Mwanaume akitaka kumshusha thamani mwenzake atamuita jina la mwanamke, viungo vya mwanamke au kumpa sifa au hulka za wanawake kama namna ya kumuaibisha, kumtusi au kuonyesha udhaifu wake.
Naona limekua jambo la kawaida hasa huku mitandaoni na hata huko nje kwenye jamii zetu. Naomba nisaidiwe kuelewa, nini kimesababisha tufike hapa? (hasa kwa vijana) na kama si chuki, je wewe unaona ni nini?