MFALME WETU
JF-Expert Member
- Feb 1, 2021
- 4,071
- 10,028
Ughonile..
Nina mpenzi wangu mmoja juzi katoka mkoa kuja kunitembelea ikabidi nilipie room hotelini tukaekae siku kadhaa then kila mtu aendelee na mambo mengine ya kujenga taifa.
Mimi ni mtu wa pilikapilika muda mwingi niko bize so alivokuja nikamwambia leo hatutaweza kuonana akakubali japo kishingo upande kwa maneno kibao mara bora arudi zake tu mimi sina time nae na blaablaa kibao ikabidi nimrudishe kwenye mfumo, nikatuma Taxi kwenda kumchukua hadi hotelini kwa miyadi ya kukutana kesho yake maana iyo siku nilikua occupied kidogo.
Alifika mida ya mchana, kwenye kuchatichati akanambia hana hela yoyote hata ya kula nikamwambia mimi pia sina atumie tu yakwake nikija ntamrudishia akasema hela ipo kwenye laini yake ya Lipa Namba kashamtumia mama yake hela kiasi so hawezi kutoa tena kuepuka makato makubwa. Moyoni nikajisemea huyu hanijui vizuri 😀
Nikamwambia mimi pia sina hela yoyote leo pesa yote ipo kwenye fixed account, akasema basi atashinda tu njaa nikamjibu poa akidhani natania maana kama ni hela anajua kweli ninayo namimi nilikua nawaza ivoivo alivokua anawaza yeye.
Hamuezi amini yule dada alishinda njaa na kulala njaa kisa kuepuka makato, kesho yake navoenda kumcheki asubuhi nakuta kachoka balaa ananambia hajala chochote tangu alivokuja aisee nilijisikia vibaya ukizingatia anasumbuliwa na vidonda vya tumbo pia, ilinifikirisha sana inakuaje mtu anashindwa kulipia chakula kisa makato au tozo.!!?
tulivoshuka kwenda resta kula akaenda moja kwa moja kwa wakala kutoa kiasi cha 150,000/= taslimu kwa madai kuwa jana yake nilishindwa kumjali so bora alipe bills zake mwenyewe.
Nishakutana na cases kibao za wanawake wa design iyo kwenye mahusiano ila hii ya huyu mpenzi wangu imeniacha dilemma, mwenye kujua sababu atuambie