Kwanini wanawake hamna huruma?

Kuna wanawake wafujaji na wanaopenda sifa yani Vimnwaga. Ukimjazia mavitu ndani anaanza kugawa gawa kwa majirani ili aonekane zimo.
 
Kulalamikia vitu kama hivi ni ushamba
πŸ‘‡
"Sidhani kama ni sawa kuandaa chakuala kingi, iwe mchana au jioni, kisha kinatumika kidogo, na kinachobakia kinatupwa,"

Je kwanini chakula kisiandaliwe kwa kiasi kulingana na uhitaji??
Je kwanini chakuala kitupwe?


Mleta mada ana hoja, ni baadhi ya wanawake/ wamama hawako makini na hawajui kufanya bajeti ya chakula kulingana na idadi yao au uhitaji wao.
 
Saingine uharibifu unakuwa kwa ajili mtu hajui uchungu wa hela inapatikanaje ila siku ukiachiwa shughuli uiendeshe hata kwa mwezi tu ndio utajua hujui.
 
Ni utetezi tu
 
Ukweli ni kwamba mtu yoyote ambae hatafuti hela kwa jasho, hua hajui kupanga matumizi.

Wasichana wa kazi na hawa wadogo zetu tunaoishi nao jamani sijui hua wanadhani sisi ni matajiri sana? Mtu atabandika MAJI YA KUOGA (na joto lote) kwenye jiko la GESI! Halafu anayasahau hapo yeye yuko chumbani na simu. Maji yatachemka wee mpaka yanakaukia we unapita unakuta maji yamebaki nusu, yeye hana habari, akikurupuka anajazia sufuria anaendelea kuchemsha! Au mwingine anachemsha maji, yakichemka anazima jiko anaenda kufanya shughuli nyingine. Akija anawasha tena jiko anayachemsha upya ndio akaoge!
TV ni masaa 24 ipo on, kuwe kuna mtu anaangalia au laa. Taa zote ni on hakuna anaezima.

Yaani kuna vitu vinakera sana mtu unaongea mpaka unachoka
 
Endelea kumfunza bila kuchoka.

wastani wa mtu hula robo. Japo wengine huwa hawafiki robo.
anzia hapo. kama mko wanne so ni mchele kilo moja tu au pungufu ya hapo.
 
Huyo mkeo ana ushamba fulani hivi, cha kufanya nunua mahitaji kwa wiki ( weakly basis), tena pungufu ya bajeti nzima, kama robo tatu hivi, utajionea
 
Kwakweli inauma si kidogo,

Home kuna jiko la kuni,mkaa,gesi na mafuta,

Maji ya kuoga kwenye jiko la kuni huko, na kupikia huko hasa mchana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…