Kwanini Wapalestina hawadai kuwa raia wa Israel tu na Itakuaje siku Wapelestina wakitaka kuwa taifa moja na Israel?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Katika mgogoro wa Israel na Wapelestina ni wazi mpango wa mataifa mawili kama umeshakufa kimya kimya. Fursa moja kubwa iliyobaki ni uwepo wa taifa moja lenye kujumuisha jamii zote mbili za Wayahudi na Wapalestina kama raia walio sawa katika taifa moja.

Inawezekana Siku moja Wapestina wakakubali haiwezekani tena kuwa na taifa lao tofauti na Israel na wakataka kuwa sehemu ya Israel?
Itakuaje wakitaka kuwa raia kamili wa Israel na watambulike rasmi kama raia wa Israel wenye haki zote za taifa la Israel?
 
Kijana punguza bangee ni hatari kwa afya yako Ulikuwa unataka kumaa'niniii hapo
 
Katika mgogoro wa Israel na Wapelestina ni wazi mpango wa mataifa mawili kama umeshakufa kimya kimya. Fursa moja kubwa iliyobaki ni uwepo wa taifa moja lenye kujumuisha jamii zote mbili za Wayahudi na Wapalestina kama raia walio sawa katika taifa moja.

Inawezekana Siku moja Wapestina wakakubali haiwezekani tena kuwa na taifa lao tofauti na Israel na wakataka kuwa sehemu ya Israel?
Itakuaje wakitaka kuwa raia kamili wa Israel na watambulike rasmi kama raia wa Israel wenye haki zote za taifa la Israel?
kama huna cha kuandika si lazima uje hapa na kuandika chochote, kaa kimya
 
Hata Egypt tu hawezi kukubali wa Palestine wavuke mpaka wa Philadelphia kule Rafar waingie Egypt wawe wakimbizi. Sembuse Israel kuungana na Palestine kuwa taifa moja!!!!!
Misri ni suala lingine kwa sababu kule wanaenda kama wakimbizi na kila taifa lina sera zake za kudhibiti uhamiaji ila hapo walipo sasa hivi ni ardhi yao inagombaniwa na hawatambuliki rasmi kama taifa ila wako chini ya udhibiti wa Israel, sasa kwa nini wasiamu tu pote pawe Israel na wao wawe raia kamili wa Israel??
 
Wakati wa Herode the Great, walikuwa kama jamii moja, pengine huenda kuna siku Likawezekana hilo.
Ni jambo linalowezekana sana ikizingatiwa kama kila mmoja hatalazimisha tamaduni zake juu ya jamii nyingine.
 
Katika mgogoro wa Israel na Wapelestina ni wazi mpango wa mataifa mawili kama umeshakufa kimya kimya. Fursa moja kubwa iliyobaki ni uwepo wa taifa moja lenye kujumuisha jamii zote mbili za Wayahudi na Wapalestina kama raia walio sawa katika taifa moja.

Inawezekana Siku moja Wapestina wakakubali haiwezekani tena kuwa na taifa lao tofauti na Israel na wakataka kuwa sehemu ya Israel?
Itakuaje wakitaka kuwa raia kamili wa Israel na watambulike rasmi kama raia wa Israel wenye haki zote za taifa la Israel?
Waarabu ambao wapo Israel sasa hivi wanabaguliwa, asilimia 20% ya Waisrael ni waarabu, in short hapo mpaka damu imwagike sana ndio respect itapatikana.

Mifano ya ubaguzi
1. Wanawatenga waarabu Hospitali

2. Waarabu wengi hasa wakristo wakipita mitaani wanatemewa mate

3. Shule zao ni tofauti most of time hawaruhusiwi kusoma na wayahudi

4. Wana passport na vitambulisho tofauti ambavyo habiwapi access ya vitu vyote kwenye nchi

Long story short waarabu Israel ni second Citizens,
 
Misri ni suala lingine kwa sababu kule wanaenda kama wakimbizi na kila taifa lina sera zake za kudhibiti uhamiaji ila hapo walipo sasa hivi ni ardhi yao inagombaniwa na hawatambuliki rasmi kama taifa ila wako chini ya udhibiti wa Israel, sasa kwa nini wasiamu tu pote pawe Israel na wao wawe raia kamili wa Israel??
Nielewe vyema ndugu yangu haiwezekani kabsa
 
Katika mgogoro wa Israel na Wapelestina ni wazi mpango wa mataifa mawili kama umeshakufa kimya kimya. Fursa moja kubwa iliyobaki ni uwepo wa taifa moja lenye kujumuisha jamii zote mbili za Wayahudi na Wapalestina kama raia walio sawa katika taifa moja.

Inawezekana Siku moja Wapestina wakakubali haiwezekani tena kuwa na taifa lao tofauti na Israel na wakataka kuwa sehemu ya Israel?
Itakuaje wakitaka kuwa raia kamili wa Israel na watambulike rasmi kama raia wa Israel wenye haki zote za taifa la Israel?
Kwanini chadema hawataki kuwa wanachama wa ccm tu?
 
Hata Egypt tu hawezi kukubali wa Palestine wavuke mpaka wa Philadelphia kule Rafar waingie Egypt wawe wakimbizi. Sembuse Israel kuungana na Palestine kuwa taifa moja!!!!!
Wapalestina wapo Nchi zote za Kiarabu, hii ni myth ya kijinga inayosambazwa na watu wenye Allergy na kusoma Data.

Egpty kuna wapalestina zaidi ya laki 1.

Soma hapa kuona Population ya wapalestina nchi mbalimbali

Sijakataa! Wapo hata west na America...! Walienda huku sio kwa namna ambayo nimeieleza kuhusu Egypt
 
Waarabu ambao wapo Israel sasa hivi wanabaguliwa, asilimia 20% ya Waisrael ni waarabu, in short hapo mpaka damu imwagike sana ndio respect itapatikana.

Mifano ya ubaguzi
1. Wanawatenga waarabu Hospitali

2. Waarabu wengi hasa wakristo wakipita mitaani wanatemewa mate

3. Shule zao ni tofauti most of time hawaruhusiwi kusoma na wayahudi

4. Wana passport na vitambulisho tofauti ambavyo habiwapi access ya vitu vyote kwenye nchi

Long story short waarabu Israel ni second Citizens,
Huu utakuwa uongo mtupu na propoganda tu, hatujawahi kusikia raia Waarabu wa Israel wakilalamika kwamba wanabaguliwa au wamefanywa kuwa raia wa daraja la pili. Bunge la Israel pia lina limekuwa na wabunge waarabu tangu Israel iwe taifa mpake leo hii.
 
Kwanini chadema hawataki kuwa wanachama wa ccm tu?
Kwa sababu CHADEMA wanaamini bado upo uwezekano wa kuindoa CCM madarakani kupitia sanduku la kura.
 
Israel ni Jewish state kwa katiba yao!

Ukienda humo ukubali kuwa second grade citizen!

Ni kama apartheid ya South Africa wakati ule!

Israel Imekaa ki-fake fake sana , existence inategemea uungwaji mkono wa US!
 
Huu utakuwa uongo mtupu na propoganda tu, hatujawahi kusikia raia Waarabu wa Israel wakilalamika kwamba wanabaguliwa au wamefanywa kuwa raia wa daraja la pili. Bunge la Israel pia lina limekuwa na wabunge waarabu tangu Israel iwe taifa mpake leo hii.
Nimeweka link nayo ni propaganda? Nakuekea link hapa za kutosha na wewe unaweza weka link kuthibitisha?

1. Reuters

2. Human Right watch

3. Amnesty International

Vyote hivyo ni vyombo vya magharibi na vyote kwa pamoja vinakubali kinachoendelea Israel ni Apartheid. Siongelei Israel vs Palestina bali Israel vs Arabs Israel ambao wanaishi mule mule toka 1948.

Kama israel imeshindwa kuwatreat kwa haki raia wake waarabu almost miaka 100 sasa ina credibility ya kuanzisha taifa moja?
 
Back
Top Bottom