Kwanini wanaume wengi wa kilokole hawapo romantic?

Kwanini wanaume wengi wa kilokole hawapo romantic?

Hiyo Avatar unahisi mume wako huko barabarani kaona wangapi waliovaa hivyo?

unajua kuna mavaazi ya kuvaa mbele ya Mume tu,hayo ndio uyavae sasa

yani unanipokea ukiwa umevaa hivyo kama kwenye Avatar,itanichukua muda sana kuruhusu hisia.

Kuna makanisa watu wanavaa hivyo ulivyovaa ila kuna mavazi ukivaa hata shetani haruhusu uvae mbele ya mtoto.
Shikamoo CONTROLA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza nakupa pole , kwa unayopitia ...yanahitaji muda sana ...ila nakumbuka nilipokuwa nasoma theology pale chuo cha lake victoria bible college kuna masomo kwa wana ndoa tulikuwa tukifundishwa

Cha kwanza nachokushauri endelea sana kuomba ili mungu amfungue atambue nafac yake

Halafu zidisheni muda wa kukaaa wawili faragha chumbani au sebleni ...mkifanya hivyo mara kwa mara itaongeza ukaribu zaidi

Ukaribu ndio unaoleta mapinduzi ya kuwa marafiki , PASIPOKUWA NA URAFIKI KWA WANANDOA UJUE KUWA hakutakuwa na romatic yoyote

Tangulizeni urafiki tembeeni pamoja ,jioni zungumzeni mkiwa mnatizamana hiyo inaongeza nafac ya kila mtu kueleza dukuduku lake

sent from toyota Allex
mungu × Mungu√! Umesoma theology mkuu, nakukumbusha tu.

Ubarikiwe sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli nazidi kuamini mwanamke haridhiki hata umfanyie nini!!!
Na sijuwi kwanini wanafikiri ni rahisi kumbadilisha mwanaume wakati wakikumbuka ile package walioipenda iko hivyo, sasa endelea kuichokonowa hiyo package uone itakavyo kuchachaia!
Just be careful what you wish woman, yatakayokukuta utajuta...🙁😡😕
 
Nawasalim wapendwa
Uzi huu unawahusu wanandoa au vijana walioshika dini sna, kiasi kwamba wao hawana habar na mambo yanayoendelea dunian.
Kama, unywaji pombe, kuchepuka, kupenda starehe na company, kupenda music wale ambao wamejitoa maisha yao yote kumtumikia Mungu.

Mume wangu ni mtu wa aina hiyo, kwakweli nashukuru Mungu hatujawah kuzozana habar za kutoaminiana tunaishi kwa aman na furaha tele sababu wote tumekutana tuna hofu ya Mungu.

Tatizo ni moja tu, ambalo linaniumiza mwenzangu hayupo romantic kabisaaa, kwa mfano
1) unaweza ukammiss au ukawa unahamu kuchat na mpz wako kimahaba whatsup ukamtext, nimekumiss mume wangu au nakupenda na malove DAV meng yy akakujibu kwa ufupi tu ahsante mke wangu nakupenda pia..
Ukiendelea labda kumchombeza atakwambia nipo bize tunaongea nikirud, au unaweza ukamtex nimekumiss love akakupigia unasemaje mke wangu nipo bize nimechoka kutaype


2) akirud home ni mskajiwangu tutapiga story tutacheza karata na mambo mengi tu, tukiwa chumban ukitaka cjui kumchezea au kumsumbua sumbua kimahaba anakwambia wife niache nipumzike nimechoka kuna siku aliniambia mke wangu ww ni msumbufu kama unataka c useme nikupe mm nilale nikamwambia ndio nataka basi akanipa unyumba akalala.
Yaan kwa kifupi hana muda na mapenz kwake tendo LA ndoa c lazima yupo bize na famila na mambo ya kanisan na kazi zake.

Kiukweli wanawake sometimes tunapenda kubendelezwa kupetiwa petiwa na kupewa raha,

Sio kwamba kabadilika Ila ndivyo alivyo, na sio kwamba sio mwaminifu ila hayupo hivyo.
Ukitaka unyumba ujirengeshe akupe then mlale mnaweza mkalala pia unamwambia nikumbatie anakwambia mm sipat usingizi mpaka nijifunike shika nilalalie tumbo basi atakjfurahisha dk 5 then anakwambia nataka nilale hiyo anavuta shuka mpaka asbuh.

Nifanyaje niweze mbadilisha mume wangu, awe romantic namm nifurahie mapz, mengi nimejitahid amebadilika lakin kwenye mapz ndo mtihan.

NB:Sihitaji ushuri wa kuambiwa chepuka,

sio wanaume wote kwenye ndoa zao wanachepuka wengine wanajiheahimu na wana hofu ya Mungu,

Na sio kila mwanamke mzur akiwa na chngamoto kwenye ndoa yke solution ni kuchepuka, muda mwingine inabid utafute ufumbuz wa tatizo ili uzidi kujenga nyumba yko.


Sent using Jamii Forums mobile app
Wanaogopa kupata dhambi wakiwa romantic...
Nilimsikia mlokole mmoja hivi anasema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mshukuru Mungu hata huyo ni best friend wako anakusikiliza
Kuna walokole wanawadunda adi wake zao na ibada inapanda kama kawa ila ndani ni paka na panya
Mbebe huyo kama alivyo as you go on kumwelewesha taratibu ipo siku ataelewa
Usiforce kumbadili asije akabadilika gafla akaanza kukutia tena mashaka na wewe ukaja hapa kuanzisha thread ingine
 
No body is perfect hapa duniani, hiyo ni kasoro yake hivyo maamuzi ni yako kumbadilisha awe unavyotaka au umkaushie.
 
Sasa ulivyo mwambia "nimekumiss mume wangu au nakupenda" ulitaka akujibuje zaidi ya hivyo? "Ahsante mke wangu nakupenda pia" mimi naona alikujibu vizuri tu sasa wewe sijui ulitaka ujibiweje zaidi ya hapo eti,
Hata mimi ukinisumbua nikiwa kazini ukianza kunitext lazma nitakuona msumbufu, "pesa kwanza mapenzi baadae", ndio nyie wenyewe pesa zikiyumba kwa mwanaume nyie nduki,
Na kuhusu tendo la ndoa mfano mimi nimetoka kazini nimechoka kupita kiasi unataka nifanyeje sasa, utatakiwa usubiri hadi siku nitakapo kuwa 4G, 🙈
 
Atakuwaje romantic wakati anasali pentekoste pengine aanze kusali Roman catholic ndio atakuwa Romantic kwasababu romantic na Roman vinaendana
 
Back
Top Bottom