Kwanini wanaume wengi siku hizi hupenda sana kubeba mafuta ya mgando mifukoni?

Kwanini wanaume wengi siku hizi hupenda sana kubeba mafuta ya mgando mifukoni?

Jamani Msiishie Tu Kucheka Hebu Toeni Basi Michango Yenu Kwani Hili TATIZO Linaongezeka Na Nahisi Wanaume Wa Sasa Wana Shida Iliyojificha Na Inayohitaji UFUMBUZI WA KUTUKUKA Ili Kulitatua. Tuwasaidieni Hawa Ndugu Zetu ( Wanaume ) Wenye Hii Tabia Tafadhalini.
 
Hii Tabia Ilianza Kidogo Sana Ila Kadri Siku Zinavyoenda Sasa Imeota MIZIZI Huku Ikileta Sintofahamu Katika Jamii.

Imegundulika Ya Kwamba Wanaume Wengi Sana Siku Hizi Wameanzisha Tabia Ya Kutembea Kama Siyo Kubeba MAFUTA Ya Mgando Katika Either Mifuko Yao Ya Suruali Or Katika Mabegi Yao Na Kuna Wengine Wameonekana Kabisa Kuwa Hawataki Masihara Ambapo Wao Huyabeba Yakiwa Yamezungushwa Katika Gazeti Kidogo Tu Yakiwa Yamechotwa Na Kuyahifadhi Katika Mifuko Yao Ya Mbele Ya Mashati.

Binafsi Nimekutana Nayo Sana Hii Hali Na Nimejiuliza Maswali Mengi Ni Kwanini au Wanaume Wenzangu Siku Hizi Wamekubwa Na Tatizo Gani Sijapata Jibu. Nawaombeni Ndugu Zanguni Kama Kuna Anayejua Nini Kipo Nyuma Ya Pazia Basi Si Vibaya " Akitiririka " Humu Ili Sote Tujifunze Kwani Yawezekana Kuna TATIZO Kubwa Lililojificha Na Pengine Linahitaji UFUMBUZI Wa Kina Na Wa Haraka Sana.

Karibuni Na Naomba Kuwasilisha.

Nawe kwa kupekuapekua mifuko ya watu. Ulifuata nini huko?
 
Back
Top Bottom