Kwanini wanawake hamna huruma?

Kwanini wanawake hamna huruma?

Mkuu umeeleweka aisee. Lipo nililojifunza kiukweli tunakosea sana. Mungu atusamehe kwa haya makosa tunayofanya ndo maana katunyima mvua jamani. Lakini kuna mapoint mazuri sana humu. Kaa na mkeo chini ongea nae..kila kizuri kilichoandikwa humu na kitawafaa kibebe.

Na kama unaweza... weka kabisa ultimatum Kwamba hii ni ya mwisho hutarudia kusema tena. Then baada ya hapo kama hakutakuwa na mabadiliko chukua likizo kazini ama jifanye mshahara umesimamishwa kabisa. Kwa kosa ambalo na wewe umeshiriki. Itawaumiza na watoto lakini kama unataka somo lieleweke huna budi kulisimamia ukucha.

Kwenye huo mwezi itabidi breakfast ziwe viporo na sometimes mchana papite kiugumu. Wewe utajua tu namna ya kulisongesha maana wewe ndo kichwa. Nakumbuka bimkubwa kuna siku tulipika pilau sikukuu tukasahau kuhifadh kwenye friji. Tukakuta pilau limenata. Aah wee yule mchaga alitunyoosha. Tulikula asubuh, mchana, jion na hatukuhara wala nn hata kama mdomon mambo yalikua si mambo.

Kuanzia siku iyo somo tulielewa. Na hakujali mkubwa wala mtoto. Kwaiyo kuna muda ili heshima iwepo lazima darasa lipite. Hata Mungu huwa anatuadhibu kwa mapenzi si kwa ajil ya kutuangamiza. Wewe ndo kichwa..simamia misingi wala hujakosea. Big up!!
Asante sana mkuu, hakika kufunguka kumenisaidia nimetoka na madini ya kutosha leo
 
Toa agizo wawe wanapika mchele kilo moja au moja na nusu daily,Kuna wakati kwangu nilikuwa nanunua mpaka kg 5o kwa mwezi,nilikuja kuuliza rafiki yangu mwenye familia Kama yangu akaniambia anatumia kg 14 nilichoka,nikamwambia wasipike Zaid ya kg moja per day
Kwangu wanapiga 35-40kg kwa mwezi lakini kwa rafiki yangu (baba Alice) ananiambia 50kg zinafika hadi miezi mitatu na ukubwa wa familia kama sawa.
 
Daah kutokana na maelezo yako hayo,ebu fanya uchunguzi WA kiaina huenda mkeo anagawa baadhi ya vitu Kwa jirani au nduguze

Haingii akilini bajet ya mafuta Lita 5 halafu ulivyoleta Lita 10 zote zikaisha,that means ukileta Lita 15 nazo zinaisha hahahah

Nasema hayo kwakuwa Nina uzoefu na Bibi yangu mzaa Baba, yeye bwana analetewa mazagazaga yote lkn bwana huwa anagawa chakula ovyo ovyo Tu

Sasa wengine hufanya hivyo kuonyesha yeye mambo Safi au huruma iliyopitiliza ambayo ina kukosti wewe.

Naomba hili nalo usili dharau,huenda chakula kinaenda Kwa shoga yake au jirani zake
Tunapoishi ni mbali kabisa na familia zetu labda kama anagawa kwa mashoga zake na kwa majirani zangu sina shaka nao sababu ya life style zao. Lakini nisitoe majibu mapema nitalifanyia kazi pia
 
Memtata naona umeona HOPECOMFORT alipozungumzia juu ya kiporo kufanyiwa kazi siku inayofuata

Ndivyo hata Mimi ninavyojua,umebaki wali usiku basi asubuhi mnapita nao na chai,hakuna kununua vitafunwa,huo utaratibu ni mzuri Sana unaweka nidhamu ya kuepuka kutupa chakula.

Mimi na mke wangu bwana nashukuru wote tulikutana hatupendi huo upuuzi,Yan hata kama labda niliacha maagizo nitakula mchana then ikatokea sikurudi on time,ujue huo ugali yupo tayar aule yeye na asile wali usiku huo ili mradi chakula kisitupwe au ujue kesho utakorogewa na kusongwa tena.

Kwahiyo mkuu pambana Sana hiyo Tabia iishe kabisa,ukiwa kama msimamizi WA familia usikubali kuingia dhambini Kwa kuchezewa chakula.

Kila la kher mkuu
Hayo ndiyo maisha niliyokulia mimi, nilitaka kukata tamaa na kujihisi labda mimi nna mawazo ya kimasikini ndomana naumia lakini nimepata nguvu mpya. Shukran
 
Memtata naona umeona HOPECOMFORT alipozungumzia juu ya kiporo kufanyiwa kazi siku inayofuata

Ndivyo hata Mimi ninavyojua,umebaki wali usiku basi asubuhi mnapita nao na chai,hakuna kununua vitafunwa,huo utaratibu ni mzuri Sana unaweka nidhamu ya kuepuka kutupa chakula.

Mimi na mke wangu bwana nashukuru wote tulikutana hatupendi huo upuuzi,Yan hata kama labda niliacha maagizo nitakula mchana then ikatokea sikurudi on time,ujue huo ugali yupo tayar aule yeye na asile wali usiku huo ili mradi chakula kisitupwe au ujue kesho utakorogewa na kusongwa tena.

Kwahiyo mkuu pambana Sana hiyo Tabia iishe kabisa,ukiwa kama msimamizi WA familia usikubali kuingia dhambini Kwa kuchezewa chakula.

Kila la kher mkuu
Umezungumza vyema kaka
 
Nyie vijana bwana, hii slogan yenu ya "tafuta pesa" nani kawafundisha? Fikirisha ubongo wako mkuu, elewa alichoandika ndio utoe hoja, au huna majukumu mzee?
Mwandishi ndo kijana kama sio mtoto, ameshindwa kutiisha familia yake anatafuta faraja jamvini….. umri sio miaka.
 
Ulishawahi kutoka na mwanamke wa mjini sister du fulani out? Akiletewa menu anaagiza nusu kuku na chips alafu anakula kiupaja kimoja na vichips kadhaa anajifuta na tishu kwa mikogo vingereza vingi alafu anakwambia ameshiba! 🤔

Wanaume tumeumbwa mateso hadi kwenye ndoa yanatukuta haya. Leo naongelea wanawake walioolewa au wanaoshi na wanaume kama familia, kwanini wengi wao wana tabia hii? KUTUPA CHAKULA!!! 😭

Nikijitolea mfano mimi binafsi nimetoka familia masikini, Mungu kanijaalia nna kipato cha kubadilisha mboga kwa sasa. Kwakuwa chanzo kikuu cha mapato ni mshahara basi huamua kununua vyakula vya jumla kila mwisho wa mwezi mf. mchele,unga, mboga kama maharage, dagaa, samaki, nyama ya ng'ombe, kuku n.k yani kiufupi mwisho wa mwezi friji inakuwa top kwa mazagazaga na huwa tunapanga kabisa na mke wangu anunue vitu kiasi gani lakini matumizi ya vitu hivi yanakuwa ya hovyo sana hadi kupelekea kitu fulani kuisha mapema kabla ya muda mliojiwekea. Na hata ukimuuliza kuhusu pesa ya matumizi uliyompa tofauti na ya manunuzi ya vitu hivyo utaambulia patupu.

Kuna jambo wanawake hawawezi kubajeti kabisa hasa kipimo cha chakula. Unakuta mchana wanapika ugali mkubwa hadi jioni unatoka kazini unakuta hotpot limejaa ugali na mboga kibao zimebaki wote wameshakula na mimi huwa sili nyumbani mchana siku za kazi. Usiku pia wanapika wali kibao unabaki, asubuhi hauliwi wote sababu kuna mkate au mwanamke kajisikia kupika tambi au chapati, mchana unakuta sufuria limelowekwa na mpunga kibao mwisho wa siku wanapewa kuku wale....

Nimeongea kwa ujumla wanawake maana hiki ni kilio cha wanaume wengi tunaofatilia mambo ya jikoni. Siwafichi mimi huwa nafatilia mambo ya jikoni.

Nna rafiki zangu wengi, ndugu zangu na jamaa wanaoishi maisha ya shida sana, mfano jana nilipigiwa simu na rafiki yangu ananiambia hadi muda huo (saa 2 usiku) hajajua watoto watakula nini akaniomba nimsaidie kumtumia buku mbili tu japo anunue mkate. Si kwamba napesa nyingi lakini najua uhalisia wa anachoniambia sababu haya maisha nimeyaishi nilipambana nikamtumia hela ya kula siku hiyo.

Nikirudi kwa mke wangu mimi hajali kabisa unaweza kushangaa baada ya siku 15 tu anakwambia mchele karibia unaisha, namuuliza mmetumia mchele kilo 30 kwa siku 15?! Jibu lake rahisi anajibu 'unadhani mimi naumwaga, si watoto wako wanakula!' Mwanamke mwenyewe katoka familia hizi hizi kama zetu sijui kwanini hana uchungu!

Lakini si wote kuna wanawake wanajua kubajet aiseee... Kama shemeji yangu mama Alice nakumbuka wakati huo tunaishi nae nyumba moja na mume wake(rafiki yangu). Huyu mwanamke hatumii kwasababu vipo tu, nisiseme mengi.

Kama kusema nilishasema sana sasa hivi naumia tu maana ukizidi kuongea hawachelewi, utasikia "We mwanaume una gubu kweli, mambo ya jikoni yana kuhusu nini?"

Ah! Basi bana, namwachia Mungu 😢
Mwanamke asiye jielewa hufanya hivi .lakin kwa ushauri kaa na mke wako muambie hiyo tabia huipendi ya kumwagwa chakula. Kuna wakat mnaeza kukosa hiko chakula.
 
Back
Top Bottom