Kwanini wanaume wafupi wanadharauliwa?

Kwanini wanaume wafupi wanadharauliwa?

Ni psychologia tu mkuu na nyie wafupi kujidharau wenyewe maana muda wote mnahisi mnakuwa treated kutokana na kimo chenu
 
Mtoa mada jikubali tu,

Angalia watu kama Tyson, Messi,

Wapo wengi tu wanajikubali,,

Ila ndo ivo uwezi kuwa mlizi wa rais kama ni mfupi
Najitahidi pia kuwa hubiria wafupi wenzangu kwamba hakuna haja ya kuwa na wivu kuhusu ulefu sababu tuna extra ability tutumie kidogo tulichonacho kwa furaha
 
Hivi huu ulefu na ufupi mnaouongelea hapa ni kuhusu pesa au kimo? Maana kama ni kimo mtakuwa watu wa ajabu maana sasa ni zama za pesa na madaraka tu ndio yatakayokuondoa kwenye hiyo inferiority complex
 
Hapana mzee mi nachojua kuzauriwa na kuheshimika kunatokana na wewe umejiwekaje kwenye hiyo jamii inayokuheshimu au kukudharua so uwe mrefu ama mfupi hakikisha unaishi maisha ya kukujengea heshima na pesa ili jamii inayokuzunguka ikose sababu ya kukudharau.
Kuwa mfupi hakuleti dharau kinacholeta dharau ni muonekano wako,maneno na vitendo vyako vya kila siku.BOSS wangu ni mfupi ili ni mtu mwenye busara mpaka unamtamani yaani.
Mkuu Pana ukweli kukosea kutype tu ndio kulete kuzalauliwa
 
Tatizo si lao peke yao,,, ni la jamii nzima.
Ilianza tangu enzi hizo,,,, kakake Daudi(Eliabu) alikuwa ni mrefu kuliko Daudi, basi watu wote wakasema huyu anafaa kuwa mfalme wa Israel.



Jamii imekuwa ikitukuza vitu virefu ,,, hata wanyama,,,, Twiga anaheshimika sana(sihitaji kuweka reference)


Kwa maoni yangu, tuliache kama lilivyo,,, pengine hii ni NATURE.
MUNGU alivyoumba viumbe vyote alisema tazama vyote ni vyema Tena ni vyakupendeza. Swali la kujiuliza kwa Nini walefu wanaheshimika kuliko sisi wafupi , bila hata ya kujieleza kabisa watu walefu huonekana Bora kuliko wafupi.

Matatizo makubwa ya watu wafupi;

1. KUKOSA MOYO WA SHUKRANI
Sio kitu laisi kwa mtu mfupi kushukuru kwa Jambo lolote zuli au baya analofanyiwa , baya moja utakalo mfanyia linaweza futa mema yote uliyowai mfanyia

2. TAMAA YA MACHO
Watu wafupi tunasumbuliwa na pepo la Tamaa ya kujulikana na kuonekana mbele za watu Kama sisi ni Bora kuliko wengine, tatizo hili uzalisha matatizo madogo mengine Kama; kujipendekeza , kuongea Sana , ubishi , kiherehere , uongo

3. KUHISI TUNAONEWA / KUHISI HATUJALIWI
Tatizo hili linatutesa Sana watu wafupi , haswa kwenye mahusiano ya kijamii na kimapenzi. Tunajikuta Kila siku tunakua single na kuanza upya , hatakama wapenzi wetu watafanya mistakes ndogo tu. Hali ya kuhisi hatuwezi kupendwa inatutafuna hii ni kwa jinsia zote .

4. UVIVU
Hali ya kuona juhudi zetu watu hawazitambui inatutafuna Sana watu wafupi na kuzalisha roho ya uvivu na kujikuta tunakua na maendeleo ya midomoni.

5. KUTO KUKUBALIANA NA UHALISIA KWAMBA SISI NI WAFUPI
Ukishajua wewe ni mfupi wa kimo haina maana una uwezo mdogo wa kilakitu mfano uwezo wa kufikili vizuri, kukosa msimamo, kufanya kazi , hekima nk


USHAURI
Kuwa mfupi sio dhambi Bali ni zawadi toka kwa MUNGU kwamba upo Bora ivyo ulivyo na unaweza ukiamua kutimiza ndoto zako . INUKA NA UTHUBUTU.
 
Back
Top Bottom