na complicated at the same time.

Walio wengi wanajisahau na kufikiri ukishakuwa kwenye mahusiano au ndoa basi ndo hupaswi kuwa na privacy tena.Kama mtu anataka kucheat huwezi kumzuia hata ukipekenyua sim yake anaweza kucheat vilevile kwasababu huendi nae kila mahali na kuna wengine wanaweza kuwa na namba zaidi ya moja au sim zaidi ya moja na usijue.

Muhimu kati ya yote pande zote muwe wawazi na muaminiane ila kuchunguzana mpaka sim ni tatizo tayari maanake hamuaminiani!
M
 
Kwa kweli hata mimi ntashika simu ya boyfriend tu naishika akijichanganya ndo nisije shika ya mume [emoji23][emoji23]
Kuna watu kupitia simu wamejua kama wanaume zao wanataka kuchukua mkopo nyumba ya familia. Wengine wamejua kama wenzao wameathirika.
 
Endelea kushika mkuu.. ila uwe na misuri ya moyo mgumu
Yaani mm nilishasema kabisa mwanamke amtunukuu tu mume wangu K yake lakini asitegemee kama tutaachana. Siwezi kuucha muhogo wangu wa jang'ombe ninaokesha nao usiku mzima najisevia ninavyotaka kwa ajili ya mtu mwingine. Nitaachana na mwanaume wangu kama hatoi huduma kwa familia yake.
 
Uzinzi na umalaya ni kipaji kama ilivo kucheza mpira au basket ball na inaonekana mapema kama vipaji vingine tu toka udogoni ndio maana mkiambiwa mchague wa kuzaa naye mnakuwa na jazba na hasira,serikali hawezi kuingilia vipaji vya watu its in human nature.

WHERE THERE IS A WHEEL, THERE IS A WAY!!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Msingi wa mahusiano ni uaminifu. Hilo linaanza kabla ya kupendana.

Kama mmeanza kupendana kisha uaminifu ukaja baadaye inakua ni tatizo hata kwa ishu ndogo. Privacy ni muhimu na inakua rahisi kugeana privacy kama mwanzoni kabisa msingi wenu ulikua uaminifu.
Na msingi wa uaminifu ni nini?

Kama hufanyi lolote baya au ambalo hupaswi kufanya, basi hutopatwa na shida yoyote ile endapo mwenzako atashika simu yako.

Lakini kama hutaki mwenzako aguse simu yako, tayari unampa sababu za kuanza kuhisi kuna kitu au jambo unaficha.

Hivyo, msingi wa imani ni kuwa mkweli, muwazi, na kutokufanya kile ambacho hupaswi kufanya.
 
Umewahi kua na mwanamke ambaye akipiga simu usipopokea inafuata meseji ya kukuita malaya? Au mwanaume anayemuuliza mwanamke kila muda alipo na kukasirika akiona anaongea na mwanaume mwengine.

Hiyo mifano miwili ndiyo ya watu wanaoshika simu za watu day in day out.

Kustaarabika ni kua mkweli na muwazi na kuheshimu faragha ya mwenza wangu, sishiki simu kwakua najihesabia nimestaarabika.
 
Mjadala huu ni mpana sana mbaya zaidi hakuna majibu yenye kujitosheleza, kila mmoja anasababu zake zinazo mtosha yeye na si rahisi mwenza wake nae akatosheka nazo.

Kwenye ulimwengu wa sasa 90% ya taarifa zako unashea kupitia simu yako.

Si kila kitu unapswa kushea na mwenza wako, mfano: Kazi, watu katika idara nyeti za fedha, upelelezi, ulinzi na usalama hata udactari maana unabeba siri za Afya za viongozi na hata watu wa kawaida.
Nature ya kazi yako inaweza kuwa sababu Kwa mwenza wako kutoshika sim yako.

Family and personal issues nazo zinanafasi kubwa ktk huu usiri, maana si kila jambo lihusuyo familia yako unapaswa kushea na mwenza wako japo kushea nae si dhambi ila jambo lenyewe liko ktk stage gani? au mambo yako binafsi mipango yako, matarajio yako na changamoto ziko ktk hatua ipi kias cha mwenza wako nae kufahamu?

Lakini pia uwezo wa kuhimili au kustahmili yale unayopitia kama changamoto je mwenza wako anakifua cha kuyabeba pindi akiyaona kwenye simu yako?

Madhaifu binafs, Bosi kakutusi Kwa uzembe kazini, ama business partner kakutolea maneno ya dhihaka haya yote, Mrs wako anayaona!! Lazima itakushushia heshima kias flani japo ni mwenza wako ila kila mmoja anafaham mapungufu ya mtu alienae, "kuna siku mkeo anaweza kuvurugwa akakwambia ndio maana na Bosi anakutukana.

Kuaminiana ni Jambo muhim sana ila hakuhitaji kuchunguzana ili kuleta uaminifu, maana penye uchunguzi tayari panatatizo.
 
Na hio nafasi ndio mnayoitumia ku entertain watongozaji na ma crush wenu makazini wanaowainamisha kwenye siti za magari na vyooni huku mkiitana bae bila aibu!
Wewe utakuwa umechanganyikiwa si bure!Kwa maana hio kwa usemi wako na upande wa pili anafanya hivohivo au?Hovyoo!Kama mtu anataka kufanya yake huwezi kumzuia kwa kupekenyua sim yake period!Atafanya tu!!Endeleeni kujidanganya!

And i dont understand why u think every comment is funny because it isnt indeed!
 
Mjadala huu ni mpana sana mbaya zaidi hakuna majibu yenye kujitosheleza, kila mmoja anasababu zake zinazo mtosha yeye na si rahisi mwenza wake nae akatosheka nazo.

Kwenye ulimwengu wa sasa 90% ya taarifa zako unashea kupitia simu yako.

Si kila kitu unapswa kushea na mwenza wako, mfano: Kazi, watu katika idara nyeti za fedha, upelelezi, ulinzi na usalama hata udactari maana unabeba siri za Afya za viongozi na hata watu wa kawaida.
Nature ya kazi yako inaweza kuwa sababu Kwa mwenza wako kutoshika sim yako.

Family and personal issues nazo zinanafasi kubwa ktk huu usiri, maana si kila jambo lihusuyo familia yako unapaswa kushea na mwenza wako japo kushea nae si dhambi ila jambo lenyewe liko ktk stage gani? au mambo yako binafsi mipango yako, matarajio yako na changamoto ziko ktk hatua ipi kias cha mwenza wako nae kufahamu?

Lakini pia uwezo wa kuhimili au kustahmili yale unayopitia kama changamoto je mwenza wako anakifua cha kuyabeba pindi akiyaona kwenye simu yako?

Madhaifu binafs, Bosi kakutusi Kwa uzembe kazini, ama business partner kakutolea maneno ya dhihaka haya yote, Mrs wako anayaona!! Lazima itakushushia heshima kias flani japo ni mwenza wako ila kila mmoja anafaham mapungufu ya mtu alienae, "kuna siku mkeo anaweza kuvurugwa akakwambia ndio maana na Bosi anakutukana.

Kuaminiana ni Jambo muhim sana ila hakuhitaji kuchunguzana ili kuleta uaminifu, maana penye uchunguzi tayari panatatizo.
Wewe umeongea vizuri sana 👏👏Watu wengine akili zao ni fupi wanafikiri kila kitu mwenza wako anapaswa kujua!
 
Hizi simu ni mtihani sana. We pekua tu lakini bomu la machozi likikukuta utakuwa mwenyewe. Kunasiku nimejilalia zangu bas wife akachukua simu anaperuziperuzi mara ghafla meseji ya bint fulani ikaingia. Inasema '' mambo''. Akaijibu na kuendelea kuchati bila yule bint kujua kuwa hachati na mm. Basi kunakipengele wife akamhadaa yule bint kuwa ""mara ya mwisho ilikua tamu? binti akaijibu ndio, then akamuuliza tukutane tena lini? binti akaijibu ni wewe tu. Du nkaamshwa ghafla na maswali kama yote, mm chakujibu sina ila ndio kipindi ambacho almanusra ndoa ivunjike kijinga sana na kiukweli yule bint alikuwa anajibu kimasihara na alikua mfanyakazi mwenzangu lakini kila nilivyojitetea sikueleweka kbsa lakini mwishowe nikajisemea Mimi ni mwanaume ngoja nikae kimya nione mwisho wake. Japo tunaishi lakini imekuwa kama dowa.
 
Kuna watu kupitia simu wamejua kama wanaume zao wanataka kuchukua mkopo nyumba ya familia. Wengine wamejua kama wenzao wameathirika.
Mahusiano yanatakiwa yajengwe na misingi ya imani.Kama mtu anakuficha vitu kama hivo na unakuja kuvijua kupitia kwenye sim unatakiwa uamke coz something is seriously wrong somewhere!Kuna vitu havipaswi kuwa siri!
 
Back
Top Bottom