Kwanini wasanii wa Bongo hawajui kujieleza?

Hivi maana kujua kujieleza ni ipi? Kwa sababu naona kila mtu anaeleza kivyake wengine wanahusisha kujieleza na usomi kwamba watu hawana elimu ndio hawajui kujieleza,wengine wanaona kujieleza ni kipaji na wengine wamefika mbali zaidi kusema watanzania hawajui kujieleza.
 

Vilevile kusoma vitabu....
Kiongozi asiyesoma vitabu hata kujieleza na kujibu hoja mbalimbali utashangaa anavyopwaya....

Angalia Magufuli, jinsi hata kujieleza kwa Kiswahili ilivyo shida.
Yani akiongea mpaka mwenyewe ndio unaogopa asikosee huku ukijawa na wasiwasi mkubwa kuwa lazima atachapia au kuvuruga.

Lkn ukiona jinsi Zitto na Lissu wanavyojieleza na kupangua hoja unajua hawa watu wanasoma/kujisomea
 
Hotuba za Magufuli nimeacha kuangalia/kusikiliza kitambo sana.Labda nipate dondoo tu.

Asipomnyanyapaa mkewe, atambashia mke wa Kikwete au kusema atawapiga shangazi za wapinzani.

Rais anaongea kama mgubegube gani ambaye hana heshima wala staha!
 
Tanzania bado kuna UJINGA SANA.

Watanzania bado Washambashamba sana
 
Maybe tatizo ni elimu na pia malezi. Mzazi pia inatakiwa ujaribu kumjengea mtoto wako confidence tangu akiwa mdogo. Maana suala la kujieleza ni janga la taifa.

Shule za wenzetu tangu wadogo kabisa kwenye miaka 3 na nusu wanapewa nafasi ya kujieleza mbele za watu. Mfano wanaambiwa waende shule na toy wanayoipenda.

Baadae mmoja mmoja anasimama mbele ya darasa na kuielezea hiyo toys yake. Hiyo ni moja ya mbinu mtoto awe na uwezo fulani wa kujieleza. Nyumbani mzazi anakuwa mkali mpaka mtoto anaenda zake chumbani
 
nifanye nini nisiwe na yote haya??
Mara nyingi matatizo katika kujieleza yanaonesha matatizo katika kufikiri.

Hususan, kukosa uwezo wa kufikiri kwa kina, au kutojali habari za kufikiri kwa kina.

Sifikiri kwamba hatuna uwezo wa kufikiri kwa kina. Hakuna sababu ya kunifanya nikubali hilo. Naona kama tumekubali utamaduni wa kutofikiri kwa kina.

Wengi tunatakiwa kubadilika kwa angalau haya.

1. Kufikiri kabla ya kusema. Ni rahisi kuharibu kujieleza kama tunasema sana bila kufikiri.

2. Kujali wengine sana. Ukijali wengine, utaweza kufikiri sana jinsi ya kujieleza mpaka wakuelewe vizuri. Kwa mfano, ukiongea na mtoto, ukimjali, utataka kuongea kwa njia ambayo mtoto atakuelewa. Ukimuelezea mtoto kwa lugha ambayo imekaa kikubwa utamchanganya. Mara nyingi makosa katika kujieleza yanaonesha mtu anayejieleza kutojali wanaomsikiliza.

3.Kujifunza kujieleza kutoka kwa watu maarufu waliofanikiwa kuweza kujieleza kwa umakini. Kuna watu wana kipaji hiki. Ni muhimu kuwasoma.

4. Kusoma vitabu. Kusoma kunajenga mawazo na kupanua wigo. Kunatupa kanuni za msingi za kufuatilia na jinsi ya kuzihakiki.

5. Kutotaka kutafsiriwa vibaya. Ukiwa hutaki kutafsiriwa vibaya utaweka juhudi zaidi kujieleza vizuri. Kwa mfano, hata ukisema kitu, halafu ukagundua hakijamalizika au kina utata, utarudia ili kufanya masahihisho au maongezo. Hiki ni kitu ambacho wengi wetu hatufanyi.

6. Kumalizia sentensi. Jaribu kumalizia kila sentensi na wazo. Usidhani tu kila mtu anaelewa unachosema na anaweza kumalizia.

7. Kuelezea mambo kutoka mwanzo mpaka mwisho. Tuepuke kuanza kuelezea habari kutoka kati au bila hitimisho.

8. Kuuliza kama umeeleweka au kama kuna maswali. Mara nyingi mawasiliano ni kitu chenye utata, kwa sababu, hujui mwingine unayewasiliana naye ana uwezo gani, kaelewa nini, hajaelewa nini n.k. Hivyo, ni muhimu kumuachia nafasi na yeye ajieleze, kumpa muda wa kuuliza maswali na kuweza kuhakiki kwamba wote mnaelewana. Kuna watu wakianza kuongea wanataka kuongea wao tu bila kuwapa nafasi wengine.

9. Kuangalia "non verbal communication". Mambo mengine hayasemwi, unaweza kuona mtu anaangalia saa yake wakati mna maongezi ukajua labda unamchelewesha. Hapo unaweza kumpa nafasi ya kuaga kwa kumuuliza "Una miadi sehemu nini?"

10. Kusikiliza si tu kinachosemwa, bali hata ya kilichoachwa kusemwa. Ukimuuliza mtu swali moja, halafu asijibu hilo swali na kujibu lingine, unatakiwa kujua ama hajaelewa swali au anataka kuficha na kutojibu. Unaweza kuamua kuuliza swali tena ili kumpa nafasi ajibu, hususan kama unaona hajaelewa, au kuacha kuuliza kwa kuona anakwepa kujibu.
 
Niliwahi kuwa na tatizo la kuongea bila kujua wapi ninyamaze hadi nilipokutana na wacanada wawili ndo nkajua kumbe maongezi ni kama kuimba vile hivyo kupokezana ni muhimu.

Conversation is an art.
Hili tatizo tunalo sana.

Unakaa na mtu anahodhi maongezi kama Profesa Kabudi vile.

Kila ukitaka kutia neno anakukatisha anasema yeye.

Mwisho unaamua kumuacha aongee yeye tu.
 
Kivumishi Kielezi, Umegusa kitu muhimu sana.

Malezi ya watoto.

Tunashangaa sana inakuwaje mtu kasoma mpaka Ph.D halafu hajui kujieleza?

Ukichunguza utakuta alivurugwa tangu utotoni huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…