Aiseee....kama ulikuwepo vile, mimi mwenyewe hata sijui kwanini sijaoa/siowi mpaka sasa. Tena wala sijisikii hamu ya kufanya hivyo na wala sina hofu kwanini sijaoa mpaka sasa. Labda wataalam mtutajie umri wa mwisho kuoa labda ntaogopa nifanye fasta. Though ndoa za siku hizi macomplications kibao(vikao, kamati, ukumbi, michango, sijui suti, saloon, vyakula, vinywaji, kadi, sijui ninini na ninini tena) mambo kibao hata kuanziasha kampuni kuna nafuu!
Mara ndugu sijui waende wapi mara wapelekwe sijui kwa nani.....mambo lukuki hadi ndoa inaisha uko hoi! Mweeeee....mie hapana ngoja nisubiri subiri kwanza labda ajilete mwenyewe twende bomani then church, tena huko kwa wazazi wake akamalize mwenyewe mie ntampa mpunga tu apeleke mambo ya sijui kupigana faini, sijui mila amalize mwenyewe hukohuko.[/QUOTE]
Nashukuru nimeanza siku kwa kicheko lol!