Kwanini wanaume ni waoga kiasi hiki

Brother hakuna tofauti katika wanawake wawe wamesoma au hawajasoma..

Bottom line utarudi saa ngapi, umechelewa ..

Huwezi kumuogopa mwanamke
 

hakuna wanaume ambao hawajitambiui? Hawajiamini?
Hakuna wanaume wanaofukuza wake zao kila kukicha kwa sababu tu hana kitu au katoka familia masikini?
Hakuna wanaume wanaokimbia wanawake wenye pesa kwa 'hofu' tu kuwa anahisi atatawaliwa?
Unataka kusema hayo yote hayatokei mtaani? Sio swala la mtazamo ndg ni swala la yanayotokea mitaani?

Ni wanaume wangapi wenye guts za kuanzisha mahusiano na wanawake wenye pesa?(unless serengeti boys?)

face the reality
 
Unadhani kwa nini most men hawasamehi wake zao wakicheat; kwa sababu hawana dependence kwao. Wanawake wengi tu wanavumilia sababu hawana altenative. Kwa hiyo wana opt kuishi maisha ya mateso kwa kuwa hawana namna na si kwa kuwa wanapenda.

 
Hawa ndo wakisikia wife kapewa ukatibu mkuu BP inapanda.

Hivi mnadhani hao wenye wake wenye vyeo walipowaoa walikuwa navyo?? Mkeo cheo kikipanda akakuzidi kipato utampa talaka??? Poleni; wajanja wanaangalia mbali.

hahaha mwanamke ni mwanamke tuuu! pesa na elimu hazinaga nafasi kwenye mapenzi ila huwa zinaletaga tu vitabia vidogovidogo havina effect kwenye mapenzi.Acha woga thubutu ,utaweza na utafanikiwa .all the best
 

Wanaume wasiojiamini wapo, ila si wengi kiasi cha kusema kila mwanamke mwenye shule/fedha/madaraka anakosa wanaume eti sababu wote hawajiamini.

Hakuna mwanaume anayefukuza mke eti sababu katoka familia maskini!!! Hii haipo. Alimchumbia akiwa maskini hadi akamuoa akiwa maskini. Akimfukuza huko baadaye, sababu si umaskini - ni matatizo ya kimahusiano ambayo yanaweza kumkumba yeyote!!

Hakuna mwanaume anayekimbia kwa kuhisi atatawaliwa!! Wanaume wengi (Nasema wengi) huwa ni pragmatic. Anakaa na mke kwanza, vitabia vile vikishaanza kuwa common ndo mme anasepa. Hapa kilichomfukuza si kuhisi atatawaliwa no. Wanaume hawaamui kwa kuhisi. Wanaona ndo wanaamua.

Wanaume wengi wana guts za kuanzisha mahusiano na mwanamke yeyote hata awe na fedha au elimu au madaraka makubwa kivipi. Hata hao unaowaita Serengeti boys unadhani si wanaume? Usiniambie eti Serengeti boys wana guts kuliko baba zao!! Baba zao wameyaona ndo maana baadhi ya ngoma wanawaachia Serengeti boys!!
 
Unadhani kwa nini most men hawasamehi wake zao wakicheat; kwa sababu hawana dependence kwao. Wanawake wengi tu wanavumilia sababu hawana altenative. Kwa hiyo wana opt kuishi maisha ya mateso kwa kuwa hawana namna na si kwa kuwa wanapenda.

Nyumba kubwa,

Usinishawishi eti wanaume wengi hawawasamehi wake zao waki-cheat. Hizi nyumba zina mengi. Wanaume wengi, nasema wengi sana wanaojua kuwa wake zao wanawacheat wanawasamehe tu. Yaani nikuhakikishie wanaume wengi wanawasamehe wake zao kwa makosa ya cheating, tena wengine wanalea hata watoto ambao wanajua kabisa si wa kwao.

Wanaume wanaochukua hatua ya kufukuza wake zao, hawafanyi hivyo eti sababu hawawategemei hao wake zao!! No way. wanafanya hivyo kutokana na hali halisi ya tukio lenyewe na mwenendo mzima wa mahusiano ulivyokuwa! Ni vigumu sana kwa mwanaume kumwacha mkewe kuliko ilivyo vigumu kwa mke kumwacha mmewe!!

Yaani usidanganyike eti wanaume hawajui matendo ya cheating za wake zao na wakawasamehe. Tena mwanaume akisamehe ni kimya kimya hawezi kumwambia hata rafiki yake wa karibu mno. Ila wanawake akimsamehe mumewe, lazima mashosti zake na au mtaa mzima ujue kuwa mke alikuwa anacheatiwa hili ndo tatizo.
 
kwangu mwanake ni mwanamke...huwa siangalii how much she got or how beutiful she is or how powerful she when am attracted to her! i dont luz any chance.
 

serengeti boys wana guts kuliko baba zao kwa sababu wapo kibiashara zaidi. Mwanaume anayetaka kusettle na mwanamke wengi wao hawataki wanaume wenyemali, tofautisha hawa na serengeti boys.

Hujawahi ona wanawake wakifukuzwa na kunyanyaswa kisa umasikini? Labda unaishi ulimwengu wa peke yako. (ofcourse wanawake hawa hawaondoki kwa sababu kadha wa kadha mojawapo ni uvumilivu)

narudia tena kuna wanawake akiwa na fedha na mali wanaume huwaogopa kuwaoa/ tongoza kutokana na kutokujiamini, woga wa kudhani hawatakua na sauti. Na hili tunaliona na linatokea huku mitaani kwetu. Its the reality
 
mimi daily nawatafuta hao wenye pesa!km yupo humu mmoja wao,tuwasiliane tu....
 
....kutojiamini na ujinga tu....badala kufikiria utapambana vipi na maisha kuyaweka kwenye malengo uloyakusudia, unafikiria elimu au cheo cha mkeo kitakukathiri vipi maishani...

maisha bila malengo ni sawa na kutupa ngumi gizani!
 
....kutojiamini na ujinga tu....badala kufikiria utapambana vipi na maisha kuyaweka kwenye malengo uloyakusudia, unafikiria elimu au cheo cha mkeo kitakukathiri vipi maishani...

maisha bila malengo ni sawa na kutupa ngumi gizani!

Kweli kabisa!
 
Ndio maana mwanaume akaitwa provider, kazi yake kubwa ni kuprovide kwa familia awe ana pesa au hana pindi majukumu yanapobadilika na mama kuwa main provider basi mwanaume hujiskia vibaya, sio mbaya sana mwanamke kua provider kinachochukiza na kuwakimbiza wanaume wengi ni dharau zinazoambatana na huduma hizo, utaskia mwanaume gani suruali tu huna lolote....ni hayo tu.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…