Kwanini wanawake hamna huruma?

Kwanini wanawake hamna huruma?

Hili nalo la msingi sana na nipo kwenye hatua za mwisho. Mke wangu ni mama wa nyumbani lakini tumekubaliana nimfungulie biashara, nataka asimamie kila kitu; kulipa Kodi, kununua mzigo n.k alafu mwisho wa siku tukae mezani kuona maendeleo ya biashara
Hapo safi...uchungu lazima aupate. Kipindi cha mwanzo wa biashara asitoe matumizi kabisa mpaka biashara isimame...isije kufa yakasingiziwa mahitaji ya nyumbani
 
Mkuu umeeleweka aisee. Lipo nililojifunza kiukweli tunakosea sana. Mungu atusamehe kwa haya makosa tunayofanya ndo maana katunyima mvua jamani. Lakini kuna mapoint mazuri sana humu. Kaa na mkeo chini ongea nae..kila kizuri kilichoandikwa humu na kitawafaa kibebe.

Na kama unaweza... weka kabisa ultimatum Kwamba hii ni ya mwisho hutarudia kusema tena. Then baada ya hapo kama hakutakuwa na mabadiliko chukua likizo kazini ama jifanye mshahara umesimamishwa kabisa. Kwa kosa ambalo na wewe umeshiriki. Itawaumiza na watoto lakini kama unataka somo lieleweke huna budi kulisimamia ukucha.

Kwenye huo mwezi itabidi breakfast ziwe viporo na sometimes mchana papite kiugumu. Wewe utajua tu namna ya kulisongesha maana wewe ndo kichwa. Nakumbuka bimkubwa kuna siku tulipika pilau sikukuu tukasahau kuhifadh kwenye friji. Tukakuta pilau limenata. Aah wee yule mchaga alitunyoosha. Tulikula asubuh, mchana, jion na hatukuhara wala nn hata kama mdomon mambo yalikua si mambo.

Kuanzia siku iyo somo tulielewa. Na hakujali mkubwa wala mtoto. Kwaiyo kuna muda ili heshima iwepo lazima darasa lipite. Hata Mungu huwa anatuadhibu kwa mapenzi si kwa ajil ya kutuangamiza. Wewe ndo kichwa..simamia misingi wala hujakosea. Big up!!
 
Pole mkuu, ongea kwa vitendo, pangeni bajeti ya mwezi ama nusu mwezi then mkabidhi pesa za jikoni, wewe usinunue kitu muachie hilo jukumu yeye. Matokeo utayaona kwa uharaka zaidi
Huyo ana tabia ya ufujaji sugu...usikute hata anagawa kwa kujiona yupo pazuri..na bora angegawa kwa wenye uhitaji zaidi.
 
Toa agizo wawe wanapika mchele kilo moja au moja na nusu daily,Kuna wakati kwangu nilikuwa nanunua mpaka kg 5o kwa mwezi,nilikuja kuuliza rafiki yangu mwenye familia Kama yangu akaniambia anatumia kg 14 nilichoka,nikamwambia wasipike Zaid ya kg moja per day
 
Yaani....! Kuna wakati bajeti yetu kwa mwezi ilikuwa lita5, siku moja nikaamua kupelekea ndoo ya lita10 mwezi mmoja ikakata 🤣
Daah kutokana na maelezo yako hayo,ebu fanya uchunguzi WA kiaina huenda mkeo anagawa baadhi ya vitu Kwa jirani au nduguze

Haingii akilini bajet ya mafuta Lita 5 halafu ulivyoleta Lita 10 zote zikaisha,that means ukileta Lita 15 nazo zinaisha hahahah

Nasema hayo kwakuwa Nina uzoefu na Bibi yangu mzaa Baba, yeye bwana analetewa mazagazaga yote lkn bwana huwa anagawa chakula ovyo ovyo Tu

Sasa wengine hufanya hivyo kuonyesha yeye mambo Safi au huruma iliyopitiliza ambayo ina kukosti wewe.

Naomba hili nalo usili dharau,huenda chakula kinaenda Kwa shoga yake au jirani zake
 
Memtata naona umeona HOPECOMFORT alipozungumzia juu ya kiporo kufanyiwa kazi siku inayofuata

Ndivyo hata Mimi ninavyojua,umebaki wali usiku basi asubuhi mnapita nao na chai,hakuna kununua vitafunwa,huo utaratibu ni mzuri Sana unaweka nidhamu ya kuepuka kutupa chakula.

Mimi na mke wangu bwana nashukuru wote tulikutana hatupendi huo upuuzi,Yan hata kama labda niliacha maagizo nitakula mchana then ikatokea sikurudi on time,ujue huo ugali yupo tayar aule yeye na asile wali usiku huo ili mradi chakula kisitupwe au ujue kesho utakorogewa na kusongwa tena.

Kwahiyo mkuu pambana Sana hiyo Tabia iishe kabisa,ukiwa kama msimamizi WA familia usikubali kuingia dhambini Kwa kuchezewa chakula.

Kila la kher mkuu
 
Back
Top Bottom