Kwanini wasanii hawamuigi Diamond?

umamtazamo tofauti sana ktk tasnia hii utakua hujui muziki

sio lazima wasanii wote wawe na dancers sio lazima wasanii wote wavae kisharobaro, sio lazima kua kama Diamond ili kutoboa kimataifa

Wizi Kid techno Davido hawafanani kwa lolote na Diamond ila niwasanii wakubwa

soDiamond amepitia njia yake na kuna njia nyingi kama 1000 za kupita ili kua msanii mkubwa

Ali Kiba,Vanessa Mdee na Navy Kenzo wanaweza kufika mbali sana hata zaidi ya Diamond wakiwekajitihada kwa namna zao.

I support Diamond ila sijapenda mtazamo wako ktk hili
 

Wenzie wanafanya bidii sana ashuke kisanii awe kama wao wamcheke na waseme ''si tulisema sisi!'.
Wasanii wenyewe wanachukiana mpaka kuendeana kwa waganga kizuri wataiga vipi!?Ona walivyomsema Mavoko wakati akienda WCB,lakini walau karudi sokoni.
hawaamini kwenye kua na Diamond na Kiba wengi,ila wanatamani lazma wamshushe mmoja ili wachekane na uduni wao!
 
Cha muhimu ni wao kuridhika na walipofikia na wao kuwa wao [being themselves].

Kama nimekuelewa vema mkuu,hapa pana shida kubwa.'Kuridhika' ni subjective so naweza kua nakosea lakini kama ni kwa maana hii nilioelewa 'wakiridhika na walipofikia' muziki huu ndo unakufa kabisa kama Bongo Movie baada ya kifo cha Kanumba.
Atleast wafanye bidii na kuiga the basics kama promo za nguvu(bila scandal..well..kutegemea personality ya mtu), kukamata fursa inapoibuka(majina na umaarufu wao uwasaidie),breaking new markets(kule muziki wetu haujafika bado through collabos na vitu kama hivyo).
...they can atleast copy a thing or two wakavi channel kwenye njia zao binafsi na wamuache na ma scandal yake...sababu dogo ndo kama nembo ya msanii aliefanikiwa zaidi hapa kwetu kwa sasa!
 
Wasanii wengi wa bongo wanazidiwa Akili na Diamond sana tena sana,,huyu dogo akili kubwa sana yani kama angefanikiwa kuendelea kusoma naamini angekuwa na PHD kama sio docta kabisa, sababu najaribu kufikiri baadhi ya kazi zake za mziki ufundi anaoutumia kuandika nyimbo zake na hata ile kujua tu huu wimbo utakmata mtaa.. Niliwahi kumsikia ney wa mitego pamoja na utata wake ule alisema siku ambayo amefanya kazi na diamond alikiri wazi kwamba dogo anajua sana mziki

Halafu ukija kuzungumzia alivo kuwa na vision ya mziki aliwahi kusema pia anataka tufike na sisi tufanye show za Dollar elf 30 kama kina psquare,hapo ni wakati huo anaanza kutoka kimziki leo tunaongelea show ya mill100.

Na ukiangalia kwa namna Diamond alivokuwa kipindi hicho anaanza kutoka utaona wazi kwamba macho yake yalikuwa kwa Psquare namna wanavovaa na dansi zao zile kwenye Show kwa hiyo kuiga kwenye mziki ni njia ya mafanikio naye leo amefanikiwa pamoja na kuiga huko.
Haya tukaja kwenye kutengeneza timu ,wasanii wengi hata marekani wana team kubwa ya watu kuanzia manager, organizer, stylist, photographer,make up artist, video director na wengine wengi tu,hapa bongo kuna siku niliwahi msikia msanii akisema manager wa nini na kwanini niwe na team kubwa gharama tu. Lakin Diamond kaweza kuwa na team(hapa ndio namuona dogo kichwa kwa uthubutu)na amefanikiwa.

Pia tukubali tukatae dogo kabadili mziki wa bongo kwa kiasi kikubwa sana wengi walikuwa hawajitambui enzi hiyo hawajui thamani yao malipo ya shows zao sasa yako vizuri..lakini nijitihada zote za dogo.

Mwisho sijaweza kung'amua mpaka sasa kujua ni nani atakuja kuwa the Next Diamond in Bongo maana kijana anavotusua kila leo na hata dalili za kushuka sizioni na wengine hawatokei wa kucompete ,basi tunamuacha tu aendelee kushika chati. Maana hakuna namna.!!
 
Wakati mwingine inakuwa too much. Leo una huyu na kesho yule...sasa utawatamvukisha wangapi. Unaweza kuina kama Wolper kila anayempata anatangazia watu ndiys wa ndoto zake. Muda kidogo wanekorofishana. Anapata mwingine anarudia usemi huo. Na hii ni kwa wasanii wengi hata kama akina Shilole. Bora mtu akae kimya maana maana inakuwa si vizuri we kila siku ninkutambulisha wachumba. Mwishowe unaionyesha jamii kwamba una matatizo ndo maana unaachana na wapenzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…