SoC02 Kwanini Wanaume wanaongoza kwa kujiua?

Stories of Change - 2022 Competition

2Laws

Member
Joined
Sep 4, 2022
Posts
37
Reaction score
38
suicide.jpg

UTANGULIZI
"Kila mwaka watu 703,000 wanajiua idadi ya wanaume ikiwa mara tatu ukilinganisha na wanawake" (Shirika la afya Duniani)

Pamoja na kuwa baadhi ya jamii zinaamini mwanaume kujiua ni hatua ya ujasiri; Mkazo/Msongo wa mawazo,Kukosa kazi,Kutengwa/Unyanyapaa,mizozo ( hasa katika mahusiano),kupoteza wapendwa,Unyanyasaji wa kijinsia,Wahusika wa mapenzi ya jinsia moja Vimechangia zaidi kama katika matukio ya kujiondolea uhai miongono mwa wanaume wengi ulimwenguni.

KIINI
Kwa kuzingatia Tanzania Pekee tutaangazia sababu hizi kwa muktadha wa mazingira yetu kwani sababu hizi zinaonyesha kuwa tofauti na nchi zenye maendeleo na sera tofauti na za hapa kwetu;

Mkazo/Msongo wa mawazo ni jambo lisilo kwepeka kwa kila mtu, lakini namna ya kukabiliana nao hutofautiana miongoni mwa watu na hii huchangia tofauti ya matokeo ikiwa wengine wakifanikiwa kushinda na kuishi maisha ya furaha baada ya hapo, wengine wakiwa na matokeo hasi yasiyowza kurekebishwa ya kiafya, kiakili na kijamii na wengine kufikia uamuzi wa kukatisha maisha yao. Kwa wasioelewa maana ya mkazo, Mkazo ni jinsi tunavyotenda tunapokuwa chini ya shinikizo au kutishwa. Kwa kawaida hutokea tukiwa katika hali ambayo hatuhisi kuwa tunaweza kuisimamia au kuidhibiti.

Tunapopata mfadhaiko, inaweza kuwa kama: Mtu binafsi, kwa mfano unapokuwa na majukumu mengi ambayo unatatizika kuyasimamia. Wanaume wanokua katika ndoa hukabiliwa na Mkazo na kwakuwa sio rahisi kuzungumza haya na watu kazini au mahala pa mapumziko wengi huishia kunywa pombe na kuzini wakidhani wataweza kusahau yanayo wakabili. Matokeo ni kuwa mkazo hurejea mara na maumivu huongezeka mara dufu na wanapoendelea kukosa msaada huchoka kuvumila na kufikia maamuzi ya kukatisha maisha yao wakidhani wanazuia matokeo mabaya zaidi ama wanapata pumziko la moyo.

Japo Kuzungumza hakuwezi kubadilisha. Lakini wakati mwingine ndicho anachotaka zaidi, kumwambia mtu; mara nyingi, ingawa, anataka tu kuepuka hisia hizo za kutisha, kutoroka mwenyewe, kwa hivyo asingekuwa na maumivu, woga wala ubaya.

Kukosa kazi ni tatizo kubwa si tu kwa Tanzania. maendeleo ya sayansi na teknolojia yalikusudiwa zaidi kuongeza fursa kwa vijana lakini kwa kiasi imepunguza uhitaji wa wafanyakazi wengi hasa katika viwanda kwani kazi nyingi zinafanywa na mashine. Wengi tunasoma katika mazingira magumu na maumivu wayoyapata wazazi au wale wanao tusomesha huweka hatia na deni moyoni mwa kijana.

Anapomaliza masomo tegemeo ni kuwa yale mateso ya kusoma, njaa, kukosa mavazi na pumziko vingekoma tuu kwa kupata ajira na mshahara, kuwa wale walioumia wakitusomesha watatibiwa majeraha yao. Sera ya kujiajiri bado haina wepesi kwa vijana wa kitanzania kutokana na mfumo wetu wa elimu na ni mada nyingine pana kabisa, lakini embu fikiri! mkazo atakaokua nao, uhitaji atakaoendelea kuwa nao baada ya kuvumilia kipindi kirefu cha masomo ni wazi sio rahisi kuendelea kuwa na nguvu na subira. lakini Dunia inamtaka aendelee kuwa hodari hata mwisho na anapokosa msaada na faraja kukatisha maisha kunaweza kuonekana kama chaguo bora.

Kutengwa/Unyanyapaa kwa sehemu nyingine inaongeza hali ya upweke na unaweza kuelewa tofauti na wasichana, watoto wa kiume hushawishika sana kujiunga na makundi kwani wanachohitaji ni kuwa wanakubalika na watu fulani. Hali ya kutengwa na kunyanyapaliwa hasa shuleni huchochea upweke na mawazo yakuwa wao ni watu wasiokubalika katika jamii.Tofauti labda ya kimaumbile/hali ya ulemavu, tatizo la kisaikolojia/kiakili, udhaifu fulani ama kukosa kitu ambacho hupewa kipaumbele sana na wanaume wengine hatengeza tabaka la wakandamizwao na kwa kuwa sio rahisi wao kukiri udhaifu na kuomba msaada wengi huishia kutafuta namna ya kutoroka aibu, fedheha na mkandamizo huo na kujiua huonekana kama njia bora wakati huo.

Mizozo ya kifamilia kw akiasi, mizozo ya mahusiano yakiwa mbele katika kuchangia matukio ya kujiua ni changamoto kubwa kwa wanaume kuliko ilivyo kwa wanawake na labda ni kwa kuwa wnawake huwa na rafiki wakueleza uchungu wao na kulia au labda ni kwa kuwa wanaume ndio hutoa zaidi katika kipindi hiki. Mfano wawili wanaweza kuwa wanachuo, aidha wana mkopo au wadhamini lakini unakuta mwanaume ndie hulipa kodi na kugharamia maisha ya mwanamke anayempenda bila kujali yeye anakosa nin wakati huo.

Pale wanaposalitiwa maumivu yasioelezeka, fedheha na majuto huwalemea kiasi cha kutovumilika. Hata katika ndoa kuna wanaume wanapigwa na wake zao, kuna wanaoteswa kwa kunyimwa haki kama mume japo wanaoongoza katika utetezi ni wanawake. Kwa kuwa Kama mwanaume huwezi kulia mbele ya wanaume wenzako kisa mapenzi mtaani wanasema ni "umama" hivyo hujikaza tu. Mambo/siri yasiyosemwa yanaumiza zaidi.

Unyanyasaji wa kijinsia na washiriki wa mapenzi ya jinsia moja nitazungumzia kwa pamoja. Nimetembela vituo vya kulea watoto Mwanza na Dar Es Salaam na nimeona ukatili wanofanyiwa watoto, kuna waliolawitiwa tena na watu wa karibu, wengine wamechomwa sehemu za siri kwa moto vitendo ambacho hakifai kulinganisha na Unyamma kwani kwenye hifadhi za Taifa sijawahi sikia wala kushuhudia wanyama wakifanya vitendo hivyo.

Hizi kumbukumbu za ukatili huathiri sana saikolojia ya vijana na wengi hukosa maana ya kuishi kutokana na ubaya waliopitia katika utoto wao na kitu kidogo mabacho kinaweza kutonesha vidonda hivyo vyenye kumbukumbu isiofutika hupelekea kuchukua hatua za kujiua. Jamii yetu haikubali mahusiano ya jinsia moja lakini wahusika wapo na ni wengi.

Hofu ya kutambulika hadharani, kupoteza nafasi yao katika familia na jamii na namna jamii itakavyowachukulia ikiwa siri yao itafichuka huweka hofu kubwa ambayo endapo itatokea yakawa wazi; ili kukwepa kunyanyapaliwa, fedheha, aibu na unyanyasaji kuondoa uhai wao inaweza kuwa wazo bora kama watakosa msaada. Nini kifanyike? tukubaliane na sera ya haki za binadamu inavyosema/ Je tutaandaa jamii gani ya kesho ikiwa tutakubaliana na hilo? unaweza kuona utata katika kutatua hii changamoto.

1662996237879.jpeg

Hitimisho
Biolojia inasema kulia huondoa uchungu ndani lakini sio rahisi kuona chozi la mwanaume, hawawezi kuwa watu wa hisia kwani jamii imemchora mwanaume kuwa hodari na jasiri.

Ninaamini katika kusikilizana kwani kila mmoja ana haki hio. Ninaamini katika upendo kama njiaa kuu ya kutatua changamoto hii kubwa.

Tuanzishe vkundi/dawati la utetezi la wanaume? inaweza kuwa hoja yenye maana sana. Wazazi wana ukaribu wa kutosha na watoto wao kiasi cha kujua siri zinazowaumiza wana wao? tunaweza kusema hapana kwani ni wazi kabisa sasa wazazi si rafiki namba moja kwa watoto tena.

Je mashuleni kuna wataalamu wa saikolojia na washauri rafiki? kama wapo ni kwa upungufu mkubwa, Unaweza kuona uhitaji wake kutetea vijana kwnye changamoto zao wanapokuwa masomoni.

Je una mapendekezo? fanya mawazo yako yafike kwenye mamlaka husika kwa kutoa maoni yako hapa.

Je, nini kifanyike? Japo wanawake wanongoza kuwa na mawazo ya kujiua, wanaume wanaojiua ni mara tatu zaidi ya wanawake.
 
Upvote 9
Nashukuru sana
Habari yako ndugu 2Laws.

Hongera kwa nakala nzuri yenye mawaidha na tija kwa jamii.

Kura yangu umepata!!

Nikiamini katika uchakataji wako wa mambo na uwezo wako wa fikra na ubunifu, naomba ukipendezwa, nipate mawazo yako au mapendekezo juu ya nakala ihusuyo

Ahsante!!
 
Kupewa majukumu asiyo yaweza!
Tangu anazaliwa mtoto wa kiume anasifiwa kuwa anaweza na kujua yote kuliko mtoto wa kike na ni culture zote duniani![emoji24][emoji24][emoji24]
Jinsia zote ziwe sawa tangu utotoni, maana kuna makabila mtoto wa kike hata shule hapelekwi, imani ya wazazi ni kuwa mtoto wa kiume akisha kuwa atawatunza dada zake au mtoto wa kike ataolewa hivyo hamna sababu ya kumuendeleza mke wa watu wengine!
Inasikitisha sana sana, wachaga wanao sana upumbavu huu!
Dawa ni kubadilika watoto wa kiume na wakike ni sawa kwenye maendeleo jamani [emoji29]
 
View attachment 2350114

View attachment 2354681

Hitimisho
Biolojia inasema kulia huondoa uchungu ndani lakini sio rahisi kuona chozi la mwanaume, hawawezi kuwa watu wa hisia kwani jamii imemchora mwanaume kuwa hodari na jasiri.

Ninaamini katika kusikilizana kwani kila mmoja ana haki hio. Ninaamini katika upendo kama njiaa kuu ya kutatua changamoto hii kubwa.

Tuanzishe vkundi/dawati la utetezi la wanaume? inaweza kuwa hoja yenye maana sana. Wazazi wana ukaribu wa kutosha na watoto wao kiasi cha kujua siri zinazowaumiza wana wao? tunaweza kusema hapana kwani ni wazi kabisa sasa wazazi si rafiki namba moja kwa watoto tena.

Je mashuleni kuna wataalamu wa saikolojia na washauri rafiki? kama wapo ni kwa upungufu mkubwa, Unaweza kuona uhitaji wake kutetea vijana kwnye changamoto zao wanapokuwa masomoni.

Je una mapendekezo? fanya mawazo yako yafike kwenye mamlaka husika kwa kutoa maoni yako hapa.

Je, nini kifanyike? Japo wanawake wanongoza kuwa na mawazo ya kujiua, wanaume wanaojiua ni mara tatu zaidi ya wanawake.

Ni sawa na kusema kwa nini kisu kinaua, na chenyewe hakifi, wanawake ndo wanasababisha wanaume wajiue! Wao hawawezi kufa.
 
Unaloema ni halisi kabisa kuna uhitaji mkubwa wa mabadiliko kayika jamii zetu kama tutazungumzia usawa basi tusizungumzie kutetea haki za wanawake tuzunumzie na wanaume pia kwani wanavyozidi kuvumilia muda mrefu wanazidi kuchoka na kukata tamaa. Nashukuru sana kwa maoni yako ningefurahikupata kura yako pia. Asante
 
Ni sawa na kusema kwa nini kisu kinaua, na chenyewe hakifi, wanawake ndo wanasababisha wanaume wajiue! Wao hawawezi kufa.
kwa kiasi kikubwa wamechangia ni kweli hasa wanandoa na wapenzi japo wakati mwingine wote ni waathirika lakini kuna sababu inayowafanya wanaume wengi kuishia kujiua na sio wanawake. Nashukuru kwa maoni yako ningefurahi kupata kura yako pia.Asante
 
View attachment 2350114
UTANGULIZI
"Kila mwaka watu 703,000 wanajiua idadi ya wanaume ikiwa mara tatu ukilinganisha na wanawake" (Shirika la afya Duniani)

Pamoja na kuwa baadhi ya jamii zinaamini mwanaume kujiua ni hatua ya ujasiri; Mkazo/Msongo wa mawazo,Kukosa kazi,Kutengwa/Unyanyapaa,mizozo ( hasa katika mahusiano),kupoteza wapendwa,Unyanyasaji wa kijinsia,Wahusika wa mapenzi ya jinsia moja Vimechangia zaidi kama katika matukio ya kujiondolea uhai miongono mwa wanaume wengi ulimwenguni.

KIINI
Kwa kuzingatia Tanzania Pekee tutaangazia sababu hizi kwa muktadha wa mazingira yetu kwani sababu hizi zinaonyesha kuwa tofauti na nchi zenye maendeleo na sera tofauti na za hapa kwetu;

Mkazo/Msongo wa mawazo ni jambo lisilo kwepeka kwa kila mtu, lakini namna ya kukabiliana nao hutofautiana miongoni mwa watu na hii huchangia tofauti ya matokeo ikiwa wengine wakifanikiwa kushinda na kuishi maisha ya furaha baada ya hapo, wengine wakiwa na matokeo hasi yasiyowza kurekebishwa ya kiafya, kiakili na kijamii na wengine kufikia uamuzi wa kukatisha maisha yao. Kwa wasioelewa maana ya mkazo, Mkazo ni jinsi tunavyotenda tunapokuwa chini ya shinikizo au kutishwa. Kwa kawaida hutokea tukiwa katika hali ambayo hatuhisi kuwa tunaweza kuisimamia au kuidhibiti.

Tunapopata mfadhaiko, inaweza kuwa kama: Mtu binafsi, kwa mfano unapokuwa na majukumu mengi ambayo unatatizika kuyasimamia. Wanaume wanokua katika ndoa hukabiliwa na Mkazo na kwakuwa sio rahisi kuzungumza haya na watu kazini au mahala pa mapumziko wengi huishia kunywa pombe na kuzini wakidhani wataweza kusahau yanayo wakabili. Matokeo ni kuwa mkazo hurejea mara na maumivu huongezeka mara dufu na wanapoendelea kukosa msaada huchoka kuvumila na kufikia maamuzi ya kukatisha maisha yao wakidhani wanazuia matokeo mabaya zaidi ama wanapata pumziko la moyo.

Japo Kuzungumza hakuwezi kubadilisha. Lakini wakati mwingine ndicho anachotaka zaidi, kumwambia mtu; mara nyingi, ingawa, anataka tu kuepuka hisia hizo za kutisha, kutoroka mwenyewe, kwa hivyo asingekuwa na maumivu, woga wala ubaya.

Kukosa kazi ni tatizo kubwa si tu kwa Tanzania. maendeleo ya sayansi na teknolojia yalikusudiwa zaidi kuongeza fursa kwa vijana lakini kwa kiasi imepunguza uhitaji wa wafanyakazi wengi hasa katika viwanda kwani kazi nyingi zinafanywa na mashine. Wengi tunasoma katika mazingira magumu na maumivu wayoyapata wazazi au wale wanao tusomesha huweka hatia na deni moyoni mwa kijana.

Anapomaliza masomo tegemeo ni kuwa yale mateso ya kusoma, njaa, kukosa mavazi na pumziko vingekoma tuu kwa kupata ajira na mshahara, kuwa wale walioumia wakitusomesha watatibiwa majeraha yao. Sera ya kujiajiri bado haina wepesi kwa vijana wa kitanzania kutokana na mfumo wetu wa elimu na ni mada nyingine pana kabisa, lakini embu fikiri! mkazo atakaokua nao, uhitaji atakaoendelea kuwa nao baada ya kuvumilia kipindi kirefu cha masomo ni wazi sio rahisi kuendelea kuwa na nguvu na subira. lakini Dunia inamtaka aendelee kuwa hodari hata mwisho na anapokosa msaada na faraja kukatisha maisha kunaweza kuonekana kama chaguo bora.

Kutengwa/Unyanyapaa kwa sehemu nyingine inaongeza hali ya upweke na unaweza kuelewa tofauti na wasichana, watoto wa kiume hushawishika sana kujiunga na makundi kwani wanachohitaji ni kuwa wanakubalika na watu fulani. Hali ya kutengwa na kunyanyapaliwa hasa shuleni huchochea upweke na mawazo yakuwa wao ni watu wasiokubalika katika jamii.Tofauti labda ya kimaumbile/hali ya ulemavu, tatizo la kisaikolojia/kiakili, udhaifu fulani ama kukosa kitu ambacho hupewa kipaumbele sana na wanaume wengine hatengeza tabaka la wakandamizwao na kwa kuwa sio rahisi wao kukiri udhaifu na kuomba msaada wengi huishia kutafuta namna ya kutoroka aibu, fedheha na mkandamizo huo na kujiua huonekana kama njia bora wakati huo.

Mizozo ya kifamilia kw akiasi, mizozo ya mahusiano yakiwa mbele katika kuchangia matukio ya kujiua ni changamoto kubwa kwa wanaume kuliko ilivyo kwa wanawake na labda ni kwa kuwa wnawake huwa na rafiki wakueleza uchungu wao na kulia au labda ni kwa kuwa wanaume ndio hutoa zaidi katika kipindi hiki. Mfano wawili wanaweza kuwa wanachuo, aidha wana mkopo au wadhamini lakini unakuta mwanaume ndie hulipa kodi na kugharamia maisha ya mwanamke anayempenda bila kujali yeye anakosa nin wakati huo.

Pale wanaposalitiwa maumivu yasioelezeka, fedheha na majuto huwalemea kiasi cha kutovumilika. Hata katika ndoa kuna wanaume wanapigwa na wake zao, kuna wanaoteswa kwa kunyimwa haki kama mume japo wanaoongoza katika utetezi ni wanawake. Kwa kuwa Kama mwanaume huwezi kulia mbele ya wanaume wenzako kisa mapenzi mtaani wanasema ni "umama" hivyo hujikaza tu. Mambo/siri yasiyosemwa yanaumiza zaidi.

Unyanyasaji wa kijinsia na washiriki wa mapenzi ya jinsia moja nitazungumzia kwa pamoja. Nimetembela vituo vya kulea watoto Mwanza na Dar Es Salaam na nimeona ukatili wanofanyiwa watoto, kuna waliolawitiwa tena na watu wa karibu, wengine wamechomwa sehemu za siri kwa moto vitendo ambacho hakifai kulinganisha na Unyamma kwani kwenye hifadhi za Taifa sijawahi sikia wala kushuhudia wanyama wakifanya vitendo hivyo.

Hizi kumbukumbu za ukatili huathiri sana saikolojia ya vijana na wengi hukosa maana ya kuishi kutokana na ubaya waliopitia katika utoto wao na kitu kidogo mabacho kinaweza kutonesha vidonda hivyo vyenye kumbukumbu isiofutika hupelekea kuchukua hatua za kujiua. Jamii yetu haikubali mahusiano ya jinsia moja lakini wahusika wapo na ni wengi.

Hofu ya kutambulika hadharani, kupoteza nafasi yao katika familia na jamii na namna jamii itakavyowachukulia ikiwa siri yao itafichuka huweka hofu kubwa ambayo endapo itatokea yakawa wazi; ili kukwepa kunyanyapaliwa, fedheha, aibu na unyanyasaji kuondoa uhai wao inaweza kuwa wazo bora kama watakosa msaada. Nini kifanyike? tukubaliane na sera ya haki za binadamu inavyosema/ Je tutaandaa jamii gani ya kesho ikiwa tutakubaliana na hilo? unaweza kuona utata katika kutatua hii changamoto.

View attachment 2354681

Hitimisho
Biolojia inasema kulia huondoa uchungu ndani lakini sio rahisi kuona chozi la mwanaume, hawawezi kuwa watu wa hisia kwani jamii imemchora mwanaume kuwa hodari na jasiri.

Ninaamini katika kusikilizana kwani kila mmoja ana haki hio. Ninaamini katika upendo kama njiaa kuu ya kutatua changamoto hii kubwa.

Tuanzishe vkundi/dawati la utetezi la wanaume? inaweza kuwa hoja yenye maana sana. Wazazi wana ukaribu wa kutosha na watoto wao kiasi cha kujua siri zinazowaumiza wana wao? tunaweza kusema hapana kwani ni wazi kabisa sasa wazazi si rafiki namba moja kwa watoto tena.

Je mashuleni kuna wataalamu wa saikolojia na washauri rafiki? kama wapo ni kwa upungufu mkubwa, Unaweza kuona uhitaji wake kutetea vijana kwnye changamoto zao wanapokuwa masomoni.

Je una mapendekezo? fanya mawazo yako yafike kwenye mamlaka husika kwa kutoa maoni yako hapa.

Je, nini kifanyike? Japo wanawake wanongoza kuwa na mawazo ya kujiua, wanaume wanaojiua ni mara tatu zaidi ya wanawake.
Wow story yako inaendena na yangu, ngoja nikuunge mkono karibu pia kuunga kazi yanguhttps://www.jamiiforums.com/threads/vyanzo-na-jinsi-ya-kukabiliana-na-kujiua.2021976/
 
Aa ni kweli nafikiri wote tunakusudia kukomesha haya matukio. Asante
 
Haha nashukuru kama umeona hivyo nafikiri wengine pia wamepata chakuchukua hata kama hawakupiga kura kwani lengo kuu sio mm kushinda ni tatizo kupungua kama sio kukoma. Nashukuru sana
Kwa kwl tatizo kufumbuliwa ndio kitu kikuu zaidi ,mabadiliko ndio tija
 
Haha nashukuru kama umeona hivyo nafikiri wengine pia wamepata chakuchukua hata kama hawakupiga kura kwani lengo kuu sio mm kushinda ni tatizo kupungua kama sio kukoma. Nashukuru sana
Napigilia msumari.
Ikiwezekana na kushinda ushinde, wakupe pia ubunge wa viti maalum.
 
Back
Top Bottom