Kwanini Wang Yi ameichagua tena Tanzania kuwa miongoni mwa nchi za ziara yake ya Afrika ya 2026

Kwanini Wang Yi ameichagua tena Tanzania kuwa miongoni mwa nchi za ziara yake ya Afrika ya 2026

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,310
Reaction score
1,265
tyTLgJRfdHaknC7q.png


Kwa mwaka wa 36 mfululizo sasa, Afrika imekuwa ikiangaliwa kwa jicho la udugu na China na kuteuliwa kuwa kituo cha kwanza katika ziara ya nje ya nchi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China kila mwaka unapoanza. Desturi hii ya kidiplomasia inaeleza kwa kinywa kipana kwamba uhusiano baina ya China na Afrika una umuhimu mkubwa wa kimkakati.

Kuanzia Januari 7 hadi 12, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi alianza kutembelea baadhi ya nchi za Afrika zikiwemo Ethiopia na Tanzania na kwa mujibu wa mpango wa awali Somalia pia ilikuwa itembelewe, lakini baadaye yakaja mabadiliko ghafla. Kama ziara ya Somalia ingefanyika, ingekuwa ziara ya kwanza nchini humo tangu miaka ya 1980. Hata hivyo maafisa wa Somalia wanasema wanatarajia ziara hiyo kufanyika katika siku za mbeleni, ila hawakutaja ni siku gani. Waziri Wang alihitimisha ziara yake hiyo kwa kutembelea nchi ya Kusini mwa Afrika, Lesotho.

Kawaida China inapoteua nchi za kutembelea huwa inaweka uwiano, kwani inahakikisha inafanya ziara katika pande zote za Afrika, ikijali nchi kubwa na ndogo, mfano mzuri ni Lesotho, hii ni nchi ndogo zaidi katika Afrika, ambayo mwaka jana ilipata pigo la kuongezewa ushuru mkubwa na Marekani.

Safari hii ziara ya Wang ilianzia nchini Ethiopia ambako alikwenda kuhudhuria sherehe ya uzinduzi wa Mwaka wa Mawasiliano baina ya watu wa China na Afrika katika makao makuu ya Umoja wa Afrika huko Addis Ababa. Wakati mwaka huu wa 2026, China na nchi za Afrika zinaadhimisha miaka 70 ya kuanza kwa uhusiano wao wa kidiplomasia hivyo ziara ya Wang barani Afrika imeonesha kwamba kuendeleza uhusiano na Afrika ni kipaumbele cha juu kwa diplomasia ya China.

Kwa Tanzania ambayo mwishoni mwa mwaka jana ilikumbwa na rabsha za hapa na pale na taharuki kubwa ambazo hazijawahi kushuhudiwa nchini humo hata mara moja baada ya Uchaguzi uliofanyika Oktoba 29, imefikiwa na mkono wa rehema wa China. Na hii yote ni kutokana na kudumisha uhusiano wao wa muda mrefu wa kidiplomasia, kiuchumi na kitamaduni.

Watu wengi wamekuwa wakijiuliza kwanini ndani ya kipindi kifupi tu, Bw. Wang Yi amerejea tena kwenye ziara yake ya mwanzo wa mwaka nchini Tanzania yaani kwenye mzunguko wa miaka minne au mitano tu. Hili si jambo la kushangaza hata kidogo, kwani hakuna asiyejua kuwa Tanzania na China zimekuwa zikishirikiana katika maeneo mbalimbali, ikiwemo biashara na uwekezaji.

Tukiangalia mwaka 2025 pekee, Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (Tiseza) ilisajili miradi 343 inayoungwa mkono na China, yenye thamani ya Sh trilioni 7.7 (dola bilioni 3.1) ambayo ilitoa nafasi za ajira zaidi ya 82,000.

Uwekezaji huo unahusisha sekta mbalimbali muhimu, ikiwa ni pamoja na viwanda, kilimo, huduma, usafiri, mali isiyohamishika ya kibiashara, mawasiliano ya simu na utalii. Lakini pia China imekuwa na ushirikiano mkubwa na Tanzania katika maendeleo ya miundombinu ya usafiri, ambayo yanaelezwa kuwa ni kichocheo muhimu cha ukuaji wa uchumi na ujumuishaji wa kikanda.

Isitoshe pia tunatakiwa kutambua kwamba sasa Reli ya Tazara inaadhimisha miaka 50. Reli hii inafanyiwa ukarabati na makampuni ya China, hivyo inachukuliwa kuwa na ushawishi mkubwa sana. Katika muktadha huu, Mamlaka ya Reli ya Tanzania-Zambia (Tazara) ilitajwa kama mojawapo ya alama za kudumu za urafiki na ushirikiano kati ya Tanzania, Zambia na China. Reli hiyo, ambayo ina urefu wa kilomita 1,860; kilomita 975 nchini Tanzania na kilomita 885 nchini Zambia, inabaki kuwa mradi muhimu unaoonesha miongo 6 ya ushirikiano.

Ethiopia, Tanzania na Lesotho ni miongoni mwa nchi 53 za mataifa ya Afrika zinazoshiriki kwenye pendekezo la China la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, na Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika. Kupitia mihimili hii miwili, kumekuwa na uwekezaji mkubwa wa miundombinu unaolenga katika kuboresha muunganisho wa dunia na biashara. Wakati nchi nyingi za Afrika zikitafuta uwekezaji na bishara badala ya mikopo inayosababisha ongezeko la madeni, vyombo hivi viwili vinazidi kukita mizizi yake barani Afrika.

Matokeo yake ni kwamba Afrika sasa inashuhudia kupanuka kwa miundombinu, maendeleo na kuongezeka kwa safari za kibiashara, upatiknaji wa rasilimali, na ushawishi wa kimkakati wa China.
 
China inaitazama Afrika kama ndiyo eneo pekee inayoweza kuiba rasilimali zake ili kuinufaisha nchi yake, na inafanya hivyo kupitia watawaka wasiojali maslahi ya watu wao.

China ikienda Ulaya inaenda kutafuta wawekezaji, ikija Afrika inajifanya mwekezaji!
 
Back
Top Bottom