Mkuu sorry kwa kukuharibia naomba piga picha label yake iweke hapa ili watu waone ni kitu gani hasa wananunua. Hakuna analysis yoyote kuonesha kwamba hio ni mbolea kwa maana ya nitrogen, potassium, phosphorus n.k.
Kuhusu surfactant kufanya maji kupenya kwenye udongo, effect ni yake ni ndogo sana kiasi cha kuitwa haipo tu. Soil structure nzuri yenye mchanganyiko mzuri wa silt, sand, organic matter, na kiasi kidogo cha clay, granular soil structure inatosha kabisa katika kufanya maji yapenye kwa urahisi. Weka hio surfactant kwenye clay soil hakuna matokeo yoyote, udongo utafunga na kuzuia maji yasipenye.